Mkutano ukiendelea
===========================================================
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO WA MAWAZIRI WA MAANDALIZI YA
MKUTANO WA SABA WA TOKYO KUHUSU MAENDELEO YA AFRIKA (TICAD 7) WAFANYIKA JIJINI
YOKOHAMA, JAPAN
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John
Kabudi leo tarehe 27 Agosti 2019 ameshiriki Mkutano wa Mawaziri wa Maandalizi ya
Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (TICAD 7) uliofanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Pacifico jijini Yokohama, Japan.
Mkutano
huo pamoja na mambo mengine unatarajiwa kupitia na kupitisha rasimu ya Azimio
la Yokohama na Mpango Kazi wa Utekelezaji wa Azimio hilo litakalowasilishwa
kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali utakaoanza tarehe 28 hadi 30 Agosti
2019 kwa ajili ya kuridhiwa.
Akifungungua
mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mhe. Kono Taro amezipongeza nchi
za Afrika kwa kupiga hatua katika maendeleo kupitia ushirikiano na Japan na
kwamba nchi yake itaendelea kuunga mkono jitihada zinazofanywa na nchi hizo ili
kuziwezesha kufikia malengo ikiwemo mapinduzi ya viwanda.
Mhe.
Taro alisema kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na Japan kupitia mpango wa TICAD
umeendelea kuimarika tangu kuanzishwa kwa mpango huo mwaka 1993 na kwamba ni
matarajio yake Mkutano wa Saba utakuwa wa tija zaidi kwa pande hizo mbili.
“Nawakaribisha
Mawaziri wenzangu Yokohama ambapo maandalizi ya mkutano wa saba wa kimataifa wa
Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika yanaendelea. Jukumu letu ni kupitia na kupitisha
rasimu ya Azimio la Yokohama na Mpango kazi wake ili hatimaye litunufaishe sote
pale litakapopitishwa na Wakuu wa nchi” alisema Mhe. Taro.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri ambaye pia ni Mwenyekiti Mwenza wa Mkutano huo,
Mhe. Sameh Shoukry ameipongeza Japan kwa kuendelea kuandaa mikutano hiyo ambayo
ina nia ya kuifikisha Afrika katika mapinduzi ya viwanda na kuondokana na
changamoto mbalimbali ikiwemo ukosefu wa ajira kwa vijana na umaskini.
Kwa
upande wake, Naibu Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika ambao ni miongoni
mwa waandaaji wa Mkutano wa Saba wa TICAD, Bw. Kwesi Quartey amesema kuwa,
mkutano huo unafanyika wakati Umoja wa Afrika unaendelea kutekeleza agenda
2063. Agenda hiyo pamoja na mambo mengine inalenga kuziwezesha nchi za Afrika
kufikia maendeleo ya hali ya juu kwenye sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu,
teknolojia na miundombinu.
Kadhalika
Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Kanda ya Afrika kutoka Shirika la Maendeleo
la Umoja wa Afrika, Bw. Lamin Manneh alisema kuwa ushirikiano kati ya Afrika na
Japan kupitia TICAD umekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya Bara la
Afrika. Aliongeza kuwsema kuwa, Shirika lake ambalo linasimamia maendeleo
linaridhishwa na ushirikiano uliopo kati ya Japan na Afrika ambao kwa kiasi
kikubwa umefanikiwa.
Mkutano
wa Saba wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Ushirikiano na Afrika pamoja na mambo
mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano na agenda za
kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi cha miaka
mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
Agenda
za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha
mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na
ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha
amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na
agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa
Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu
Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
Mkutano
huu ambao umewashirikisha Mawaziri kutoka nchi za Afrika, na wadau mbalimbali
wa maendeleo unafanyika ikiwa ni maandalizi ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na
Serikali utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama,
Japan.
27 Agosti 2019
|
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.