Balozi Doanh naye akifafanua jambo katika mazungumzo hayo. |
Mazungumzo yakiendelea |
Balozi Doanh naye akifafanua jambo katika mazungumzo hayo. |
Mazungumzo yakiendelea |
|
Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Bibi Ayelet Shaked akiwahutubia mamia ya watu hawapo pichani waliohudhuria hafla ya ufunguzi wa ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Israel. Kushoto ni Waziriwa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga na kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watanzania wanaoishi Israel. |
Bi. Kisa Doris Mwaseba (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watanzania wanaoishi Israel. |
Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye anaiwakilisha pia Tanzanaia nchini Uswisi, Mhe. Dkt. Abdallah Possi akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afriika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga katika Uwanja wa Ndege wa Zurich. Dkt. Possi alikuja kumpokea na kumsindikiza Mhe. Waziri akiwa njiani kuelekea Israel. |
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Dkt, Mahiga afungua Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania,
Israel
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amezindua
rasmi ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Israel na kuitaka Israel nayo
iharakishe kufungua ofisi ya ubalozi nchini Tanzania.
Ufunguzi wa ofisi
hiyo ya ubalozi iliyopo katika mji wa Tel Aviv ulifanyika leo na ulihudhuriwa na
watu mbalimbali wakiwemo Waziri wa Sheria wa Israel, Mhe. Ayelet Shaked,
Mabalozi wa nchi za Afrika na Watanzania wanaoishi nchini humo.
Katika hotuba yake,
Dkt. Mahiga aliitaja Israel kama nchi ya kupigiwa mfano kwa sababu licha ya
changamoto za kimahusiano na baadhi ya jirani zake lakini bado nchi hiyo imepiiga
hatua kubwa za kimaendeleo katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo cha
umwagiliaji, viwanda, matibabu, TEHAMA, ulinzi na usalama, uhifadhi wa maji na
masuala ya nishati ikiwemo nishati ya kutumia joto ardhi.
Kwa upande wa
ulinzi na usalama, Waziri Mahiga alisema Watanzania hawataisahau Israel kwa kuwa
ndiyo nchi iliyoisaidia Tanzania kuanzisha Jeshi la Kujenga Taifa ambalo
mafanikio na mchango wa jeshi hilo unajulikana na kila Mtanzania. Alisema JKT
baada ya lugha ya Kiswahili ndiyo chombo cha pili kilichosaidia kwa kiasi
kikubwa kuunganisha makabila zaidi ya 120 ya Watanzania na kuwa wamoja hadi
leo.
Dkt. Mahiga
alieleza kuwa Israel ni nchi yenye mafanikio makubwa duniani ambapo imepelekea
raia wake wengi kushinda tuzo za Nobel na hiyo imetokana na harakati zao kwa
ajili ya wanadamu.
Aliishukuru Israel
kufuatia mawaziri wake wawili kufanya ziara za kikazi nchini Tanzania hivi
karibuni. Mawaziri hao ni Waziri wa Ulinzi, Mhe. Avigdor Liberman aliyetembelea
Tanzania tarehe 20 hadi 22 Machi 2018 na Waziri wa Sheria, Mhe. Ayelet Shaked ambaye
alikuwa nchini tarehe 23 na 24 Aprili 2018.
Katika ziara hizo
masuala mbalimbali yaliafikiwa ikwemo Israel kuisaidia Tanzania kuanzisha
chombo cha kutoa msaada wa kisheria kwa wasiojiweza ambacho kwa upande wa
Israel kimeshaanzishwa na kina mafanikio makubwa.
Dkt.Mahiga aliwakaribisha
Waisrael kuja Tanzania kwa ajili ya kufanya utalii kwa kuwa Tanzania ina
vivutio lukuki vya utalii. Alisema zaidi ya watalii elf 50 wanakuja Tanzania
kila mwaka lakini hawatoshi kutokana na uwingi wa vivutio vya utalii vilivyopo
nchini.
Kwa upande wake,
Mhe. Shaked alibainisha kuwa Israel ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika
sekta mbalimbali ikiwemo kusaidia teknolojia ya kisasa kwenye kilimo ili
kuongeza tija katika uzalishaji.
