Saturday, May 4, 2019

Ubalozi wa Tanzania, Jamhuri ya Korea wafanikisha kwa kishindo maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano

Balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Korea , Mhe. Matilda Masuka akitoa hotuba wakati wa maadhimisho ya kilele cha Wiki ya Tanzania katika kusherehekea miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na miaka 27 ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea. Ubalozi wa Tanzania mjini Seoul uliandaa shughuli mbalimbali za kuitangaza nchi kama vile maonesho ya Tingatinga, maonesho ya Kahawa, semina za biashara, utalii na uwekezaji na kubadilishana utamaduni kupitia mapishi ya vyakula mbalimbali. Pia msaanii maarufu wa Tanzania Abdul Nasib maarufu kwa jina la Diamond alifanya onesho la muziki. Katika hotuba yake Balozi Masuka aliwapongeza watanzania na viongozi wa Tanzania kwa kuulinda Muungano na pia alisifu ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Jamhuri ya Korea.

Sehemu ya wageni waalikwa wakiwa kwenye kilele cha maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar 

Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Korea Mhe. Lee Juyoung baadhi ya mazao yanayolimwa Tanzania ikiwemo korosho wakati wa wiki ya Tanzania kuelekea maadhimishoya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Mhe. Balozi Masuka akimkabidhi Spika huyo majarida na vipeperushi mbalimbali vinavyotangaza vivuytioa vya utalii nchini

Watanzania waishio Korea (TANROK) wakionesha tamaduni za kitanzania kupitia sanaa ya ngoma

Mtaalam wa michoro maarufu ya Tanzania "Tingatinga" akiwafundisha wananchi wa Jamhuri ya Korea kuchora michoro hiyo

Wanafunzi wakiwa wamefuzu na kuonesha michoro yao ya "Tingatinga" inayovutuia

Balozi Masuka akifurahia jambo na wageni waalikwa wakati wa maadhimisho hayo

Balozi Masuka akimkaribisha Seoul msanii wa muziki Diamond alipokwenda kutumbuiza wakati wa maadhimisho ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

Wageni waalikwa wakifurahia muziki kutoka kwa msanii Diamond hayupo pichani

Ratiba ya matukio ya Wiki ya Tanzania jijini Seoul kama inavyoonekana

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.