Friday, August 16, 2019

Rais Ramaphosa aitembelea kambi ya Wapigania uhuru wa Afrika Kusini iliyopo Mazimbu, Morogoro

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akiwa ameongozana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mhe. Cyril Ramaphosa pamoja na mkewe mara baada ya kuwapokea walipotembelea iliyokuwa Kambi ya Wapigania uhuru dhidi ya ubaguzi wa rangi kutoka Afrika Kusini iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro. Kambi hiyo ni maarufu kwa jina la Solomon Mahlangu mmoja wa wapigaia uhuru aliyewahi kuishi kwenye kambi hiyo. Ziara ya Mhe. Rais Ramaphosa imefanyika tarehe 16 Agosti 2019
Mhe. Rais Ramaphosa akizungumza wakati alipotembelea kambi za wapigaia uhuru kutoka Afrika Kusini zilizopo Mazimbu mkoani Morogoro. Katika hotuba yake alitoa shukrani kwa Watanzania hususan wakazi wa eneo hilo kwa mchango mkubwa walioutoa ikiwemo kutoa eneo na kuwahifadhi wapigania uhuru wa nchi hiyo ambapo alisema amefarijika kukanyaga ardhi hiyo yenye historia kubwa ya ushirikiano wa kindugu kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Pia aliahidi kuhakikisha nchi yake inaimarisha soko la mazao mbalimbali kutoka Morogoro na pia kuifanya kambi hiyo kuwa kituo kikubwa cha utalii.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ziara ya Mhe. Rais Ramaphosa iliyofanyika kwenye kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro. Mhe. Waziri Mkuu alisistiza nchi hizo kuimarisha ushirikiano  wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini
Mhe. Prof. Kabudi naye akizungumza wakati wa ziara ya Rais wa Afrika Kusini mkoani Morogoro
Sehemu ya wadau mbalimbali wakifuatilia hotuba za viongozi

Sehemu nyingine ya wananchi waliojitokeza kwenye ziara ya Mhe. Rais Ramaphosa mkoani Morogoro

Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi akiwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiabo wa Afrika Mashariki, Bw. Emmanuel Buhohela wakati wa ziara ya Rais wa Afrika Kusini kwenye kambi za wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini zilizopo Mazimbu mkoani Morogoro

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika  Mashariki, Bw. Wilbroad Kayombo (katikati) akishiriki na wadau wengine ziara ya Rais wa Afrika Kusini alipotembelea mkoani Morogoro
Wageni waalikwa

Mhe. Waziri Mkuu akimkabidhi zawadi Mhe. Rais Ramaphosa
Mhe. Rais Ramaphosa akiwa ameongozana na Mhe. Waziri Mkuu wakipita kwenye makaburi ya wapigania uhuru kutoka Afrika Kusini yaliyopo Mazimbu, Morogoro
Mhe. Rais Ramaphosa akimsikiliza mmoja wa watoto wa wapigania uhuru aliyezikwa kwenye eneo hilo

Mhe. Rais Ramaphosa akipanda mti wa kumbukumbu mara baada ya kumaliza ziara yake kwenye kambi ya wapigania uhuru kutoka nchini kwake iliyopo Mazimbu, Morogoro

Mhe. Rais Ramaphosa aliumwagia maji mti huo mara baada ya kuupanda

Mhe. Rais Ramaphosa akiweka shada la maua kuwakumbuka wapigania uhuru wa Afrika Kusini waliokufa wakiwa kwenye harakati za kuiokomboa nchi hiyo dhidi ya ubaguzi wa rangi 

Mhe. Rais Ramaphosa akiwaaga wananchi waliojitokeza kwenye ziara yake alipotembelea kambi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini iliyopo Mazimbu, Morogoro

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.