Aidha, Balozi wa
kwanza wa Tanzania nchini Israel, Mhe. Job Masima alishukuru wadau wote ikiwemo
Serikali ya Israel kwa kumpa ushirikiano wa kutosha uliofanikisha upatikanaji
wa ofisi hiyo na kufunguliwa rasmi tarehe 08 Mei 2018. Aliwahakikishia umma
uliohudhuria hafla hiyo na wadau wengine kuwa wasisite kufika kwenye ofisi hiyo
kwa ajili ya kupata huduma watakazozihitaji.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Israel
09 Mei 2017
|
Mabalozi kutoka Nchi zinazounda kundi linaloitwa United for Consensus wakifuatilia mazungumzo hayo kutoka kulia ni Balozi wa Pakistan nchini, Mhe. Amir Mohamed Khan, balozi wa Hispania nchini, Mhe. Felix Costales, Balozi wa Canada nchini, Mhe. Alexander Leveque, Balozi wa Korea Kusini nchini, Mhe. Song Geum Yong na Mwisho ni Balozi wa Uturuki nchini, Mhe. Ali Davutaglu. |
< img border="0" data-original-height="1067" data-original-width="1600" height="426" src="https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhEEzdZagi5bvoM5-taNfQfEv-oXyk1lr_cKyw_djjJPoRaw33Kqamw1r8CqO8nm-Uovy1sFId6l55xBtqweudZlOjxJln9y2SJw-VI_HD8bRv0U45-j0_qKKaP4K3HrAmr5MJ_zmWR5Gs/s640/1X2A6499.JPG" width="640" /> |
Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mazungumzo hayo. |
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Adolf Mkenda amekutana na kufanya mazungumzo na Bw. Apple Sun, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Kutengeneza Magari ya Foton Motors Group Kenya, Mazungumzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Wizara, Tarehe 08 Mei,2018, Dar es Salaam. Katika kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli za Tanzania mpya ya Viwanda na pia katika kuendelea kutekeleza Diplomasia ya Uchumi, Prof.Mkenda alitumia mazungumzo hayo kuishawishi kampuni hiyo kujenga kiwanda cha kutengeneza magari hapa nchini, Kampuni hiyo iwapo itajenga kiwanda hicho hapa nchini itachangia kwa kiwango kikubwa kuongeza ajira kwa Watanzania na pia kusaidia katika juhudi za kutunza mazingira kwani itapunguza uagizaji wa magari yaliyotumika ambayo huchangia katika uharibifu wa mazingira. Prof. Mkenda amewahakikishia ushirikiano kutoka Serikalini iwapo watajenga kiwanda hicho hapa nchini.Kampuni hiyo kutoka nchini China inatengeneza magari mbalimbali kama vile pick-up, magari ya kawaida, SUV, maroli, matrekta n.k yenye kutumia teknologia ya hali ya juu na ubora mkubwa. Kwa sasa Kampuni hiyo ina Kiwanda cha kutengeneza magari (Assembling Plant) nchini Kenya. Naye Bw. Sun alisema Kampuni yake iko tayari kwa mazungumzo na Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuona uwezekano wa kujenga Kiwanda hicho hapa nchini, hata hivyo kwa sasa wameishafungua ofisi ya uwakilishi hapa nchini. |
TAARIFA KWA VYOMBO HABARI
Waziri Mahiga kuzuru Israel
Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) atafanya
ziara ya kikazi nchini Israel kuanzia tarehe 07 hadi 10 Mei 2018. Ziara hiyo
imekuja kufuatia mwaliko wa mwenyeji wake ambaye ni Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo
ya Nje wa Israel, Mhe. Benjamin Netanyahu. Dkt. Mahiga anakuwa Waziri wa kwanza
wa Mambo ya Nje kutoka Tanzania kufanya ziara nchini Israel.
Atakapowasili nchini
Israel, Dkt. Mahiga atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Mhe. Netanyahu
na kushiriki uzinduzi rasmi wa Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini humo.
Ikumbukwe Israel ni
moja kati ya nchi sita ambazo Serikali ya awamu ya tano imefungua Balozi Mpya.
Mhe. Job Masima aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuwa Balozi wa kwanza wa Tanzania nchini humo.
Waziri Mahiga ataitumia
ziara hiyo sio tu kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia uliopo bali pia
kuishawishi Serikali ya Israel iunge mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano
ya kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa viwanda.
Israel ni moja ya nchi
zenye maendeleo makubwa duniani katika sekta mbalimbali zikiwemo kilimo,
viwanda, uhifadhi wa maji, matibabu, ulinzi na usalama, mawasiliano na nishati
ya joto ardhi. Hivyo kupitia ziara hiyo, agenda ya uchumi wa viwanda ya
Tanzania inaweza kupata ushirikiano mkubwa wa Israel kutokana na hatua kubwa ya
kimaendeleo iliyofikia.
