Monday, February 26, 2018

Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Palestina

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akisalimiana na Balozi wa Palestina hapa nchini, Mhe. Hazem Shabat alipokuja kumtembelea na kufanya nae mazungumzo katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Jijini Dar es Salaam
Prof. Mkenda akimweleza jambo Balozi Shabat walipokutana na kufanya mazungumzo.
Balozi Shabat naye akifafanua jambo kwa Prof. Mkenda 
Mazungumzo yakiendelea. Kulia ni Afisa Mambo ya Nje, Bi. Kisa Doris Mwaiseba.




Friday, February 23, 2018

Naibu Waziri akutana na Mjumbe Maalum kutoka Poland

Naibu Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  Mhe. Dkt. Suzan Kolimba akiwa katika mazungumzo na Mjumbe maalum kutoka Nchi ya Poland Mhe. Krzysztof Szczerki alipomtembelea Wizarani, tarehe 22 Februari, Dar es salaam. Mazungumzo yao yalilenga zaidi jinsi ya kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Nchi ya Poland katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

  Mhe. Dkt Kolimba na Mhe. Szczerki wakiendelea na mazungumzo, wanaofuatilia   wa kwanza kushoto ni Balozi wa Poland nchini Mhe. Krzysztof Buzalski pamoja na wajumbe waliombatana nao kutoka Ubalozini na wa kwanza  kulia ni Bw. Salvatory Mbilinyi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika  na Maafisa kutoka Wizarani.
Wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Mkutano

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mkurugenzi wa masuala ya Afrika kutoka Canada


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akizungumza na Mkurugenzi Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kusini na Mashariki mwa Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Canada, Bw. Marc-André Fredelte. Katika mazungumzo yao walijadili masuala ya ushirikiano katika masuala ya diplomasia, biashara na maendeleo. Bw. Fredelte yupo nchini kwa ziara ya kikazi.
Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ukifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Bw. Fredelte (hayupo pichani). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Salvator Mbilinyi, Bw. Mustafa M. Ussi, Afisa Mambo ya Nje na Bi. Lilian Kimaro, Afisa Mambo ya Nje
Mazungumzo yakiendelea
Balozi Mwinyi akiagana na Bw. Fredelte baada ya kumaliza mazungumzo yao
Picha ya pamoja

Kaimu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje akutana na Mbunge kutoka Uturuki

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan M. Mwinyi akiwa katika mazungumzo na Mhe. Zehra Taskesenlioglu, Mbunge na Mwenyekiti wa Umoja wa Wabunge wa Bunge la Uturuki wanaounda Kundi la Wabunge Marafiki na Wabunge wa Bunge la Tanzania alipofika Wizarani tarehe 23 Februari, 2018. Katika mazungumzo yao walizungumzia umuhimu wa kukuza na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Uturuki katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu.
Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutoglu (kulia) akiwa pamoja na Bw. Aytak Dincer, Mwekezaji na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Tanzania na Uturuki wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mwinyi na Mhe. Zehra (hawapo pichani)
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Salvator Mbilinyi (kulia) akiwa na Bw. Hassan Mwamweta, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo
Kikao kikiendelea

Naibu Waziri Kolimba aongoza maadhimisho ya siku ya Taifa la Kuwait

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Suzan Kolimba (Mb.) akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya Taifa la Kuwait. Katika hafla hiyo Dkt.Kolimba ambaye alikuwa mgeni rasmi alitumia fursa hiyo kulipongeza taifa hilo na kuahidi kuendeleza ushirikiano  uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.Pia alimpongeza Balozi wa Kuwait hapa nchini Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem kwa juhudi zake za kuboresha na kukuza ushirikiano kati ya Tanzania na Kuwait hususan kwa kuchangia  sekta mbalimbali zikiwemo huduma za kijamii kama elimu na afya. Hafla  hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Jijini Dar es Salaam

Sehemu ya Mabalozi walio hudhuria hafla hiyo wakimsikiliza kwa makini Dkt. Kolimba (hayupo pichani).
Dkt. Kolimba akiendelea kuzungumza huku wageni waalikwa wakimsikiliza.

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jasem Ibrahim Al Najem naye akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Sehemu nyingine ya Mabalozi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Najem akihutubia.
Dkt. Kolimba akishiriki katika zoezi la kukata keki kwenye hafla hiyo.
Dkt. Kolimba akipokea picha iliyochorwa kwa Mkono kutoka kwa Balozi Najem.
Dkt. Kolimba akisalimiana na Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim walipokutana kwenye hafla hiyo.
Dkt. Kolimba akisalimiana na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania Mhe. Monica Patricip Clemente Mussa. 
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba.










Friday, February 16, 2018

Serikali kutoa viwanja kwa ajili ya Mabalozi kujenga ofisi na makazi Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda akiongea katika kikao na Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wa hapa nchini kuhusu Mpango Mkuu wa mji wa Serikali mjini Dodoma ambao utakuwa na eneo kwa ajili ya wanadiplomasia.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mshereheshaji wa kikao, Bi. Mindi Kasiga akitoa utaratibu na ratiba ya kikao hicho.
Prof. Mkenda akiendelea kuongea na wanadiplomasia wa hapa nchini kuhusu Mpango Mkuu wa mji wa Serikali mjini Dodoma.


Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Umma walioshiriki kusikiliza mada kuhusu Mpango Mkuu wa mji wa Dodoma.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi akitoa maelezo kuhusu manispaa yake ilivyojipanga kujenga mji wa Serikali Dodoma.

Mtaalamu kutoka kamati maalum ya kupanga Manispaa ya Dodoma akiwasilisha mada kuhusu mji wa Serikali Dodoma.

