Dodoma, 14 Mei 2019
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawahimiza Watanzania wenye
sifa kuomba nafasi za kazi na masomo zilizotangazwa na jumuiya za kimataifa kama
ifuatavyo:
- i.
Sekretarieti
ya Jumuiya ya Madola;
Afisa
Msaidizi wa Programu katika Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini (Assistant
Program Officer-Monitoring and Evaluation Unit na
Meneja
wa Utafiti–Uchumi, Vijana na Maendeleo Endelevu (Research Manager–Economic,
Youth and Sustainable Development.
Maelezo
kamili kuhusu nafasi hizi yanapatikana katika tovuti: http://thecommonwealth.org/jobs. Mwisho wa kuwasilisha maombi ni tarehe 23 Mei
2019.
Aidha,
Jumuiya ya Madola imetangaza nafasi za ufadhili wa masomo kwa nchi wanachama wa
Jumuiya hiyo katika ngazi ya shahada ya uzamili (masters degree). Mwisho wa
kuwasilisha maombi ya nafasi hizo zinazojulikana kama Queen Elizabeth Commonwealth Scholarship ni tarehe 26 Juni 2019.
Maelezo
kuhusu taratibu za kuomba nafasi hizo yanapatikana kupitia tovuti: www.acu.ac.uk/scholarships/qecs.
- ii Shirika
la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR);
Kamishina
Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Hifadhi kwa Wakimbizi (Assistant High Commissioner
for Protection).
Maelezo
kuhusu nafasi hii yanapatikana kupitia tovuti: https://www.unhcr.org/career-opportunities
ambapo mwisho wa kuwasilisha mombi ni tarehe 20 Mei 2019 katika baruapepe recruitment.AHC-P@unhcr.org.
Imetolewa
na:
Kitengo
cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.