Mhe. Nahim Azizi Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na Umoja wa Afrika akisalimiana na mfanyakazi wa Bandari ya Dar es Salaam akiwa na ujumbe wa mabalozi wengine walipowasili bandarini hapo kwa ziara ya kikazi.
Wakiwa katika Bandari ya Dar es Salaam mabalozi walipata nafasi ya kutembelea mradi wa ujenzi wa upanuzi wa bandari sambamba na kuongeza kina cha bahari ili kuweza kuhudumia meli zinazobeba mzigo mkubwa.
Mara baada ya kukamilika kwa mradi huo, Bandari ya Dar es Salaam itakuwa na uwezo wa kuhudumia mizigo ya kiasi cha tani milioni 28 kwa mwaka, ikiwa ni mara mbili ya kiwango cha sasa ambapo inauwezo wa kuhudumia mizigo kiasi cha tani milioni 13 pekee.
Aidha, sambamba na kuongezeka kwa uwezo wa kuhudumia mizigo mingi, pia mradi huo utapunguza muda wa kuhudumia meli kutoka masaa 80 kwa meli moja kama ilivyo sasa hadi masaa 30 mara mradi huo utakapo kamilika.
Wakati huo huo mabalozi walitembelea mradi wa ujenzi wa wa reli ya kiwango cha kimataifa (SGR) ambapo walipata fursa ya kuona maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kuanzia Stesheni jijini Dar Salaam hadi Soga mkaoni Pwani.
Mabalozi wamefurahishwa na jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi madhubuti wa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli za kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kasi na ufanisi wa hali ya juu kwa manufaa ya Wananchi. Mabalozi kwa nyakati tofauti wamesema licha ya miradi hii kuliongezea pato Taifa, mara baada ya kukamilika miradi hii itaiweka Tanzania katika nafasi nzuri zaidi ya ushindani wa kibiashara katika soko la Afrika Mashariki na katika ukanda wa Kusini mwa Afrika
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.