Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akijibu maswali Bungeni kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Augustine Mahiga (Mb).
Dkt. Ndumbaro alianza kwa kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa kumuamini na kumteua kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Ndumbaro akijibu swali kuhusu sababu zinazofanya hadi sasa Tanzania kutoridhia Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Chaguzi na Utawala Bora uliopitishwa mwaka 2017.
Mhe. Naibu Waziri alieleza kuwa Tanzania inachelewa kuridhia kutokana na baadhi ya ibara za mkataba huo kukinzana na Katiba na Sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.