Friday, August 26, 2016

Naibu Waziri akutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba  akisalimiana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Mhe. Zhang Ming walipokutana Nairobi  kwa mazungumzo ya kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China.  Mhe. Dkt. Kolimba pamoja na Mhe. Zhang wapo mjini humo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa TICAD VI utakaofanyika tarehe 27 na 28 Agosti, 2016.
Mhe. Kolimba akimweleza jambo Mhe. Zhang wakati wa mazungumzo yao.
Mhe. Zhang na ujumbe wake wakati wa mkutano na Mhe. Dkt. Kolimba (hayupo pichani)
Mhe. Dkt. Susan Kolimba akiwa na Waziri wa Fedha na Uchumi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Khalid Salum Mohammed (kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbelwa Kairuki (wa pili kutoka kushoto) na Bw. Adam Isara, Msaidizi wa Naibu Waziri.
Mhe. Naibu Waziri na Mhe. Waziri Mohammed pamoja na wajumbe wengine wakimsikiliza Mhe. Zhang ambaye hayupo pichani. Kulia ni Bi. Bertha Makilagi, Afisa Mambo ya Nje. 








Thursday, August 25, 2016

Mkutano wa TICAD kufanyika Afrika kwa mara ya kwanza

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya, Balozi Monica Juma (mwenye nguo ya kijani) akifuatiwa na Bw. Takeshi Osuga, Balozi wa TICAD kutoka Japan na  Mhe. Cherif Mhamat Zene, Balozi wa Chad, Ethiopia wakiongoza moja ya vika vya Maafisa Waandamizi ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Sita wa TICAD.
=====================================================================================

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkutano wa  6 wa Kimataifa kuhusu Ushirikiano wa Maendeleo kati ya Japan na Afrika (Tokyo International Conference on African Development-TICAD VI) unatarajiwa kufanyika tarehe 27 na 28 Agosti, 2016 Jijini Nairobi, Kenya. Hii ni mara ya kwanza kwa mkutano huu kufanyika nje ya Japan tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.

Mkutano huu wa Sita ambao umetanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu Wakuu na Mabalozi tarehe 24 na 25 Agosti, 2016 utafuatiwa na kikao cha Mawaziri tarehe 26 Agosti, 2016 unatarajiwa kupitisha Azimio la Nairobi ambalo litajikita katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazolikabili Bara la Afrika katika kufikia maendeleo na ustawi.

Changamoto hizo ni pamoja na kuporomoka kwa bei za bidhaa zinazotegemewa na nchi za Afrika katika ustawi wake kama vile mafuta, gesi na madini na hivyo kupelekea kuathirika kwa ukuaji wauchumi katika nchi nyingi za Afrika; kulipuka kwa magojwa kama Ebola na kusababisha vifo vilivyopelekea kusitishwa kwa shughuli za kiuchumi na kupotea kwa nguvu kazi; na Kuongezeka kwa vitendo vya ugaidi.

Agenda nyingine zitakazojadiliwa ni pamoja na: Kuhamasisha mageuzi ya kiuchumi kupitia uendelezaji wa viwanda; Kuboresha sekta ya Afya kwa maisha bora na Kusaidia jitihada za kudumisha amani na utulivu katika jamii.

Vile vile Mkutano huu umetoa kipaumbele kwa ushiriki wa sekta binafsi hususan wafanyabiashara na wawekezaji wakubwa kutoka Japan na Afrika. Hivyo mkutano utatoa fursa kwa taasisi zenye dhamana ya kuvutia uwekezaji, biashara na utalii nchini kutangaza fursa zilizopo kwa kampuni za Japan.

Mkutano huu wa 6 wa TICAD ambao unashirikiana kwa karibu na Kamisheni ya Umoja wa Afrika unalenga kuiwezesha Afrika kujitegemea katika kukua na kufikia maendeleo yaliyokusudiwa ikiwemo utekelezaji wa Agenda 2063 ambayo viongozi wa Afrika walikubaliana wakati wakuadhimisha miaka 50  ya Umoja wa Afrika. Agenda 2063  inalenga kuliunganisha Bara la Afrika katika masuala ya kukuza uchumi; kuhamasisha utawala bora na utawala wa sheria; kuhakikisha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja; kuhakikisha amani na usalama unaimarika na kuiweka Afrika kwenye nafasi ya mchangiaji mkuu wa uchumi duniani.

