PRESS RELEASE
Tanzania wins the Best Tourist Destination
Award in Russia
Tanzania has won the Award for the ‘’Best Destination to the World’’ in
the Category of Exotic Destination 2018.
Today, on 21st November, 2018, the Ambassador
of Tanzania to Russia, His Excellency Maj. Gen. (Rtd) Simon Mumwi on behalf of the
Government of the United Republic of Tanzania will be receiving a Russian
National Geographical Traveler Award at the ceremony scheduled to be held in
Moscow.
Tanzania won the Award after online voting conducted by
the Russian version of National Geographic Magazine that involved 263,000 online
readers.
Tanzania is winning this Award for the third time since
2011 where Zanzibar was chosen as the Best Beach Tourist Destination in Africa
and therefore awarded the Star Travel Award. Last year, Tanzania also received
a National Geographical Travel Award as the second best destination in the
world in the category of exotic destination.
These achievements reflect efforts made by the
Government of Tanzania through its Embassy in Russia, Ministries of Tourism and
Natural Resources both in Tanzania Mainland and Zanzibar and other Institutions
in tourism industry.
Through these efforts, the volume of Russian tourists visiting
Tanzania has been increasing. For instance; last year (2017) 10,060 tourists
from Russia visited Tanzania as compared to only 4,021 tourists in 2012.
More concerted efforts will be made by the Ministry of
Foreign Affairs and other stakeholders to promote Tanzania as the best tourist destination
in the world and looking forward to see more Russian tourists choosing Tanzania
as their best destination for tourism.
Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African
Cooperation,
Dodoma
21st November 2018.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania
yashinda Tuzo ya Utalii nchini Urusi
Tanzania imeshinda tuzo ya utalii kwa kuonekana ni
eneo bora zaidi la utalii duniani nchini Urusi kwa mwaka 2018 (The Best
Destination to the World in the Category of Exotic Destination 2018).
Leo tarehe 21 Novemba 2018, Balozi wetu nchini
Urusi Mhe. Maj. Gen. (Mst). Simon Mumwi atapokea Tuzo hiyo kutoka Jarida la
kirusi la “National Geographic Magazine” jijini Moscow kwa niaba ya nchi.
Tanzania imepata ushindi huo kutokana na kura
zilizopigwa kwenye mtandao wa jarida hilo la “National Geographic Magazine”
lililoshirikisha wapiga kura 263,000 kwa njia ya mtandao.
Hii ni mara ya tatu katika kipindi cha miaka saba
tokea mwaka 2011, raia wa Urusi kupitia jarida hilo wanaichagua Tanzania kama
eneo bora zaidi la utalii. Mwaka 2011, Zanzibar ilipata tuzo ya ‘Star Travel’
kama eneo bora zaidi la utalii wa ufukweni katika bara la Afrika na mwaka jana,
Tanzania ilipata tuzo ya NGT na Tanzania ilishinda nafasi ya pili katika tuzo
hiyo katika kundi la eneo bora la utalii
duniani.
“National Geographic Traveller Awards” (NGT Awards)
ni tuzo ya kifahari zaidi katika sekta ya utalii nchini Urusi na hutolewa na
Jarida la kirusi la “National Geographic Magazine”.
Mafanikio hayo yanatokana na jitihada zinazofanywa
na Serikali ya Tanzania kupitia Ubalozi wetu Urusi, Wizara za Utalii za
Tanzania Bara na Zanzibar, na Taasisi zote zinazosimamia masuala ya utalii za
ndani na nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii kwa nchi mbalimbali
duniani ikiwemo Urusi.
Kupitia juhudi hizi, idadi ya watalii wanaokuja
Tanzania kutoka Urusi imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka. Kwa mfano, idadi
hiyo imeongezeka kutoka watalii 4,021 mwaka 2012 hadi watalii 10,060 mwaka
2017.
Wizara kupitia Ubalozi wetu itaendelea kuongeza
juhudi za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania na tunategemea kwa
kushirikiana na wadau wengine katika juhudi hizi, idadi ya watalii kutoka Urusi
wanaokuja nchini itaongezeka zaidi.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki,
Dodoma.
21
Novemba 2018
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.