Wednesday, May 1, 2019

Prof. Kabudi ashiriki maadhimisho ya siku ya Taifa la Uholanzi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye kuadhimisha siku ya Taifa la Uholanzi, kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul.

Prof. Palamagamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Elimu, Biashara na Ujenzi wa Miundombinu. Pia alilipongeza taifa hilo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa Uholanzi kuja kuwekeza nchini kwa wingi, ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Uholanzi ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongza kwa uwekezaji nchni, ambapo imewekeza jumla ya miradi 159 Tanzania.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchi zao hapa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa. 

Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia  kwenye maadhimisho hayo. 
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchni zao hapa pamoja na wageni mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani).



Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Balozi Jeroen Verheul kwa kuwatakia viongozi wa Tanzania na Uholanzi Nguvu na Afya Njema.
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Mabalozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Sehemu Nyingine ya wageni waalikwa wakisalimiana na kubadilishana mawazo wakati wa maadhimisho hayo yakiendelea. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.









Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje washiriki maadhimisho ya Mei Mosi kwa kishindo jijini Dodoma

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,  Mhe. Dkt. Binilith Mahenge (katikati) na viongozi wengine akiwemo Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula (kushoto) wakiwa wamesimama kuwasalimu Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (hawapo pichani) walipopita mbele ya jukwaa kuu wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma tarehe 1 Mei 2019. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka 2019 ni  "Tanzania ya uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi ni sasa".
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) kwa shangwe na furaha huku wakiwa wameinua juu bango lao wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani (Mei Mosi)
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na bango la Wizara wakati wa maadhimisho ya mei Mosi jijini Dodoma.
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi jijini Dodoma
Ilikuwa ni shangwe na furaha kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  kuadhimisha siku yao ya wafanyakazi inayoadhimishwa duniani kote tarehe 1 Mei kila mwaka
Wafanyakazi waWizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa na ari katika kuadhimisha siku yao
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijumuika na wenzao duniani kote kuadhimisha Mei Mosi

Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Juu na chini ni umati wa Wafanyakazi kutoka Wizara, Sekta na Taasisi mbalimbali wakiadhimisha siku ya wafanyakazi duniani


Wafanyakazi wa Wizara ya Mabo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa jukwaani wakati wa maadhimisho ya Mei Mosi
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mgeni rasmi wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Sehemu nyingine ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa uwanjani wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walishiriki kwa wingi kuadhimisha siku yao


Sehemu nyingine ya wafanyakazi hao wakiwa kwenye maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma
Ni nyuso za tabasamu kama zinavyoonekana kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki waliposhiriki kikamilifu maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Watoto hawakuachwa nyuma na wazazi wao ambao ni Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kuja kuadhimisha siku ya mfanyakazi duniani kama inavyoonekana pichani
Juu na chini ni sehemu ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani
Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiungana na wafanyakazi wengine kuimba wimbo wa mshikamano "Solidarity Forever" kama wanavyoonekana pichani


Picha ya pamoja

Tuesday, April 30, 2019

Prof. Kabudi akutana na Naibu Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Sudan


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.),(kulia) akiwa katika mazungumzo na Naibu  Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika  Mashariki na Sudan, Balozi Makila James, katika Ofisi ndogo za Wizara Dar es salaam leo tarehe 30 Aprili, 2019. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.), akimuonesha Naibu  Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika  Mashariki na Sudan, Balozi Makila James (katikati) maeneo  mbalimabali katika ramani alipokuwa akielezea historia ya Tanzania.Kushoto kwake ni kaimu Balozi wa Marekani Mhe. Imni Patterson.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe.Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimuelezea Naibu  Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika  Mashariki na Sudan, Balozi Makila James kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini  Kushoto kwake ni Kaimu Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Imni Patterson.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (DGCU),  cha Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela (wa kwanza kulia) na Afisa Mambo ya Nje wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Albert Philipo, wakifuatilia mazungumzo baina ya Mhe. Prof Palamagamba John Kabudi na Balozi  Makila James.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akiwa katika picha ya pamoja na Naibu  Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika  Mashariki na Sudan, Balozi Makila James (wa pili kushoto), kulia kwake ni Kaimu  Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Imni Patterson. Wengine ni afisa wa Wizara wa Mambo ya Nje, Albert Philipo (wa kwanza kulia) na afisa wa Uchumi katika ubalozi wa Marekani nchini Ann Marie Warmenhoven (wa kwanza kushoto).