Mkutano wa kwanza wa TICAD uliofanyika Jijini Tokyo mwaka 1993 ulijikita zaidi katika agenda ya kuongeza misaada kwa nchi za Afrika. Kufuatia mkutano huo misaada ya Japan kwa nchi za Afrika iliongezeka kutoka Dola za Marekani bilioni 0.6 mwaka 1993 na kufikia Dola bilioni 0.8 mwaka 1998. Hadi kufikia mwaka 2013 msaada wa Japan (ODA) kwa nchi za Afrika ulifikia Dola za Marekani bilioni 2.8.

Mkutano wa 6 wa TICAD ambao kwa mara ya kwanza katika historia unafanyika Afrika utawezesha majadiliano ya ana kwa ana kati ya Wakuu wa Nchi na Wawakilishi kutoka Sekta binafsi.

Kadhalika, mbali na mwenyeji wa Mkutano huu ambaye ni Rais wa Kenya, Mhe. Uhuru Kenyatta mkutano utahudhuriwa pia na Waziri Mkuu wa Japan, Mhe. Shinzo Abe, Viongozi Wakuu kutoka nchi 54 za Afrika pamoja na wawakilishi kutoka mashirika ya kimataifa na makundi mbalimbali.

Ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huu utaongozwa na Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

-Mwisho-

 Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali
Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
25 Agosti, 2016





Wanadiaspora watembelea miradi ya maendeleo Zanzibar

Wanadiaspora wakipata maelezo kutoka kwa mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa nyumba zinazojengwa na ZSSF kwaajili ya makazi katika eneo la Mbweni Zanzibar 
Sehemu ya Wanadiaspora (watanzania waishio ughaibuni) wakitizama mradi wa nyumba za kisasa unaoendelea
Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania waishio Ughaibuni (Diaspora) waliohudhuria kongamano la tatu (3) la Diaspora lililofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.

Rais Magufuli apokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Waheshimiwa Mabalozi wa Canada, Thailand na Austria


Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Ian Myles akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Saalam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Balozi wa Kanada nchini Tanzania, Mhe. Ian Myles akiwasilisha Hati zUtambulisho kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi  wa Kanada nchini Tanzania, Mhe. Ian Myles (katikati) akitoa heshima wakati Wimbo wa Taifa ulivyokuwa ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Saalam kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi kutoka Ofisi ya Ubalozi wa Canada na Wizarani.Wapili kulia ni Balozi Joseph  Sokoine, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na wa kulia ni Balozi Zuhura Bundala, Mshauri wa Rais wa Masuala ya Diplomasia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Ian Myles baada ya kuwasilisha Hati za utambulisho. Kulia ni Balozi Joseph  Sokoine, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Balozi wa Thailand nchini Tanzania mwenye makazi  yake Nairobi, Kenya, Mhe. Prasittiporn Wetprasit akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Saalam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli

Balozi wa Thailand nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya Mhe. Prasittiporn Wetprasit akiwasilisha Hati zUtambulisho kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Balozi  wa Thailand nchini Tanzania, mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Prasittiporn Wetprasit (katikati) akitoa heshima wakati Wimbo wa Taifa ulivyokuwa ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Saalam kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Thailand nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Prasittiporn Wetprasit baada ya kuwasilisha Hati za utambulisho. Kulia ni Balozi Joseph  Sokoine, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Thailand nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Prasittiporn Wetprasit. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine na  kushoto ni Balozi Zuhura Bundala, Mshauri wa Rais wa Masuala ya Diplomasia.


Balozi  wa Austria nchini Tanzania mwenye makazi yake, Nairobi, Kenya, Mhe. Herald Gunther akisaini Kitabu cha Wageni Ikulu Jijini Dar es Saalam kabla ya kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
Balozi  wa Austria nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Herald Gunther akiwasilisha Hati zUtambulisho kwa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Balozi  wa Austria nchini Tanzania mwenye makazi yake Nairobi, Kenya, Mhe. Herald Gunther (katikati) akitoa heshima wakati Wimbo wa Taifa ulivyokuwa ukipigwa mara baada ya kuwasili Ikulu Jijini Dar es Saalam kuwasilisha Hati za Utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli. Kushoto kwa Mhe. Balozi ni Kaimu Mkuu wa Itifaki, Bw. James Bwana.

