Friday, May 20, 2016
Dkt. Mahadhi Juma Maalim amtembelea Balozi wa Malawi Nchini Kuwait
Balozi Dkt. Mahadhi pamoja na mwenyeji wake Mhe. Ali wakiendelea na mazungumzo yao. |
UN YAWAENZI WALINZI WAKE WA AMANI WALIOPOTEZA MAISHA
Sehemu ya washiriki wa hafla ya siku ya Kimataifa ya Walinzi wa Amani wa Umoja wa Mataifa hafla hiyo ilifanyika jana Mei 19. |
=============================================
Na Mwandishi Maalum, New York
Umoja wa Mataifa, jana
Mei 19 umefanya hafla maalumu ya
siku ya Kimataifa ya Walinzi wa
Amani wanaohudumu katika Misheni mbalimbali za Kulinda Amani chini ya kofia ya
Umoja wa Mataifa.
Katika hafla hiyo
jumla ya walinzi 129 wanajeshi
na polisi waliopoteza maisha mwaka jana kwa kushambuliwa na makundi ya wapiganaji wenye silaha, matukio
ya kigaidi, ajali na kuumwa walikumbukwa
na kuenziwa kwa mchango wao.
Miongoni mwa Mashujaa
hao 129 kutoka nchi 50, wapo mashujaa watatu kutoka Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania. Mashujaa hao ni Sgt. Musa Abdrahamani Yusuf, Cpl. John Leornad
Mkude na Pte. Juma Ally Khamis.
Hafla hiyo maalum ya kutambua mchango wa walinzi
hao wa Amani na ambao wamejitolea
maisha yao kwaajili ya kuwalinda na kuokoka maisha ya wananchi
wasiokuwa na hatia katika
nchi zinazokabiliwa na vita na
migogoro ya wenyewenye kwa
wenyewewe iliongozwa na Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, ndiye aliyepokea medali maalum za mashuja hao
watatu kwa niaba ya familia zao. Medali waliyotunukiwa mashujaa hao na wengine inatambuliwa kama medali
ya Dag Hammarskjold.
Hafla ya mwaka huu, pamoja na
kutambua mchango wa mashujaa hao 129 ,
pia ilitambua kwa namna ya pekee na kwa
mara ya kwanza, mchango na kujitolea wa hali ya juu ulikofanywa na Kapteni
Mbaye Diagne raia ya Senegal,
aliyepoteza maisha mwaka 1994 wakati
akiokoa maisha ya wanyarwada
wakati wa mauaji ya kimbali.
Kapteni Mbaye Diagne ameeziwa
rasmi katika maadhimisho ya mwaka huu
kwa kupewa medali maalum iliyopewa jina la
Medali ya Mbaye Diagne, medali
ambayo alikabidhiwa mjane wa Mbaye Bibi
Yacine Mar Diop huku akishuhudiwa na
watoto wake wawili.
Kapten Mbaye Diagne alikuwa
mwangalizi wa Amani nchini Rwanda, kwa ushujaa mkubwa na bila ya kujali hatari iliyokuwa ikimkabili alitumia lori kuwaficha na kuwapeleka mahali
salama mamia ya wanyarwada wakati wa mauaji ya kimbali ya Rwanda.
Kwa kutambua ushujaa na
uthubutu wake huo, Baraza la Usalama lilibuni
mwaka 2014 medali ya Kapten Mbaye
Diagne ambayo watakuwa wanatunukiwa wanajeshi, polisi na raia ambao wameonyesha uthubutu na
ushupavu wa hali ya juu kiasi cha kupoteza maisha yao wakati wakitekeleza
majukumu yao.
Akizungumza wakati wa
halfa hiyo ambayo ilibeba majonzi ya aina yake,
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alieleza kwamba, hadi kufikia mwezi wa nne
mwaka huu, jumla ya walinzi wa Amani
3,400 wakiwamo wanajeshi, polisi
na raia walikuwa wamepoteza maisha tangu
kuanzishwa wa shughuli za ulinzi wa
Amani kwa kofia ya Umoja wa Mataifa
miaka 70 iliyopita.
“Wakati leo tunawaenzi
na kuwakumbuka mashujaa hawa 129 kutoka
mataifa 50 waliopoteza maisha yao mwaka
jana wakati wakitekeleza jukumu la kuwalinda wananchi wengine, jana ( Mei 18) walinzi wengine watano
wanaohudumu huko Mali wamepoteza maisha baada ya kushambuliwa”.
