Tuesday, May 7, 2019

Prof. Kabudi awataka Watanzania kumuenzi Dkt. Mengi kwa kuchapa kazi

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akitoa salamu za pole kwa niaba ya Serikali wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya IPP, Marehemu Dkt. Reginald Mengi. Katika salamu hizo, Mhe. Prof. Kabudi ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa. Pia amemwelezea Marehemu Dkt. Mengi kuwa ni mfano wa kuigwa  kutokana na mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa wakati wote wa uhai wake na kwamba ni kiongozi atakayekumbukwa na Watanzania wote na kuwaomba Wanzania kumuenzi kwa kufanyakazi kwa bidii. Ibada ya kuuaga mwili wa Marehemu Dkt. Mengi imefanyika kwenye Ukumbi wa Karemjee jijini Dar es Salaam tarehe 7 Mei 2019 na kuhudhuriwa na Viongozi Wakuu wa Serikali akiwemo Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Sehemu ya viongozi na waombolezaji waliofika kwa ajili ya kuuaga mwili wa Marehemu Dkt. Mengi
Sehemu nyingine ya viongozi na waombolezaji wakiwa kwenye msiba huo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.