Kabla ya Tanzania
haijafungua ofisi ya Ubalozi Israel, ilikuwa inawakilishwa kupitia ubalozi wake
Misri na Ubalozi wa Israel nchini Kenya unawakilisha pia Tanzania hadi sasa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
06
Mei, 2018
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje imejipanga kutekeleza
Sera ya Uchumi wa Viwanda
Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki wametakiwa kufanya kazi kwa weledi ili kutimiza
malengo ya Serikali ya awamu ya tano ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda.
Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) wakati wa kikao cha Baraza la Wafanyakazi
kilichofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Waziri Mahiga alieleza kuwa Wizara inatakiwa
kuweka Sera na mikakati ya utekelezaji kwa kuzingatia miongozo na maelekezo ya
Viongozi wa juu akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John
Pombe Joseph Magufuli.
“Sera ya Serikali ya awamu ya tano ni kuifanya
Tanzania kuwa nchi ya viwanda, hivyo Sera yetu ya Mambo ya Nje lazima ijikite
katika diplomasia ya uchumi wa viwanda”. Dkt. Mahiga alieleza.
Dkt.
Mahiga alihitimisha hotuba yake kwa kuwataka watumishi kuhakikisha kuwa Wizara inatekeleza
majukumu yake kwa kujiwekea ratiba ya kuyakamilisha kwa kuzingatia hotuba za
Mhe. Rais Magufuli alizozitoa wakati wa
ufunguzi wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kikao cha Mabalozi na
Mhe. Rais Magufuli na kikao cha watumishi wa Wizara na Mhe. Rais Magufuli.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Adolf Mkenda amesema
kuwa Wizara yake imejipanga ipasavyo kuhakikisha kwamba jukumu la
kuchochea uchumi wa nchi kupitia Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika
diplomasia ya uchumi inatekelezwa kikamilifu.
Prof. Mkenda alisema Wizara kwa kushirikiana na ofisi zake za Ubalozi, licha ya changamoto mbalimbali inazokutana nazo, lakini imekuwa ikitafuta fursa za uwekezaji, mitaji, masoko, utalii na elimu na kuzileta nchini ili kufikia azma ya Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo mwaka 2020. Alizitaja Balozi chache zilizoleta wafanyabiashara wakubwa kwa ajili ya kutafuta fursa za uwekezaji nchini kuwa ni pamoja na Balozi za Tanzania nchini China, Ufaransa, Korea Kusini, Kenya, Ujerumani na Israel. "Balozi wetu China, Mhe. Mbelwa Kairuki ametafuta taasisi za kifedha kwa ajili ya kuzikopesha benki za Tanzania ili zikuze mitaji ya kutoa mikopo kwa wawekezaji. Aidha, Serikali ya Ujerumani imefungua ofisi maalum kwa ajili ya kuratibu na kusaidia shughuli za kibiashara na uwekezaji hapa nchini" Prof. Mkenda alisema. Prof. Mkenda alisifu jitihada zilizofanywa na Ubalozi wa Tanzania nchini Kenya hivi karibuni za kuandaa maonesho ya bidhaa za viwanda vya hapa nchini yaliyofanyika jijini Nairobi tarehe 25 - 28 Aprili 2018. Alisema maonesho hayo ya kipekee yalikuwa na mafanikio makubwa ambapo wafanyabiashara walioshiriki waliingia makubaliano na wafanyabiashara wa Kenya ya kupeleka bidhaa zao nchini Kenya.
"Tunatakiwa tuondoe vikwazo vya kufanya
biashsra, kuondoa vikwazo hivyo haina maana Tanzania iwe gulio la kuuzia bidhaa
kutoka nje, bali wafanyabiashara wetu wanatakiwa kuchangamkia masoko ya nje ili
wauze bidhaa zao kwa wingi nje ya nchi", Katibu Mkuu alisisitiza.
Katibu Mkuu alisema ili watumishi waweze kutimiza
malengo ya Wizara yakiwemo ya kuvutia wawekezaji kutoka nje, Wizara imejipanga
kuwawezesha watumishi kupata elimu, ujuzi, teknolojia na uzoefu unaohitajika
kutimiza majukumu hayo.
Kuhusu suala la kupeleka watumishi kwenye vituo
vya Ubalozi, Katibu Mkuu alieleza kuwa Wizara itatekeleza jukumu hilo kwa haki
kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa ambavyo ni weledi, ujuzi na mahitaji ya
Balozi husika. “Wizara haitapeleka watumishi vituoni kutokana na shinikizo au
kuangalia sura, kabila na dini ya mtu ili kuondoa malalamiko yaliyokuwepo kwa
muda mrefu Wizarani.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
05 Mei, 2018
|