Saturday, November 10, 2018

Ubalozi wa Poland waadhimisha miaka 100 ya Uhuru

Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Taifa ya Poland iliyofanyika kwenye makazi ya Balozi jijini Dar Es Salaam tarehe 09 Novemba 2018.

Mhe. Krzysztof Buzalski, Balozi wa Poland nchini akisoma hotuba katika hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya uhuru wa Poland

Baadhi ya wageni mbalimbali walioshiriki hafla hiyo wakisikiliza kwa makini hotuba za viongozi

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan Mwinyi alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 100 ya Uhuru wa Taifa la Poland. Sherehe hizo zilifanyika katika makazi ya Balozi wa Poland, Mhe. Balozi Krzysztof Buzalski yaliyopo Oystberbay, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Novemba 2018
.
Katika Sherehe hizo, Naibu katibu Mkuu pamoja na mambo mengine alifafanua kuwa uhusiano baina ya Poland na Tanzania ni wa kihistoria na kuwa unaimarika siku hadi siku.

Pamoja na kuishukuru Poland kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, amemuomba Balozi Buzalski, kuongeza jitihada katika kuvutia wawekezaji zaidi wa Poland kuja kuwekeza hapa nchini na kusaidia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania nchini Poland.

Naibu Katibu Mkuu amemhakikishia Balozi wa Poland kuwa Wizara na Serikali kwa jumla itampa ushirikiano wakati wowote atakapohitaji ili kufanikisha malengo kwa manufaa ya mataifa yote mawili.

Friday, November 9, 2018

RAIS DKT. MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO TOKA KWA MABALOZI WAPYA WA UAE, CANADA NA SPAIN IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Mohamed Al-Marzooqi mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018  

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Canada nchini Mhe. Pamela O'Donnel mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero  kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na  Balozi wa Spain nchini Mhe. Maria Pedros Carrtero mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho kwenye sherehe iliyofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 8, 2018




Taarifa kwa Vyombo vya Habari kuhusu fursa za ufadhili wa masomo



FURSA ZA UFADHILI WA MAFUNZO

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imepokea fursa za ufadhili wa masomo ya muda mfupi kutoka Serikali ya Singapore kupitia Programu ya Ushirikiano ya nchi hiyo (SCP) na Serikali ya Israel kupitia Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Israel (MASHAV).

Maelekezo ya kalenda ya kozi ambazo zimetolewa chini ya ufadhili wa Programu ya Ushirikiano ya Singapore inapatikana kupitia tovuti yao ya http://www.scp.gov.sg.

Taarifa ya kina kuhusu nafasi za masomo chini ya ufadhili wa MASHAV inapatikana kupitia tovuti ya https: //mfa.gov.il/MFA/mashav/Courses/Pages/default.aspx.

Sehemu ya kalenda ya kozi chini ya ufadhili wa Programu ya Ushirikiano ya Singaporekwa mwaka 2018 na 2019 ni kama inavyoonesha kwenye jedwali hapa chini.


Na.
JINA LA KOZI
MUDA WA KOZI KUANZA
MUDA WA KOZI KUMALIZIKA
1.
Maritime Public Leaders Programme
12/11/2018
16/11/2018
2.
Public Private Partnerships for Infrastructure Financing
19/11/2018
23/11/2018
3.
Smart Nation: Strategy to Implementation
26/11/2018
30/11/2018
4.
Green Climate Financing
03/12/2018
07/12/2018
5.
Integrated Cyber Security Management
10/12/2018
14/12/2018
6.
Investment Promotion and Free Trade Management-FTAs
17/12/2018
21/12/2018
7.
Strategic Foresight: From Insight to Action
14/01/2019
18/01/2019
8.
International Law of the Sea
21/01/2019
25/01/2019
9.
Aviation Security Auditing Techniques and Developing Security Manuals
21/01/2019
25/01/2019
10.
Competitive and Sustainable Ports
28/01/2019
01/02/2019
11.
Climate Change and Emerging Threats
18/02/2019
22/02/2019
12.
Aircraft Accident Investigation Management
18/02/2019
22/02/2019
13.
Strategies to Promote Active Ageing
25/02/2019
01/03/2019
14.
International Dispute Resolution
04/03/2019
08/03/2019
15.
Aviation Incident Investigation: Effective Safety Risk Management
11/03/2019
15/03/2019
16.
Aeronautical Information Services/Management-AIS-AIM
18/03/2019
22/03/2019

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma
09 Novemba, 2018



Thursday, November 8, 2018

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Announcement for Opportunities to Study in Ireland


PRESS RELEASE
Announcement for Opportunities to Study in Ireland
Applications are invited from qualified Tanzanians to apply for Irish Aid Fellowship Programme for the year 2018/2019.

The call for applications is now open and the closing date for receipt of applications from Tanzania is 12pm on Friday 30th  November 2018.

Completed applications should be submitted to the Irish Embassy in Tanzania before the specified deadline. 

For more details about the programme and the application process please refer to the Irish Embassy website: https://www.dfa.ie/irish-embassy/tanzania/our-services/opportunities-to-study-in-ireland/.

Applications from female candidates are highly encouraged.



Issued By: Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation
Dodoma
7th November 2018