Friday, August 2, 2019

Watoa Huduma Mkutano wa SADC wapigwa msasa

Naibu Kamishna na Mkuu wa Mafunzo ya Jeshi la Polisi Tanzania Ali Lugendo akihutubia kwenye ufunguzi wa mafunzo ya wanafunzi watakao hudumia kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti. Katika Hotuba yake Kamishna Lugendo amewataka wanafunzi hao kuzingatia mafunzo watakayopewa ili kutoa huduma bora na nzuri kwa wageni watakaohudhuria mkutano huo. Ufunguzi huo umehudhuriwa na Mratibu Mkuu wa Itifaki Bw. Batholomeo Jungu (wa pili kutoka kushoto) na Umefanyika katika chuo cha Polisi, Kurasini jijini Dar es Salaam
Juu na Chini ni sehemu ya Wanafunzi hao wakimsikiliza kwa makini Kamishna Lugendo (hayupo pichani)

Sehemu ya wakufunzi wakimsikiliza kwa makini Kamishna Lugendo


Wanafunzi wanaotarajiwa kupewa mafunzo ya namna ya kuhudumia kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti wakifanya mazoezi 
Kamishna Ali Lugendo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa chuo hicho, Mratibu Mkuu wa Itifaki, Bw. Batholomeo Jungu (wanne kutoka kushoto) pamoja na wanafuzi mara bade ya ufunguzi wa Mafunzo ya kutoa huduma bora na nzuri, kwa Wageni watakao hudhuria Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) unaotarajiwa kufanyika nchini mwezi Agosti





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.