TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania kupokea Watalii 10,000 kutoka Shanghai mwaka 2019
Bodi
ya Utalii Tanzania (TTB) imesaini makubaliano na kampuni ya Touchroad International Group ya China
kwa ajili ya kusafirisha watalii 10,000 kutoka jiji la Shanghai kutembelea
Tanzania mwaka 2019 kwa kutumia ndege Maalum (chartered flights).
Makubaliano
hayo yalisainiwa sambamba na mikutano ya kutangaza utalii katika soko la China-
Tourism Roadshow katika miji mitano ya China iliyoanza katika jiji la Shanghai
tarehe 12 Novemba 2018.
Mikutano
hiyo ni matokeo ya jitihada za Ubalozi wa Tanzania nchini China kwa
kushirikiana na TTB ambapo katika mkutano wa kwanza uliofunguliwa na Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Aloyce Nzuki, washiriki
mbalimbali zaidi ya 200 walijitokeza wakiwemo makampuni ya utalii (tour
operators), mawakala wa usafirishaji (travel agents), mashirika ya ndege
(airlines), na vyombo vya habari.
Katika mkutano huo, Mkurugenzi wa Bodi ya
Utalii, Bi. Devotha Mdachi alitoa mada maalum kuhusu vivutio vya utalii
vilivyopo nchini Tanzania pamoja na fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii.
Aidha,
makampuni ya utalii kutoka Tanzania yalipata fursa ya kuelezea packages zao za utalii mahsusi kwa soko
la China.
Kadhalika,
Shirika la Ndege la Tanzania lilitumia fursa hiyo kutangaza juu ya mpango wake
wa kuanza safari za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China katika mji wa
Guangzhou mwezi Februari 2019.
Mikutano
ya kutangaza utalii itaendelea kufanyika katika miji mingine ikiwa ni pamoja na
Guangzhou tarehe 14 Novemba 2018, Hong Kong tarehe 16 Novemba 2018, Chengdu
tarehe 19 Novemba 2018 na Beijing tarehe 20 Novemba 2018.
-Mwisho-
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 13 Novemba
2018
|
Balozi wa Tanzania nchini China, Mhe. Mbelwa Kairuki akitoa neno la ukaribisho katika mkutano wa kutangaza vivutio vya utalii uliofanyika Shaghai, China tarehe 12 Novemba 2018. |
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.