Balozi wa Afrika Kusini nchini Tanzania Mhe. Thami Mseleku akiuliza swali kuhusu mpango mkuu wa mji wa Serikali Dodoma.

Balozi wa Mamlaka ya Palestina nchini Tanzania  Mhe. Hazem Shabat akichangia mada kuhusu mpango mkuu wa mji wa Serikali mjini Dodoma.

Balozi wa Malawi nchini Tanzania Mhe. Hawa O. Ndilowe akichangia mada kuhusu mpango mkuu wa mji wa Serikali mjini Dodoma.

Katibu Mkuu (katikati) akijibu maswali ya Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi (kulia) na Kaimu Mkuu wa Mabalozi na Balozi wa Saharawi nchini, Mhe. Ibrahi Buseif.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali kutoa viwanja kwa ajili Mabalozi kujenga ofisi na makazi Dodoma

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf  Mkenda amewahakikishia Waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa hapa nchini kuwa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwapatia viwanja vya ukubwa wa ekari 5 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na makazi ya Balozi mjini Dodoma itatekelezwa kama ilivyoahidiwa.

Rais Magufuli alitoa ahadi hiyo katika sherehe  za  kufungua mwaka wa 2018 ya wanadiplomasia zilizofanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam tarehe 09 Februari 2018.

Prof. Mkenda alitoa kauli hiyo kwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wakati wa kuwasilisha mada kuhusu Mpango Mkuu wa Mji wa Serikali mjini Dodoma.

Mada hiyo ilitolewa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Manispaa ya Dodoma kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) leo Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa mada hiyo, mji wa Serikali mjini Dodoma utajengwa pembeni ya Barabara ya Dar Es Salaam hadi Dodoma, kilomita 17 kutoka katikati ya mji wa Dodoma na unakadiriwa kugharimu Shilingi za Kitanzania trilioni 10 hadi unakamilika.

Mji huo ambao umesanifiwa kwa asilimia 100 na wataalamu wa Kitanzania umezingatia mahitaji yote muhimu ambayo mji wa kisasa unastahili kuwa nayo. Miongoni mwa mahitaji hayo ni pamoja na miundombinu ya kutosha ikiwemo barabara, maji safi na maji taka, nishati ya umeme, TEHAMA na dampo kwa ajili ya taka ngumu ambalo ujenzi wake umeshakamilika na juhudi zinaendelea za kutafuta mwekezaji kwa ajili ya kubadilisha taka kwa matumizi mengine (recycling).

Aidha, usanifu wa mji huo umezingatia vigezo vya uendelezaji endelevu wa miji duniani ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira na urithi wa asili, kuepuka uchafuzi wa hali ya hewa na urahisi wa kufikika.
Wasanifu wa mji huo wakisisitiza kuhusu uendelezaji endelevu wa miji, katika usanifu wao wamezingatia hali ya hewa ya Dodoma ambayo ni ya joto na upepo mkali, hivyo, wametenga maeneo kwa ajili ya upandaji miti itakayopunguza kasi ya upepo na ujenzi wa vyanzo vya maji kwa ajili ya kupoza joto. 

Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Bw. Godwin Kunambi alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kwenda kuwekeza katika mji wa Dodoma katika miradi mbalimbali ikiwemo mashule, hospitali, mahoteli, maduka makubwa na miundombinu mingine. “Tumetenga eneo kubwa kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambalo limegawanywa katika ukubwa tofauti tofauti kutegemea na mahitaji ya mwekezaji, hivyo wahimizeni wafanyabiashara kutoka katika nchi zenu waje kuwekeza Dodoma”. Bw. Kunambi aliwaambia Mabalozi.

Bw. Kunambi alieleza kuwa Mpango Mkuu wa mji wa Dodoma ulisanifiwa tangu mwaka 1976 na kufanyiwa mapitio mwaka 2010 na sasa wataalamu hao ambao wamepata uzoefu kutoka nchi mbalimbali zikiwemo Nigeria, Malaysia, China na Malawi ili kusanifu mji unaozingatia mahitaji ya sasa.

-Mwisho-
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam, 16 Februari 2018

Mhe. Rais Magufuli awaapisha Mabalozi wa Tanzania nchini Nigeria na Sweden


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha Bw. Muhidin Ally Mboweto kuwa Balozi wa Tanzania nchini Nigeria. Hafla ya uapisho imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 16 Februari, 2018


Balozi Mboweto akisaini mara baada ya kula kiapo cha kuiwakilisha Tanzania nchini Nigeria
Mhe. Rais Magufuli akimkabidhi vitendea kazi Balozi Mboweto
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Dkt.John Pombe Joseph Magufuli akimwapisha Dkt. Wilbroad Peter Slaa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sweden.
Balozi Slaa akisaini kiapo chake
Mhe. Rais Magufuli alimkabidhi Balozi Slaa vitendea kazi
Balozi Mboweto na Balozi Slaa kwa pamoja wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi mbele ya Mhe. Rais Magufuli
Mhe. Rais Magufuli kwa pamoja na Balozi Mboweto na Balozi Slaa (walioketi) wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Mabalozi hao mara baada ya kuapishwa.
 Wakuu wa Vyombo vya Usalama nchini na wageni wengine waalikwa wakimsikiliza Dkt.Kolimba (hayupo pichani)
Sehemu ya viongozi mbalimbali na wageni waalikwa  wakiwa kwenye hafla ya kuapishwa kwa Balozi Mboweto na Balozi Slaa (hawapo pichani). Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi


Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Mboweto mara baada ya kumwapisha
Mhe. Rais akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Slaa mara baada ya kumwapisha

 Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi walioapishwa na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi (wa pili kulia) na  Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kushoto)
 Mhe. Rais Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi walioapishwa na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi (kushoto) na Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara ya Mambo aya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.