Akasema Ban Ki Moon kwa huzuni.
Thursday, May 19, 2016
Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki kutumika katika Taasisi za Serikali
Mkurugenzi wa Masomo katika Chuo cha Diplomasia Dkt. Watengere Kitojo (kushoto) pamoja na Afisa Mawasiliano wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Robi Bwiru. |
Bi. Mindi Kasiga akiendelea kuzungumza na Waandishi wa Habari. |
Sehemu ya Waandishi wa Habari waliojitokeza kwenye mkutano huo, katikati ni Afisa kutoka Habari Maelezo Bi. Immaculate Makilika akifuatilia kwa makini mkutano. ==================================================
Matumizi ya Alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inatoa wito kwa Taasisi za Serikali kuhakikisha kuwa zinatumia alama za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambazo ni Bendera na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Alama hizo zinatakiwa kutumika kwenye Ofisi za Serikali (Wizara, Idara zinazojitegemea, mashirika ya umma na Wakala) sambamba na alama za Taifa yaani Bendera ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wimbo wa Taifa.
Bendera ya Jumuiya inatakiwa kupepea sambamba na Bendera ya Taifa kwenye Ofisi za Serikali na Wimbo wa Jumuiya nao unatakiwa kuimbwa sambamba na Wimbo wa Taifa wakati wa shughuli rasmi za Kiserikali.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao katika kifungu cha 7(a) umesisitiza Jumuiya hii kuwa ni Jumuiya ya watu, hivyo wananchi wa Tanzania watahusishwa katika hatua zote za Mtangamano. Aidha, Serikali ya awamu ya tano (5) chini ya Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki itahakikisha kuwa Watanzania wanashirikishwa kikamilifu katika hatua mbalimbali za Jumuiya ili kuijua kwa madhumuni ya kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya Jumuiya hiyo.
Matumizi ya alama hizi ni njia mojawapo ya kujenga uzalendo na kumfanya Mwananchi ajisikie kuwa sehemu ya Ushirikiano huu. Aidha, Taasisi binafsi hasa Mashule na Vyuo wanasisitizwa kutumia alama hizi kama sehemu ya kuelimisha na kuhamasisha vijana kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki itaratibu zoezi la upatikanaji wa sampuli ya alama hizo kwa gharama za taasisi husika, hivyo Wizara, Taasisi na Ofisi za Serikali zinahimizwa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya ufafanuzi zaidi wa upatikanaji na matumizi ya alama hizo.
MAZUNGUMZO YA USULUHISHI WA MGOGORO WA BURUNDI
WAKATI HUOHUO, Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataongoza mazungumzo kuhusu mgogoro wa Burundi yanayotarajiwa kuanza tarehe 21 hadi 24 Mei, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa AICC – Arusha.
Katika mkutano wa 17 wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki walifafanua kuwa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni ataendelea kuwa msuluhishi kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki na kuteua timu ya Usuluhishi ambayo itaongozwa na Mhe. Benjamin William Mkapa.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Sekretariati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Waandishi wa Habari wataruhusiwa kwenye siku ya Ufunguzi wa Mkutano huo na siku ya kufunga Mkutano tu. Aidha, waandishi wanahimizwa kujisajili ili kupata vitambulisho vya kuingia kwenye mkutano. Usajili utafanyika AICC-Arusha tarehe 20 Mei, 2016 saa 8:00 mchana chumba namba 541, ghorofa ya tano, upande wa Kilimanjaro.
Au unaweza kutuma maelezo ya Press Card yako, picha ya ndogo (passport size) kwenye email ifuatayo; media@eachq.org, CC:oothieno@eachq.org.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 19 Mei 2016.
|
Press Release
PRESS
RELEASE
VACANCY
ANNOUNCEMENT FROM THE COMMONWEALTH SECRETARIAT
The Ministry of Foreign
Affairs, East Africa, Regional and International Cooperation has received
Application details can be
found on the Secretariat’s website, www.thecommonwealth.org.
Closing date for application is Tuesday 31st May, 2016.
“The Ministry encourages
qualified Tanzanians to apply”.
Issued by: The Ministry of Foreign Affairs and East
African Cooperation,
Dar es Salaam.
19th May, 2016
|
Wednesday, May 11, 2016
Balozi wa Tanzania nchini Kenya akutana na Balozi Austria nchini Tanzania
Subscribe to:
Posts (Atom)