Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Mhe. Prof. Elizabeth Kiondo akifungua mkutano kati ya ujumbe kutoka Makampuni 7 makubwa ya Uturuki na wadau muhimu wa masuala ya uwekezaji jijini Dar es Salaam ambao ni Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Chama cha Wafanyabiashara, wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA), Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mamlaka ya Ukanda Maalum wa Uwekezaji Tanzania (EPZA), Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Katika mkutano huo ambao ulifanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) tarehe 19 Novemba 2018, Prof. Kiondo alieleza kuwa wawekezaji hao kutoka Uturuki wana nia ya dhati ya kuwekeza hapa nchini kwa kuanzia na mikoa ya Dodoma na Simiyu katika sekta za viwanda vya nguo, uongezaji thamani bidhaa za kilimo, ujenzi wa maduka makubwa ya biashara na ujenzi wa hoteli za kimataifa. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.