TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Dkt.
Mahiga amwakilisha Mhe. Rais Magufuli katika Mkutano Maalum wa Wakuu wa Nchi na
Serikali wa AU
Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya
Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi
Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe
Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo.
Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo
wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa
Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala
na fedha ikijumuisha utendaji.
Mkutano
ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama
Mwenyekiti na Makamishna 6. Maamuzi hayo yataanza kutekelezwa mwaka 2021 baada
ya uongozi wa Kamisheni uliopo sasa kumaliza muda wake. Maamuzi yote
yaliyotolewa yalilenga kuboresha utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.
Mhe.
Waziri aliungana na viongozi wengine waliochangia katika mjadala wa kuboresha
utendaji wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kwa kuunga mkono mabadiliko ya
kitaasisi katika Umoja huo. Mhe. Waziri alieleza kwamba maamuzi hayo yanalenga
kuleta ufanisi kwenye kutekeleza majukumu ya Kamisheni na kuhakikisha Afrika
inapata maendeleo inayostahili haswa kwa kuzingatia Agenda 2063 ya Umoja wa
Afrika.
Katika
Mkutano huo Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Mhe. Paul Kagame alitoa salamu za
rambirambi kwa Serikali za Tanzania, DRC na Malawi kufuatia vifo vya walinda
amani wa nchi hizo nchini DRC.
Mhe.
Waziri alimshukuru Mhe. Kagame kwa salamu hizo za rambirambi na kuahidi kwamba
Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele kupigania amani ya kudumu barani
Afrika.
Mkutano
pia ulijadili Mamlaka ya Wakala wa Maendeleo ya Umoja wa Afrika (African Union Development Agency - AUDA).
Mkutano ulifahamishwa kuwa mchakato wa kubadilisha Taasisi ya Ushirikiano wa
Maendeleo ya Uchumi (New Economic Partnership
for Africa’s Development – NEPAD) kuwa AUDA utakamilika Februari 2019 kama
inavyoelekezwa katika Maaumuzi ya Umoja wa Afrika Na. 691. Mkutano ulikubaliana
na mapendekezo yote kuhusu Mamlaka ya AUDA na kwamba programu na miradi ya AUDA
itafadhiliwa kupitia bajeti ya Umoja wa Afrika na misaada ya washirika wa
maendeleo.
Agenda
nyingine iliyojadiliwa wakati wa mkutano huo ni mabadiliko katika Taasisi ya Mchakato
wa Kujitathimini kiutawala Bora Africa (African
Peer Review Mechanism - APRM), ambapo mapendekezo yalitolewa ya
kuiunganisha APRM kuwa moja ya taasisi za Umoja wa Afrika na kugharamia
shughuli zake kwa kutumia bajeti ya Umoja huo. Aidha, iliamuliwa kuwa Wanachama
wote wa Umoja wa Afrika wawe Wanachama wa APRM na APRM iwe huru katika
kutekeleza majukumu yake.
Agenda
nyingine kuu iliyojadiliwa na kutolewa maamuzi ni mapendekezo ya makadirio
mapya ya viwango vya kuchangia Umoja wa Afrika na mapendekezo ya adhabu kwa
Nchi ambazo zitachelewa kulipa michango yake. Mkutano uliazimia kuitishwa kwa
Mkutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Mabalozi, Wataalam wa masuala ya Fedha
kutoka nchi wanachama na Kamati ya Mawaziri wa Fedha kupitia makabrasha yote
yanayohusu Viwango vya kuchangia na adhabu kwa nchi ambazo hazitoa michango yao
kwa wakati. Mkutano huo, unatarajiwa kufanyika tarehe 28-29 Novemba, 2018,
Addis Ababa, Ethiopia na mapendekezo ya wataalam yatawasilishwa kwenye Kikao
kijacho cha Baraza la Mawaziri mwezi Februari 2019.
Mkutano
pia ulipokea mapendekeo ya mgawanyiko wa majukumu kati ya AU, Jumuiya za
Kikanda na Nchi Wanachama. Mgawanyo wa majukumu unapendekezwa kuwezesha Jumuiya
za Kikanda, Umoja wa Afrika na Nchi Wanachama kila moja kutekeleza majukumu
yake na yale ambayo watachangia kwa pamoja.
Pembezoni
mwa Mkutano huho wa Dharura Wakuu wa Nchi na Serikali walizindua Mfuko wa Amani
wa Umoja wa Afrika (AU Peace Fund) ambao utashughulikia masuala yote ya Amani
na Usalama katika Nchi Wanachama ikiwemo
viashiria vya uvunjifu wa Amani ili kuzuia kuibuka kwa migogoro. Mhe. Waziri
alishiriki katika uzinduzi huo.
-Mwisho-
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 19 Novemba
2018
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.