Saturday, August 17, 2019

Mabalozi wa Tanzania wahitimisha ziara ya miradi maendeleo


Mabalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali duniani wakiwa Makao Makuu  ya Kampuni ya Taifa Gas iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam  walipoitembelea kampuni hiyo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na Kampuni hiyo.

Maeneo mengine ambayo Mabalozi  wametembelea ni pamoja na Uwanja mpya ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Teminal 3) mradi wa ujenzi wa barabara za juu za Ubungo (Ubungo interchange), Mamlaka ya Usimamizi wa Mawasiliano Tanzania (TCRA)  na Ujenzi wa mradi wa dajara jipya la surrender.
Mabalozi wakisikiliza ufanunuzi wa masuala mbalimbali kutoka kwa watendaji wa Kampuni ya Taifa Gas walipoitembela Makao Makuu ya Kampuni hiyo. 
Mhe. Baraka Luvanda Balozi wa Tanzania nchini India (Wakwanza kulia) na Mhe. Matilda Masuka Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Korea wakifuatilia hotuba fupi ya ukaribisho.
Tokea kulia: Mhe. Asharose Migiro Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa Balozi Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, na Mhe. Wilson Masilingi Balozi wa Tanzania Washngton DC wakifuatila hotuba ya ukaribisho ya Taifa Gas, Dar es Salaam 
Mabalozi wakiwa Uwanja Mpya wa Ndege wa Julius Nyerere (Terminal 3) walipotembelea kuona ufanisi wa uwanja huo.  
Mabalozi wakisikiliza ufafanuzi kutoka kwa mtaalam walipotembelea eneo la ujenzi wa barabara za juu eneo la Ubungo, Dar es Salaam
Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki  akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano alipowasili Makao Makuu ya TCRA akiwa ameambatana na ujumbe wa Mabalozi
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa TCRA walipotembelea Makao makuu ya Ofisi hiyo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.