Wednesday, May 8, 2019

Prof. Kabudi akutana na Mkurugenzi Mkazi wa UNDP anayemaliza muda wake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na  kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Bi. Natalie Boucly, ambaye amemaliza muda wa kuliwakilisha shirika hilo nchini. Katika mazungumzo hayo, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) alimshukuru Bi.Natalie Boucly kwa uwakilishi wake mzuri katika nyanja mbalimbali katika kuchochea maendeleo nchini. 

Pamoja na mambo mengine, Prof. Palamagamba John Kabudi alimweleza Bi.Natalie Boucly ajisikie nyumbani na asisite kuitembelea tena Tanzania pamoja na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini kama mbuga za wanyama na mlima Kilimanjaro pamoja na visiwa vya Zanzibar.  
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimsikiliza Bi. Natalie Boucly wakati wa mazungumzo hayo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Emmanuel Buhohela (wa pili kutoka kushoto), Katibu wa Waziri wa Mambo ya Nje Bw. Charles Joseph Mbando (wa kwanza kulia) pamoja Afisa Mambo ya Nje Bi Diana Mhina wakifuatilia kwa makini mazungumzo ya Prof. Palamagamba John Kabudi na Bi. Natalie Boucly (hawapo pichani)
Prof. Palamagamba John Kabudi akimkabidhi zawadi ya picha yenye mchoro wa vivutio vya utalii nchini Bi. Natalie Boucly.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.