Sehemu ya wageni waalikwa wakiwemo Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa nchini wakifuatilia hotuba ya Makamu wa Rais (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka 68 ya Uhuru wa India |
Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya nae akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 68 ya Uhuru wa India |
Sehemu nyingine ya wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Balozi wa India (hayupo nchini) |
Balozi Baraka Luvanda, Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiwa na Naibu Balozi wa China, Bw. Gou Haudong na Bi. Sun kutoka Ubalozi wa China wakati wa maadhimisho ya miaka 68 ya Uhuru wa China. |
Wageni waalikwa |
Wanafunzi wakiimba nyimbo za mataifa ya Tanzania na India wakati wa maadhimisho ya miaka 68 ya Uhuru wa India |
Kikundi cha Burudani kikitumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 68 ya Uhuru wa India |
Makamu wa Rais, Mhe. Suluhu katika picha ya pamoja |
==================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
India
yaadhimisha miaka 68 ya Uhuru
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan ameipongeza India kwa
kuadhimisha miaka 68 ya Uhuru wa nchi hiyo. Pongezi hizo alizitoa jana wakati wa
hafla ya kuadhimisha Siku ya Uhuru wa nchi hiyo ambayo ilienda sanjari na
ufunguzi wa jengo jipya la Ubalozi lililopo Mtaa wa Shaaban Robert Jijini Dar es
Salaam.
Mama Samia Suluhu
aliipongeza India kwa hatua kubwa ya maendeleo iliyopata katika nyanja
mbalimbali tokea ilipopata uhuru kutoka kwa Mwingereza ambaye pia aliitawala
Tanzania.
Makamu wa Rais aliitaja
India kuwa sio tu ni rafiki mkubwa wa Tanzania bali ni ndugu wa karibu
wanaounganishwa na bahari ya Hindi ambayo imekuwa kiunganishi kikubwa cha
wafanyabiashara hata kabla ya uhuru.
Alieleza kuwa uhusiano
kati ya Tanzania na India ni wa kuridhisha na umeimarika zaidi kufuatia ziara
ya Waziri Mkuu wa India, Mhe. Narendra Modi iliyofanyika nchini mwezi Julai
2016. “Wakati wa ziara hiyo mikataba mbalimbali ilisainiwa kati ya nchi hizi
mbili ambayo inalenga uedelezaji wa sekta tofauti kwa faida ya pande zote
mbili”.
Mama Samia aliendelea
kueleza kuwa ushirika wa Tanzania na India ni wa kimaendeleo ambapo Tanzania
imekuwa ikifaidika na misaada mbalimbali ya kimaendeleo ikiwa ni pamoja na
msaada wa kuendeleza miundombimu ya maji katika mikoa ya Dar es Salaan na Pwani
pamoja na Zanzibar; msaada wa kituo cha TEHAMA katika Chuo Kikuu cha Nelson
Mandela mkoani Arusha na uimarishaji wa vyuo vya ufundi.
Mhe. Samia Suluhu alitumia
fursa hiyo pia kuishukuru India kwa msaada iliyotoa wa zaidi ya Shilingi milioni
500 kwa ajili ya kusaidia waathirika wa tetemeko la Kagera lililotokea mwezi
Septemba 2016.
Kwa upande wake, Balozi wa
India, Mhe. Sandeep Arya aliridhishwa na uhusiano mzuri uliopo kati ya Tanzania
na India na kubainisha kuwa ziara ya Mhe. Modi mwezi Julai 2016 imeboresha na
kuimarisha zaidi mahusiano hayo. Aliahidi kuwa Serikali yake itaendelea
kushirikiana na Tanzania katika maeneo mbalimbali kama ilivyokuwa inafanya siku
za nyuma.
Alisema mahusiano ya kibiashara kati ya nchi hizo mbili ni makubwa na
kwamba nchi yake imeisaidia Tanzania katika maeneo mengi ikiwemo mikopo ya
masharti nafuu, mafunzo ya muda mfupi na mrefu, mafunzo ya ufundi, ujenzi wa
vituo vya TEHAMA, na vifaa vya matibabu.
Alizungumzia pia mahusiano ya asasi za
kiraia za Tanzania na India, ushirikiano katika masuala ya utamaduni, ziara za
Watanzania kwenda India kwa ajili ya matibabu na michezo ambapo aliitolea mfano
wa ziara ya timu ya Taifa ya Serengeti Boys nchini India mwaka jana.
Mhe. Balozi alihitimisha
hotuba yake kwa kusifu uamuzi wa Tanzania na India kufuta viza kwa watu wenye
Hati za Kusafiria za Kidiplomasia na zile za Serikali.
Imetolewa na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 27 Januari 2017. |