Saturday, August 17, 2019

Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC wafunguliwa rasmi

Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa  Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja wa wajumbe mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa Mkutano wa 39 wa Kilele wa Wakuu hao wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa na Jumuiya ukipigwa. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Pamoja na mambo mengine yaliyojiri katika mkutano huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhiwa nafasi ya uenyekiti wa Jumuiya hiyo ambapo atahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja 2019/ 2020

Mkutano huu unaofanyika kwa siku mbili utafikia tamati kesho tarehe 17 Agosti, 2019
Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa SADC wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya Mkutano wa ufunguzi uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaa 
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akikabidhiwa uenyekiti na mwenyekiti anayemaliza muda wake Mhe. Hage Geingob Rais wa Namibia, wakati ufunguzi wa Mkutano wa kilele wakawaida wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akifuatilia tukio hilo.
Dkt. Stregomena Tax Katibu Mtendaji wa SADC, akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za SADC 
Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama wa SADC wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Taifa na SADC ukiwa unapigwa kabla ya kuanza kwa Mkutano
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama za SADC uliokuwa ukiendelea
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama za SADC uliokuwa ukiendelea
Baadhi ya Mambalozi wa Tanzania wanaoiwakilisha nchi sehemu mbalimbali  wakifurahia jambo wakati wa Mkutano uliokuwa ukiendelea wa Wakuu wa nchi na Serikali wa nchi wanachama za SADC
Sehemu nyingine ya Mabalozi wa Tanzania wakifuatilia Mkutano

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.