Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.) akitoa neno la ufunguzi kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maiasili na Utalii, Mhe. Dkt. Khamis Kigwangalla kuongea na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo. Viongozi hao walifanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari kuelezea mikakati inayochukuliw na Serikali ya awamu ya tano ya kuvutia utalii nchini. Mikakati hiyo imeanza kuzaa matunda ambapo wnanchi wa Urusi wameichagua Tanzania kuwa eneo bora zaidi kwa utalii duniani na kutoa Tuzo maalum kwa serikali. Aidha, Mikakati iliyofanywa nchini China hivi karibuni imewezesha kuingiwa kwa Mkataba wa kuleta watalii elf 10 kutoka Shangai mwaka 2019. Kushoto ni Balozi wa Urusi nchini, Mhe. Yuri popov. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.