Mhe. Waziri akiendelea kuzungumza na waandishi wa habari |
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akifafanua jambo kwa waandishi wa habari |
Kaimu Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Bi.Chansa Kapaya akizungumza na waandishi wa habari.
TAARIFA YA
PAMOJA YA UMOJA WA MATAIFA NA SERIKALI
YA TANZANIA KWA VYOMBO VYA HABARI
Imezuiwa hadi Oktoba 19, 2016, Mchana kwa
saa za Afrika Mashariki.
MAADHIMISHO YA MIAKA 71 YA UMOJA WA
MATAIFA YASISITIZA MALENGO YA MAENDELEO ENDELEVU
’Wito watolewa kwa kila
mwananchi kuwajibika kwa malengo ya Dunia’
Oktoba 19, 2016 Dar es Salaam – OKTOBA 24
kila mwaka Umoja wa Mataifa hufanya maadhimisho ya kuzaliwa kwake.
Mwaka huu
mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania kwa kushirikiana na serikali,
wadau wa maendeleo na vijana wataadhimisha miaka 71 ya uwapo wa Umoja wa
Mataifa kwa staili ya aina yake.
Kwa mujibu
wa taarifa iliyotolewa katika mkutano wa waandishi wa habari na Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ikishirikiana na Umoja wa Mataifa ,
maadhimisho hayo mwaka huu yamelenga kuelezea kwa undani shughuli zinazofanywa
kwa pamoja kati ya pande hizo mbili ili kuwezesha maendeleo endelevu.
Katika
mkutano huo wa pamoja, waandishi wa habari walielezwa kwa ufupi Mpango Mpya wa Maendeleo
Chini ya Ufadhili wa Umoja wa Mataifa ( UNDAP ll -2016 hadi 2021) kwa serikali
ya Tanzania; na mpango wa maendeleo wa miaka mitano wa Tanzania ambamo malengo
ya maendeleo endelevu (SDGs) kama yalivyosanifiwa na kukubalika na jumuiya ya
kimataifa, yameshirikishwa.
Katika
mkutano huo na waandishi wa habari pia kulikuwepo na majadiliano ya mafanikio ya shughuli za Umoja wa Mataifa
hadi sasa duniani na pia nchini Tanzania .
Pia
mazungumzo hayo yalijikita katika malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na
umuhimu wa malengo hayo kumilikishwa kwa wananchi na wajibu wao katika
kuhakikisha kwamba kunakuwa na utekelezaji wenye mafanikio.
Pia
ilielezwa katika mkutano huo kwamba maadhimisho ya miaka 71 ya Umoja wa
Mataifa, Siku ya Umoja wa Mataifa, yatafanyika katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es Salaam Oktoba 24.
Maadhimisho hayo ambayo mwaka huu yamebeba ujumbe wa :“Uwezeshaji
wa vijana Tanzania kufikia malengo ya dunia” yanafanyika huku kukiwa na malengo
mapya ya dunia ya maendeleo endelevu.Malengo hayo ya SDGs yamelenga kuondoa
umaskini kwa kuwa na maendeleo endelevu.
Aidha ujumbe huo unaenda
sanjari na mpango wa maendeleo wa awamu ya pili wa Umoja wa Mataifa kwa
Tanzania (UNDAP II) ambao unaendeleza ule wa awali wa kuanzia 2011-16 ukiwa
umejikita katika masuala ambayo ni muhimu kwenye kukabili umaskini kwa kuwa na
maendeleo endelevu.
Maadhimisho ya mwaka huu yalitanguliwa na kongamano la vijana wapatao 200, ambao walijadili
masuala yanayogusa fursa za uchumi na maendeleo ya jamii na mchango ambao unaoweza
kutolewa na vijana kufanikisha utekelezaji wa malengo hayo.
Maadhimisho hayo yatafikia kilele chake
nchini kwa tukio litakalofanyika Visiwani Unguja Oktoba 26 mwaka huu.
