Bibi Agnes Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari |
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano |
Meza kuu ikifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea. Wakati huohuo Waziri Kabudi amepokea ujumbe wa wawaendesha baiskeli unaojumuisha washiriki kutoka nchi wanachama wa Jamuiya ya Afrika Mashariki. Ziara hii ya waendesha baiskeli imeandaliwa na asasi ya kiraia "Camp fire" ya nchini Uganda. Ziara yao inahusisha kuzunguka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza umoja na ushirikiano wa kikanda. Akizungumza kiongozi wa waendesha baiskeli hao bwana John Balongo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa ushirikiano na mapokezi mazuri katika kipindi chote walichokuwa nchini. |
Msafara wa waendesha Baiskeli wakiwasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019 |
Waziri Kabudi akisalimiana na ujumbe wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki walipowasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere |
Waziri Kabudi akimkabidhi bendera ya Taifa mwakilishi wa Tanzania katika ziara ya baiskeli ya Afrika Mashariki, mara baada ya kuwapokea katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Waziri Kabudi akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa ujumbe wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki |
Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii (mwenye tai nyekundu) Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki |
Bw. John Barongo, Kiongozi wa msafara wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki akizungumza baada ya mapokezi |
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa waendesha baiskeli |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.