Thursday, August 22, 2019

WAZIRI KABUDI AMUAGA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI

Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez iliyofanyika hoteli ya Hyatt jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi katika hotuba yake amempongeza Bwana Rodriguez kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chote akiwa nchini. Aidha, amemshukuru kwa kushirikiana na Serikali na kujitoa kwa dhati katika kuchangia juhudi kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa Serikali nchini.

Bwana Rodriguez amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini Tanzania ambapo amefanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano.
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (Kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini, anayemaliza muda wake wa kuhudumu nchi wakifurahia jambo wakati wa hafla fupi ya kumuaga
Bw. Deusdedit Kaganda Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kimataifa akizungumza kwenye hafla fupi ya kumuaga Bw. Rodriguez Maratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu nchini 
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) na Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini wakishirikishana jambo  wakati wa hafla hiyo
Bi.Ramla Khamis Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza katika hafla ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akikabidhi zawadi kwa Bw. Alvaro Rodriguez (kushoto) Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wake wa kuhudumu
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Bw. Alvaro Rodriguez Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini ambaye amemaliza muda wa kuhudumu wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi kutoka wizarani na Ofisi ya Umoja wa Mataifa.

Wednesday, August 21, 2019

WAZIRI KABUDI AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI


Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kizungumza na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Waziri Kabudi katika Mkutano wake na wanahabari amewashukuru nakuwapongeza waandishi wa habari na vyombo vya habari, kwa ushirikiano mkubwa 
na uzalendo waliouonyesha katika kuutangaza Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC).

Waziri Kabudi alitumia fursa hiyo kutoa rai kwa waandishi wa habari kuendelea kufuatilia na kuuhabarisha umma masuala mbalimbali yanayojiri kweny ya Jumuiya SADC.

Tanzania itaendelea kuwa mwenyeji wa Mikutano mbalimbali ya kisekta ya SADC katika kipindi cha hiki cha mwaka mmoja cha Uenyekiti wake.
Bw. Emmanuel Buhohela Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  akizungumza wakati wa Mkutano na Wanahabari uliofanyika katika Ukumbi wa  Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019.


Bibi Agnes Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari

Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano

Meza kuu ikifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea.


Wakati huohuo Waziri Kabudi amepokea ujumbe wa wawaendesha baiskeli unaojumuisha washiriki kutoka nchi wanachama wa Jamuiya ya Afrika Mashariki. Ziara hii ya waendesha baiskeli imeandaliwa na asasi ya kiraia "Camp fire" ya nchini Uganda. Ziara yao inahusisha kuzunguka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza umoja na ushirikiano wa kikanda.

 Akizungumza kiongozi wa waendesha baiskeli hao bwana John Balongo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa ushirikiano na mapokezi mazuri katika kipindi chote walichokuwa nchini. 
Msafara wa waendesha Baiskeli wakiwasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019 

Waziri Kabudi akisalimiana na ujumbe wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki walipowasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere
Waziri Kabudi akimkabidhi bendera ya Taifa mwakilishi wa Tanzania katika ziara ya baiskeli ya Afrika Mashariki, mara baada ya kuwapokea katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Waziri Kabudi akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa ujumbe wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki
Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii (mwenye tai nyekundu) Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki 
Bw. John Barongo, Kiongozi wa msafara wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki akizungumza baada ya mapokezi
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa waendesha baiskeli 

Tuesday, August 20, 2019

WAZIRI KABUDI AFUNGUA KIKAO KAZI MAALUMU CHA MABALOZI WA TANZANIA



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI 
Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi. 
Waziri Kabudi ameyasema hayo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi  kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere  jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 20 hadi  23 Agosti 2019.
Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika  kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. Pia kumekuwa na ongezeko la fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada zaidi ili nchi yetu ifikie azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.
Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.
Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025. 
"Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kuiona miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile pamoja na mambo mengine itarahisha usafirishaji na kumwezesha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo", alisema Balozi Aziz.
Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa na kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
20 Agosti 2019

Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019

Lengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi. 
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. 

Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na  Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani).
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake
Viongozi Wakuu wa Wizara  wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi maalum.
Mhe. Naimi Aziz Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam

MAAZIMIO YA MKUTANO WA 39 WA WAKUU WA NCHI WA SADAC


COMMUNIQUE OF THE 
39TH SADC SUMMIT OF HEADS OF STATE AND GOVERNMENT 
JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE 
DAR ES SALAAM, UNITED REPUBLIC OF TANZANIA 
17 – 18 AUGUST 2019 
1. The 39th Ordinary Summit of the Heads of State and Government of the Southern African Development Community (SADC) was held at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam, United Republic of Tanzania, on the 17th and 18th August 2019. 

2. Summit was attended by the following Heads of State and Government and/or their representatives: 

Angola:                                      H.E. President João Manuel Gonçalves Lourenço 
Comoros:                                   H. E. President Colonel Azali Assoumani 
DRC:                                          H.E. President Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo 
Madagascar:                              H.E. President Andry Rajoelina 
Mozambique:                             H.E President Felipe Jacinto Nyusi 
Namibia:                                    H.E. President Dr Hage G. Geingob 
Seychelles:                                H.E. President Danny Faure 
South Africa:                              H.E. President Cyril Ramaphosa 
United Republic of Tanzania:     H.E. President Dr. John Pombe Joseph Magufuli 
Zambia:                                      H.E. President Edgar Chagwa Lungu 
Zimbabwe:                                 H.E. President Emmerson Dambudzo Mnangagwa. 
Lesotho:                                    Right Hon Prime Minister Dr. Motsoahae Thomas Thabane 
Malawi:                                      Rt. Hon. Everton Herbet Chimulirenji – Vice President 
Eswatini:                                   H.E. The Right Hon. Prime Minister Mandvulo Dlamini 
Botswana:                                 Hon. Dr. Unity Dow – Minister of International Affairs and Cooperation 
Mauritius:                                 Hon. Nandcoomar Bodha – Minister of Foreign Affairs, Regional Integration and International Trade.

