Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Innocent E. Shiyo akifungua Warsha ya Mafunzo ya Mfumo wa Ufuatialiaji na
Tathmini wa SADC (SADC Results Based
Online Monitoring and Evaluation System) kwa niaba ya Katibu Mkuu Prof. Aldof Mkenda, kulia kwake ni Meneja Mradi kutoka GIZ Bw. Robson Chakwama na wa mwisho ni mmoja wa Wakufunzi wa Warsha hiyo kutoka SADC Bi. Lerato Moleko
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara kwa kushirikiana na Serikali
ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti
ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), yametolewa kwa Maafisa wa Serikali na Taasisi za Umma, tarehe 15 - 17 Mei,2018 katika ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere, Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya Maafisa kutoka Wizarani wakifuatilia mafunzo hayo.
Mkutano ukiendelea
Picha ya pamoja baada ya mkutano
===============================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA
HABARI
TAARIFA KUHUSU WARSHA YA MAFUNZO JUU YA MFUMO WA
UFUATILIAJI NA TATHMINI WA SADC KWA MAAFISA WA SERIKALI NA TAASISI ZA UMMA
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki kwa kushirikiana na Serikali
ya Ujerumani chini ya Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) na Sekretarieti
ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imeandaa Warsha ya Mafunzo ya
Mfumo wa Ufuatialiaji na Tathmini wa SADC (SADC
Results Based Online Monitoring and Evaluation System) kwa maafisa wa
Serikali na taasisi za umma. Warsha hii inafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam kuanzia tarehe 15 hadi 17 Mei, 2018.
Lengo la warsha hii ni kuwezesha wizara na taasisi
mbalimbali za Serikali kufahamu utendaji kazi wa mfumo huu wa SADC ambao
unalenga kukusanya taarifa za utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za
maendeleo za SADC ambazo zinatekelezwa ndani ya nchi na kikanda kwa ujumla.
Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini wa SADC uliridhiwa
na Kikao cha Baraza la Mawaziri wa SADC kilichofanyika katika Falme ya Eswatini
(Swaziland) mwezi Machi, 2017. Pamoja na mambo mengine, mfumo huu utawezesha
pia nchi wanachama kufanya tathmini ya kina ya utekelezaji wa Mpango Mkakati wa
Maendeleo ya Kanda uliofanyiwa maboresho wa mwaka 2015-2020 (Revised Regional Indicative Strategic Plan,
2005 – 2020). Mpango huu ndio mkakati mkuu (blueprint) unaosimamia programu zote za kisiasa, kiuchumi na
kijamii zinazotekelezwa SADC.
Warsha hii itatuwezesha kufuatilia kwa karibu zaidi
maendeleo ya utekelezaji wa itifaki na programu mbalimbali za SADC katika sekta
zao na kutoa tathmini, na kubainisha fursa zinazopatikana kupitia uanachama
wetu. Hadi sasa nchi za Lesotho, Mauritius, Falme ya Eswatini (Swaziland),
Zambia na Zimbabwe tayari wameshapata mafunzo ya mfumo huu. Tanzania itakuwa ni
nchi ya sita.
Tanzania kama mwanachama hai na mwanzilishi wa
Jumuiya hii, hadi kufikia Machi, 2018 imesaini jumla ya Itifaki 28 kati ya
itifaki 31. Kati ya Itifaki zilizowekwa saini, jumla ya Itifaki 23
zimesharidhiwa na itifaki 5 ziko katika hatua mbalimbali za kuridhiwa.
Aidha,
kuna Itifaki nyingine tatu ambazo Tanzania bado haijaweka saini ambazo ni
itifaki ya Ajira na Kazi 2014; Itifaki ya Utunzaji wa Mazingira kwa Maendeleo
Endelevu 2014 na itifaki ya kulinda aina Mpya ya Mimea, 2017. Itafaki hizi
zinatarajiwa kusainiwa wakati wa Mkutano wa 38 wa Wakuu wa Nchi na Serikali
utakaofanyika mwezi Agosti, 2018 Windhoek, Namibia.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es
Salaam, 15 Mei ,2018