Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, (katikati; ambaye pia aliongoza ujumbe wa mabalozi katika ziara) akitoa maelezo kwa Mabalozi waliopotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la makazi na biashara (Shopping mall) unaotekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Jumla ya mabalozi 42 wanaoiwakilisha Tanzania maeneo mbalimbali Duniani wapo nchini, ambapo pamoja na mambo mengine wametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Wakiwa Zanzibar Mambalozi wametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la biashara na makazi (shopping mall), uwanja mpya wa ndege (terminal 3), ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Fumba, ujenzi wa mradi wa barabara ya kilomita 31 (Kitope hadi Mkokotoni) na ujenzi wa bandari ya mafuta iliyopo eneo la Mnangapwani.
Mabalozi wamendelea kuridhishwa na kufahishwa na namna Serikali zote mbili (Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano) zilivyo jidhatiti kutekeleza miradi mikubwa ambayo itachagiza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.