Monday, August 19, 2019

MABALOZI WA TANZANIA WATEMBELEA MIRADI YA MAENDELEO ZANZIBAR

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (katikati; ambaye pia aliongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara) akitoa maelezo kwa Mabalozi waliopotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) unaotekelezwa  na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Jumla ya mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani wapo nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Wakiwa Zanzibar Mambalozi wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall), uwanja mpya wa ndege (terminal 3), ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Fumba, ujenzi wa mradi wa barabara ya kilomita 31 (Kitope hadi Mkokotoni) na ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo eneo la Mnangapwani.

Mabalozi wamendelea kuridhishwa na kufahishwa na namna Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) zilivyo jidhatiti kutekeleza miradi mikubwa ambayo itachagiza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. 
Mabalozi wakisikiliza maelezo kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) lililopo eneo la Mapinduzi square, Michenzani  kutoka kwa mtaalam na msimamizi wa mradi huo
Mabalozi wakitembelea maeneo mbalimbali yanayouzunguka maradi kuona shughuli zinazondelea katika eneo hilo
Mabalozi wakiwasili katika jengo la Makubusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar lililopo eneo la Michenzani, ambapo walipata fursa ya kufahamu kwa undani historia na taarifa mbalimbali kuhusu  Mapinduzi ya Zanzibar
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Jengo la Makumbusho ya Kumbukumbu ya Mapinduzi na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki walipotembelea jengo hilo Agosti 19, 2019. 
Balozi Ramadhani Mwinyi Katibu Mkuu wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na wafanyakazi wa mradi wa ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa Zanzibar, alipoongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara ya mradi huo Agosti 19, 2019.
Mabalozi wakisiliza maelezo kuhusu ujenzi wa uwanja mpya wa ndege Zanzibar (Tereminal 3), kutoka kwa Mratibu wa Mradi huo Bw. Yasiri Costa.


Mabalozi wakiwasili eneo la mradi wa ujenzi wa barabara ya Kitope hadi Mkokotoni katika kiwango cha lami yenye urefu wa kilomita 31. Barabara hiyo hadi kukamilika kwake itagharimu jumla ya shilingi za Bilioni 58.6
Mabalozi wakiwa Wameambatana na watumishi wa Wizara wakitembelea eneo la mradi wa ujenzi wa barabara
Ujenzi wa daraja ukiendelea katika barabara ya Kitope-Mkokotoni
Mabalozi wakiwa eneo la ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo Mnangapwani walipotembele eneo la mradi huo Agosti 19, 2019.

Sunday, August 18, 2019

Naibu Waziri akutana na kufanya Mazungumzo na Balozi wa Umoja wa Ulaya, nchini Botswana


Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akisalimiana na Mhe.Jan SADEK Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Botswana walipokutana kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo baina yao yalijikita kwenye masuala mbalimbali yaliyojadiliwa kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Sambamba na hayo katika mazungumzo hayo Dkt. Ndumbaro aliendelea kumueleza Balozi Jan, juu ya umuhimu wa Umoja wa Ulaya kutekeleka wito alioutoa Mhe. Rais Magufuli wakati wa Mkutano wa SADC  kuhusu  kuiondolea nchi ya Zimbabwe vikwazo vya kiuchumi. Balozi Jan alikuwa nchini kuhudhuria Mkutano wa SADC
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza alipokutana kwa mazungumzo na Balozi  Jan.
Mazungumzo yakiendelea
Mhe. Dkt. Ndumbaro akimsikiliza Balozi Jan walipokuna kwa mazungumzo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ndumbaro akisisitiza jambo alipokutana kwa mazungumzo na Balozi Jan.

Saturday, August 17, 2019

MKUTANO WA 39 WA WAKUU WA NCHI NA SERIKALI WA JUMUIYA YA MAENDELEO KUSINI MWA AFRIKA (SADC)


Baadhi ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa Katika Mkutano wa 39 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. 

Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa waafuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania.
Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi,akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi,Zanzibar wakiwa wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. 
Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Alhaji Ali Hassani Mwinyi,akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume

Marais Wastaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi,Zanzibar pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wakifuatilia Mkutano wa 9 wa Jumuiya hiyo unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINCC) Dar es Salaam,Tanzania. 
Kutoka kulia ni Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akifuatiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akifuatiwa na  Rais Mstaafu wa awamu ya sita wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhe. Aman Abeid Karume,akifuatiwa na Makamu wa Rais mstaafu wa awamu ya tatu Dkt Mohamed Gharib Bilali,akifuatiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi John Kijazi na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa,wakiwa wanafuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan,akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaji Dkt. Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatiwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiwa wanafuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. David Cleopa Msuya (wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. John Samuel Malecela (katikati) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. faraji Kassidi Mnyepe wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)

Sehemu ya wahudhuriaji wa Mkutano wa 39 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakifuatilia Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)
Sehemu ya wahudhuriaji wa Mkutano wa 39 Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika wakiwa wamesimama kuimba wimbo wa Taifa wa Tanzania wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaoendelea jijini Dar Es Salaam,Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere(JNICC)