Imeelezwa kuwa maadhimisho ya mwaka huu
yanaonesha uwapo wa ushirikiano mkubwa na wenye tija kati ya Tanzania, wananchi
wake na Umoja wa Mataifa.
Aidha maadhimisho hayo yanaonesha ni kwa
namna gani pande zote zipo tayari kutekeleza mipango ya maendeleo ya Umoja wa
Mataifa nchini Tanzania yenye lengo la kusaidia utekelezaji wa malengo ya
maendeleo endelevu.
Akizungumza umuhimu wa ushirikiano huo
katika kutekeleza mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ukiwa ni mpango wa
wananchi wenyewe, Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw
Augustine Mahiga, alielezea Tanzania kuunga mkono Umoja wa Mataifa ukifanyakazi
kama taasisi moja na kuwataka
watengeneza sera kuhakikisha kwamba wananchi wote wananufaika na ushirikiano
huu wa Tanzania na Umoja wa Mataifa.
Waziri Mahiga alisisitiza wakati Tanzania
inajikita katika kutekeleza mpango wake mpya wa taifa wa maendeleo, kuna haja
ya kuhakikisha kwamba wananchi wanaelewa na kumiliki mpango huo ambao
umejumuisha malengo ya maendeleo endelevu.
Alisema: “Tanzania imeshirikisha malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) katika sera
za taifa na pia katika mipango ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo ya
msingi yanayohitaji uangalizi kufanikisha maendeleo endelevu”.
Hata hivyo aliongeza kusema kwamba: “ Hiyo
inajulikana wazi kwamba serikali pekee haiwezi kufanikisha utekelezaji wa
ajenda ya maendeleo endelevu bila msaada wa sekta binafsi na wadau wetu wa
maendeleo, na hivyo iko haja ya kushirikishana. Tunaitaka sekta binafsi na
wadau wetu wa maendeleo kujiunga nasi katika juhudi hizi kwa kutuwezesha
kifedha ili tuweze kutekeleza mipango yetu ya maendeleo. Tunachohitaji sisi
tunaofanyakazi katika ushirikiano wa kimataifa kuhakikisha kwamba hatutamwacha
yeyote nyuma katika harakati zetu za kuleta maendeleo”.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez akizungumzia maadhimisho ya miaka 71 ya
Umoja wa Mataifa na uhusiano wake alisema: “Tanzania
na Umoja wa Mataifa zimekuwa na ushirikiano wa maendeleo kwa miongo mingi. Wakati
Tanzania sasa inabadilika, msaada unaotolewa na Umoja wa Mataifa unatakiwa
kukidhi haja mpya, hasa taifa linapoelekea katika uchumi wa kati”.
Pia katika hotuba yake aliongeza kwamba: “Malengo ya maendeleo endelevu ni muhimu
katika ushirikiano wetu kwani unaweka umuhimu wa shughuli za Umoja wa Mataifa
nchini Tanzania za kusaidia kupatikana kwa mafanikio katika nyanja za uchumi,
ustawi wa jamii na utunzaji wa mazingira.”
Angalizo
kwa wahariri:
Umoja wa Mataifa wa sasa ulianza shughuli
zake Oktoba 24, 1945 na katika miaka yake 71 imekuwa mstari wa mbele katika
kuhakikisha kwamba duniani kunakuwa mahali bora pa kuishi kwa kuwa na amani,
maendeleo na kulinda heshima ya kila mwanadamu. Nchini Tanzania, Umoja wa
Mataifa unanufaika na ushirikiano wake na serikali na wadau wengine wa
maendeleo katika kuhudumia wananchi.
Kwa
taarifa zaidi kuhusu juma la Umoja wa
Mataifa, tafadhali wasiliana na:
Nguse
Nyerere/ Sekela (sekela.mwambegele@nje.go.tz)
Wizara ya mambo ya nchi za nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki -MOFAIC - 0715371853
hoyce.temu@one.un.org
Mtaalamu wa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa -0682262627
|