|
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na
Sultanate of Oman, Dkt Augustine Mahiga ( kushoto) na Yusuf bin Alawi bin
Abdullah wakizungumzia kuhusu namna ya kuendelea kuimarisha uhusiano mzuri
baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo hayo Waziri Mahiga ameiomba
serikali ya Oman kupitia Waziri Abdullah kuangalia uwezekano wa kushirikiana
katika uhifadhi ya nyaraka na kumbukumbu muhimu pamoja na ukarabati ya jengo la
House of Wonders lilojengwa na ufalma wa Oman mwaka 1883.
|
|
Jengo maarufu la Beit Al Jaib ( House of Wonders) ambalo Serikali ya
Tanzania inaiomba Serikali ya Oman kuangalia uwezekano wa kulikarabati kama
sehemu ya mradi wa kuhifadhi nyaraka, kumbukumbu na majengoa ya kihistoria
visiwani Zanzibar
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mshariki, Augustine
Mahiga akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na
masuala ya Afrika, Mazungumzo yao yalijielekeza zaidi katika uhusiano na
ushirikiano kati ya nchi hizi mbili.
|
=================================
Na
Mwandishi Maalum, New York
Ufalme wa Oman umeonesha nia ya kukarabati majengo ya
makubusho ya kale ya Beit Al Jaib maarufu kama “ House
of Wonders” yaliyopo mjini Unguja – Zanzibar.
Nia hiyo imeoneshwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Oman, Bw. Yusuf bin Alawi bin Addullah wakati alipokutana na
kufanya mazugumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga.
Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili
yalifanyika pembezoni mwa Mkutano wa 71 wa Baraza Kuu
la Umoja wa Mataifa, ambapo Mawaziri hao walikuwa wakiongoza ujumbe
wa Nchi zao.
Mazungumzo ya Mawaziri hao yalijikita
katika uimarishwaji wa uhusiano na ushirikiano mzuri
uliopo baina ya Oman na Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
Katika majadilaino hayo ambapo pamoja na mambo mengine,
Waziri Mahinga aliomba serikali ya Oman kuangalia
uwezekano wa kuanzishwa kwa miradi wa kutunza mambo ya kale
zikiwamo nyaraka muhimu zinazohusu uhusiano baina ya nchi hizo
mbili.
Waziri Mahiga alieelezea pia hali uchakavu wa majengo
ya Beit Al Jaib ( House of wonders) majengo yaliyokuwa
Ikulu ya utawala wa Kifalme, Zanzibar. Makubusho hayo
yamesheheni historia ya uhusiano na ushirikiano kati ya
Zanzibar na Sultanate of Oman na Afrika Mashariki kwa
Ujumla.
Na kutokana na historia hiyo na umuhimu wa jengo hilo
ambalo limejengwa mwaka 1883, Waziri ameiomba Serikali ya Oman
kuangalia uwezekano wa kulihifadhi jingo hilo ambalo pia ni kivutio
kikubwa cha utalii.
Akijibu ombi hilo na mengine yaliyowasilishwa na
Waziri Mahinga, Waziria wa Mambo ya Nje wa Oman, Bw .
Yusuf bin Alawi bin Addullah amemtaka Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuandaa andiko na
kuliwasilisha katika Serikali ya Oman ili pendekezo
hilo liweze kufanyiwa kazi pamoja na mapendekezo mengine.
Katika hatua nyingine, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Augustine Mahiga
amekuwa na kuwa na mazungumgo na Bi. Linda Thomas
Greenfield, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayehusika na
masuala ya Afrika.
Mazungumzo ya
Waziri Mahinga na Bi. Linda Greenfield yalijikita zaidi
katika uhusiano na ushirikiano baina ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na Marekani.