Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Ramadhan
Mwinyi alikuwa Mgeni Rasmi katika
sherehe za kutimiza miaka 100 ya Uhuru wa Taifa la Poland. Sherehe hizo
zilifanyika katika makazi ya Balozi wa Poland, Mhe. Balozi Krzysztof Buzalski
yaliyopo Oystberbay, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Novemba 2018
.
Katika Sherehe hizo,
Naibu katibu Mkuu pamoja na mambo mengine alifafanua kuwa uhusiano baina ya
Poland na Tanzania ni wa kihistoria na kuwa unaimarika siku hadi siku.
Pamoja na kuishukuru
Poland kwa uwekezaji katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo, amemuomba Balozi
Buzalski, kuongeza jitihada katika kuvutia wawekezaji zaidi wa Poland kuja
kuwekeza hapa nchini na kusaidia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania
nchini Poland.
Naibu Katibu Mkuu
amemhakikishia Balozi wa Poland kuwa Wizara na Serikali kwa jumla itampa
ushirikiano wakati wowote atakapohitaji ili kufanikisha malengo kwa manufaa ya
mataifa yote mawili.
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.