Wednesday, August 24, 2016

Rais Shein afungua Kongamano la 3 la Watanzania waishio Ughaibuni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano la tatu (3) la Diaspora lililofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beaach Resort Visiwani Zanzibar, 24 Agosti, 2016.
Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya kwanza visiwani Zanzibar limehudhuria na Watanzania wanaoishi nje ya nchi wapatao 342 na kushirikisha Taasisi na Idara za Serikali, Sekta binafsi na makundi ya wafanyabiashara.
Mhe. Dkt. Shein akiendelea kuzungumza
Naibu Katibu katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (wa pili kushoto) akiwa pamoja na Mkururugenzi wa Idara ya Diaspora Balozi Anisa Mbega (wa kwanza kulia ), Balozi Mohamed Mahundi (wa tatu kutoka kushoto) na Balozi Charles Sanga wakifuatilia kongamano kwa makini.
Mkurugenzi wa Idara ya Wizara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Balozi Silima Kombo Haji (wa tatu kutoka kulia),  na washiriki wengine wakifuatilia Kongamano.
Waziri wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Haji Ussi Gavu akitoa taarifa fupi ya kongamano la Diaspora pamoja na kumshukuru Mhe, Rais Shein kwa kuitikia wito wa kuwa mgeni Raismi na kufanya ufungunzi, sambamba na kumkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushiriki katika kongamano hilo pamoja na viongozi wengine walioshiriki katika Kongamano la tatu la Diaspora. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akihutubia katika Kongamano hilo ambapo aliwapongeza washiriki wote kwa kushiriki pamoja na kueleza nafasi ya diaspora katika kutumia fursa za uwekezaji zilizopo ili kuiletea Tanzania maendeleo.
Mwakilishi wa Watanzanzania wanaoishi ya Nje ya nchi ambaye aliishi ughaibuni kwa muda mrefu na baadae kurejea nchini Bw. Hussein M. Nyang'anyi akitoa taarifa katika Kongamano hilo. Bw. Nyang'anyi alitoa shukurani kwa Serikali kwa kuweza kuandaa Kongamano hilo kila mwaka na kuweza kuwakutanisha Watanzania waishio nje ya Nje, waliopo nchini na viongozi wakuu wa Serikali kwa lengo la kupeana taarifa na kupeana uzoefu katika masuala wa maendeleo hasa katika sekta ya Uwekezaji na Biashara.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akiratibu katika kongamano la tatu (3) la Diaspora, linalofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Sehemu ya washiriki wakiendelea kufuatilia mkutano wa pili kutoka kushoto ni Konseli Mkuu Dubai Bw. Mwadini   Wizara ya Mambo ya nje wakifuatilia Kongamano.
Sehemu ya Wawezeshaji walioshiriki katika Kongamano na kutoa mada mbalimbali wakifuatilia Kongamano
Sehemu nyingine ya Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na washiriki wengine wakifuatilia Kongamano
Kutoka kushoto ni Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Adolf Mchemwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Hangi Mgaka na washiriki wengine wakifuatilia Kongamano
Sehemu nyingine yamaafisa wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia Kongamano
Mkutano ukiendelea
Viongozi wa meza kuu wakiwa wamesimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa
Washiriki wakiwa wamesimama wakati nyimbo za Taifa zikipigwa
Bendi ya Jeshi la Polisi (Brass Band) wakipiga nyimbo za Taifa katika Kongamano
Mhe. Rais Shein akijadili jambo na Mhe. Waziri Mahiga mara baada ya kumaliza ufunguzi wa Kongamano
Picha ya Pamoja ya mgeni Rasmi Mhe. Dkt. Shein na meza kuu.
Picha ya pamoja ya meza kuu pamoja na wawezeshaji walioshiriki katika Kongamano

*****************************

Rais Shein afungua Kongamano la tatu (3) la Diaspora

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein amefanya ufunguzi wa Kongamano la tatu la Watanzania waishio Ughaibuni “Diaspora home coming” lililofunguliwa leo na linatarajiwa kufanyika kwa muda wa siku mbili  katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort Visiwani Zanzibar.

