TANGAZO KWA UMMA
TAARIFA KUHUSU UTHIBITISHAJI WA NYARAKA
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuukumbusha Umma
kwamba wale wote wanaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti na nyaraka
mbalimbali wanatakiwa kuzingatia mambo yafuatayo:
(1) Huduma
hizo zinatolewa katika Ofisi za Wizara Mjini DODOMA
jengo la LAPF, Barabara ya Makole Ghorofa la 6.
(2) Malipo
ya nyaraka zitakazothibitishwa yatalipwa kwa njia ya benki, akaunti namba 0150275408200 Foreign Collection Account,
CRDB Bank kwa kiasi cha Shilingi
Elfu Kumi na Tano tu kwa kila nyaraka (@TSHS
15,000/=). Hati ya malipo ya benki iwasilishwe Wizarani ili kuthibitisha
malipo hayo.
(3) Mteja
mwenye nyaraka yeyote inayohusu masuala ya talaka, ndoa, hali ya ndoa, tangazo
la kuzaliwa, cheti cha kuzaliwa, Cheti cha Kifo, cheti cha ndoa anatakiwa
kuanzia ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (Registration,
Insolvency, Trusteeship Agency- RITA) Dar es Salaam.
(4) Vyeti
vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havina budi kupelekwa
kwanza katika Taasisi za Tanzania zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe
na kuthibitishwa. Aidha, kwa vyeti au nyaraka zilizotolewa na mamlaka za nchi
za nje zinatakiwa kupelekwa kwenye Balozi wa nchi amabayo vyeti hivyo
vilitolewa kwa ajili ya uhakiki.
(5) Mteja
anayeleta nyaraka za ajira (Mkataba wa ajira) anatakiwa kuanzia ofisi za Wakala
wa Huduma za Ajira Tanzania (Tanzania Employment Services Agency –TAESA)
(6)Mteja anayeleta
nyaraka iliyo katika lugha tofauti na kingereza anatakiwa kufanya Tafisri ya
nyaraka hiyo na kuiambatisha na nyaraka halisi iliyofanyiwa tafsiri. Aidha,
tafsiri ya nyaraka ifanywe na BAKITA, BAKWATA na taasisi zilizosajiliwa na
kutambulika na Serikali.
(7) Kwa
yeyote mwenye Power of Attorney na Deed Poll ahakikishe imesajiliwa na Wizara
ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi kabla ya kuiwasilisha Wizarani.
(8)Nakala ya nyaraka
yeyote inayotakiwa kufanyiwa uhakiki imbatane na nakala halisi ya nyaraka hiyo.
(9)Mteja
anatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi
tarajiwa ya nyaraka hizo nje ya nchi. Aidha, Barua ya Katibu Mkuu iambatishwe
na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa na taasisi husika ambazo
zinahitaji kuthibitishwa na Wizara.
WATEJA
WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA
JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA SAA 3.00 ASUBUHI HADI SAA 6:00 MCHANA.
Imetolewa na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.