Joint Communique



Monday, April 29, 2019

Ubalozi wa Tanzania nchini India waadhimisha miaka 55 ya Muungano

Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda  akiwahutubia washiriki wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iliyofanyika katika Hoteli ya Leela Palace jijini New Delhi, India tarehe 26 Aprili 2019. Katika hotuba yake, Balozi Luvanda alieleza kuwa, Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni wa kihistoria na wa kupigiwa mfano duniani kote. Pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na India ambao umedumu kwa miaka 58.
Mhe. Balozi Luvanda (wa pili kushoto) kwa pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Paspoti, Visa na Diaspora wa (kushoto) na wageni waalikwa wakionesha jarida kuhusu miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lililoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini India na kuzinduliwa rasmi katika hafla hiyo.
Mhe. Balozi Luvanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mhe. Shri Sanjiv Arora ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje wa India anayeshughulikia Masuala ya Kikonseli, Pasipoti, Viza na Diaspora wa India wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
Mhe. Balozi Luvanda akiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wa nchi mbalimbali walioudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.
Mhe. Balozi Luvanda (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Ubalozi wa Tanzania, New Delhi wakati wa hafla ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano.

Mhe. Schreiber asisitiza Tanzania kutosaini mkataba wa EPA


Mbunge na Mwenyekiti wa Kamati inayohusika na Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani Mhe.  Eva-Maria Schreiber amefanya ziara ya siku saba hapa nchini. Mhe. Schreiber amepata fursa ya kutembelea mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Kigoma, ambapo pia amekutana na wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Bunge.


Akiwa nchini  Mbunge huyo ametembelea mradi wa maji ujulikanao kama “Seven Towns Urban Upgrading Programme/ Kigoma Urban Water Supply and Sanitation”. Mradi unafadhiliwa na Umoja wa Ulaya na Serikali ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW). 

Aidha, mradi huo unahusisha mikoa ya Kigoma, Shinyanga na Lindi. Kwa upande wa Kigoma, utekelezaji wa mradi huu ulianza mwezi Machi 2013 na utakamilika mwezi Oktoba, 2019.
Mhe. Schreiber amekutana na kufanya mazungumzo na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo hayo na waandishi wa habari Mhe. Schreiber amesisitiza umuhimu wa Tanzania kutokusaini Mkataba wa Makubaliano ya Kuichumi (EPA) kati ya Jumuiya ya Umoja wa Ulaya na nchi za Afrika.
 Pia alieleza kuwa endapo Tanzania na nchi nyingine za Afrika hazitofaidika na Mkataba huo kwakuwa zitapoteza mapato.  
Sehemu ya waandishi wakimsikiliza kwa makini Mhe. Schreiber
Mhe. Schreiber akiendelea kuzungumza na waandishi wa Habari.





Saturday, April 27, 2019

Ubalozi wa Urusi waadhimisha Muungano kwa Kutangaza bidhaa za Tanzania

Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akitoa neno la ukaribisho kwa wageni mbalimbali walioalikwa kushiriki kilele cha kuadhimisha Siku ya Taifa ya Tanzania (Maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano) yaliyofanyika jijini Moscow tarehe 26 Aprili 2019. Maadhimisho hayo yalipambwa na shughuli mbalimbali zikiwemo Maonesho ya bidhaa na vivutio vya utalii vya Tanzania; kukabidhi vyeti kwa wadau mbalimbali ili kutambua mchango wao katika maendeleo ya uchumi wa Tanzania, hususan katika sekta ya utalii, uwekezaji, sanaa, lugha na utamaduni pamoja na kutoa fursa ya kubadilishana mawazo baina ya Mabalozi na taasisi za Urusi zinazojihusisha na masuala ya uwekezaji. Mwingine katika picha ni Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk.


Naibu Mkurugenzi wa Afrika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi, Bw. George Cherpisk akisoma hotuba katika maadhimisho hayo.
Wageni waalikwa wakiwemo Waheshimiwa Mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi Urusi wakisikiliza hotuba.

Mhe. Balozi Mumwi na Waheshimiwa Mabalozi wa mbalimbali wa nchi za Afrika zenye uwakilishi nchini Urusi wakikata keki ya kuadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanzania.

Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mhe. Maj. Jen. Mstaafu Simon Mumwi akikabidhi cheti kwa mmoja wa wadau wanaochangia maendeleo na ukuaji wa uchumi nchini Tanzania.

Mdau akipokea cheti chake ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika maendeleo ya Tanzania.

Picha ya pamoja ya baadhi ya Waheshimiwa Mabalozi, wageni, maafisa wa ubalozi na wanafunzi wa Kitanzania wanaosoma Urusi walioshiriki katika maadhimisho hayo.


Thursday, April 25, 2019

Vacancy announcement


PRESS RELEASE

Vacancy notice
The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice for the post of Director General available at the African Development Bank (AfDB) for qualified individuals to apply. 


Application details can be found through the following website: http://www.afdb.org. Closing date for application is 1st May, 2019.


The Ministry encourages qualified Tanzanians to apply.


Issued by:
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
25th April, 2019.