Wednesday, May 1, 2019

Prof. Kabudi ashiriki maadhimisho ya siku ya Taifa la Uholanzi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akihutubia kwenye kuadhimisha siku ya Taifa la Uholanzi, kulia ni Balozi wa Uholanzi nchini Mhe. Jeroen Verheul.

Prof. Palamagamba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alitumia fursa hiyo kuelezea mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Uholanzi katika sekta mbalimbali zikiwemo Kilimo, Elimu, Biashara na Ujenzi wa Miundombinu. Pia alilipongeza taifa hilo kwa kuendelea kushirikiana na Tanzania kwenye kuleta maendeleo nchini.

Aidha, Prof. Kabudi alieleza kuwa Tanzania inaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ili kuwavutia wawekezaji wa Uholanzi kuja kuwekeza nchini kwa wingi, ambapo alieleza kuwa mpaka sasa Uholanzi ni miongoni mwa nchi 10 zinazoongza kwa uwekezaji nchni, ambapo imewekeza jumla ya miradi 159 Tanzania.

Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Makamu wa Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mabalozi mbalimbali wanao ziwakilisha nchi zao hapa pamoja na wawakilishi wa mashirika ya Kimataifa. 

Prof. Palamagamba John Kabudi akiendelea kuhutubia  kwenye maadhimisho hayo. 
Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchni zao hapa pamoja na wageni mbalimbali wakimsikiliza kwa makini Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) alipokuwa akihutubia.
Juu na chini ni sehemu nyingine ya wageni waalikwa aliohudhuria maadhimisho hayo wakisikiliza hotuba hiyo ya Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Hayupo pichani).



Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Balozi Jeroen Verheul kwa kuwatakia viongozi wa Tanzania na Uholanzi Nguvu na Afya Njema.
Prof. Palamagamba John Kabudi(Mb.) akigonganisha glasi na Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal.
Prof. Palamagamba John Kabudi akizungumza na Mabalozi pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.
Sehemu Nyingine ya wageni waalikwa wakisalimiana na kubadilishana mawazo wakati wa maadhimisho hayo yakiendelea. 
Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho hayo.









No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.