Kongamano hilo lenye kauli mbiu isemayo “Bridging Tanzania Tourism and Investment: A new Outlook” MTU KWAO NDIO NGAO ikiwa na lengo la kusisitiza kuunganishwa kwa sekta ya Utalii na Uwekezaji ili kwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya Serikali. Kongamano hili kwa mara ya kwanza linafanyika Zanzibar na kufanikiwa kwa kiasi kikubwa, lilitanguliwa na Makongamano mawili yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Mhe. Rais Shein katika hotuba yake ya ufunguzi, alieleza jitihada za makusudi zinazochukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika kutambua haki na wajibu wa Watanzania waishio Ughaibuni.  Hivyo kufuatia umuhimu huo Serikali iliamua kuanzisha Idara ya Diaspora ambayo inasimamia masuala yote ya jumuiya za wanadiaspora popote walipo katika mataifa mengine, sambamba na kuandaa sera ya diaspora ambayo itamtambua mwanadiaspora pamoja na kuainisha fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta ya utalii na uchumi na namna Wanadiaspora hao wanavyoweza kuchangia katika bajeti ya Serikali kwa kuchangia fedha katika akaunti maalum na katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo.

 Vilevile Mheshimiwa Rais Shein akaongeza kwa kusema kuwa “endapo sera hiyo ikikamilika jumuiya za wanadiaspora zitaweza kusoma sera hiyo kupitia Tovuti ya Ikulu na pale itakapohitajika kutunga sheria basi mamlaka zitafanya hivyo”.

Wazizi wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ambaye pia alishiriki katika hafla hiyo ya ufunguzi wa Kongamano, alitumia fursa hiyo kuwaeleza kuwa Tanzania inavivutio vingi na kuwashauri ni vema  wakatumia fursa hiyo kuvitangaza vivutio vilivyopo na pia kuvipa kipaumbele vivutio ambavyo bado havijatambuliwa ili viweze kutambuliwa rasmi na kutangazwa duniani kwote na kuiwezesha nchi ya Tanzania kushika nafasi ya juu miongoni mwa mataifa yenye vivutio na maajabu mengi duniani.
Pia alieleza Wizara kupitia Idara ya diaspora inaendelea na utaratibu wa kuandaa mfumo wa kuwatambua wanadiaspora na utekelezaji wake unaelekea kukamilika na kwamba zoezi hilo litakuwa la kuendelea ambapo takwimu zitakuwa zikihuishwa mara kwa mara katika ofisi zote za Ubalozi zinazoiwakilisha nchi ya Tanzania katika mataifa mengine.

Pia aliwaasa wanadiaspora hao kujiepusha kushiriki katika makosa ya kihalifu na makosa mengine ambayo yanapingana na sheria na taratibu za nchi husika. “Wizara yangu wakati mwingine imekuwa ikipokea taarifa za vitendo ambavyo zinaichafua sifa ya nchi yetu au kuleta masikitiko kwa ndugu na jamaa” alisema Waziri Mahiga.

Hivyo ni wakati sasa kila mwanadiaspora akawa balozi wa Tanzania katika nchi anayoishi kwa kutumia vizuri fursa za kimaendeleo zilizopo katika Taifa analoishi, pamoja na kudumisha sifa nzuri ya upendo, amani na mshikamano iliyojengeka tangu siku nyingi, ikiwa ni pamoja na kudumisha utamaduni wa Taifa.

Aidha, Watanzania waishio Ughaibuni walipata fursa ya kusikiliza mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa na watoa mada kutoka katika Taasisi na Idara za Serikali pamoja na sekta binafsi zilizolenga katika kuwapa taarifa  za taratibu za uwekezaji na miradi mbalimbali inayotekelezwa  na mashirika ya Umma na Makampuni binafsi sambamba na kuwaeleza  fursa nyingine mpya za miradi ya kiuchumi kama ujenzi, masoko kwaajili ya biashara mbalimbali,  utalii pamoja na uwekezaji katika sekta ya viwanda kwa lengo la kuunga mkono sera ya serikali ya awamu ya tano katika adhima yake ya kujenga Tanzania ya viwanda.