Tuesday, August 27, 2019
Monday, August 26, 2019
WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI PROF. PALAMAGAMBA JOHN KABUDI (MB) ATEMBELEA UBALOZI WA TANZANIA ULIOPO TOKYO NCHINI JAPAN.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa anaingia katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania uliopo Tokyo,Japan. August 26,2019. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika moja ya Maktaba ya vitabu iliyopo katika Ubalozi wa Tanzania - Tokyo,Japan. August 26,2019. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akikagua aina ya vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Ubalozi wa Tanzania Nchini Japan. August,26,2019. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akiwa katika ofisi ya Balozi wa Tanzania Nchini Japan. August 26,2019. |
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MKUTANO WA SABA WA TOKYO KUHUSU
MAENDELEO YA AFRIKA (TICAD 7)
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi amewasili jijini Yokohama, Japan tarehe 26 Agosti kwa ajili ya kushiriki
Mkutano wa 7 wa Kimataifa wa Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika (Tokyo International
Conference on African Development-TICAD 7) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 hadi
30 Agosti 2019.
Mkutano
huu wa Saba utatanguliwa na kikao cha Maafisa Waandamizi wakiwemo Makatibu
Wakuu na Mabalozi tarehe 25 na 26 Agosti 2019 ukifuatiwa na kikao cha Mawaziri
tarehe 27 Agosti, 2019 na utahitimiswa na Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali
tarehe 28 hadi 30 Agosti 2019. Kauli mbiu ya Mkutano huu ni “Kuendeleza
Maendeleo ya Afrika kupitia Watu, Teknolojia na Uvumbuzi”.
Mkutano
wa Saba pamoja na mambo mengine unatoa fursa ya kupanga mikakati ya ushirikiano
na agenda za kimaendeleo zitakazotelezwa kati ya Japan na Afrika kwa kipindi
cha miaka mitatu ijayo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021.
Agenda
za mkutano wa mwaka huu zinalenga kujadili mageuzi ya kiuchumi na kuboresha
mazingira ya uwekezaji kwa kukuza sekta na uvumbuzi. Pia kuimarisha usalama na
ustahimilivu endelevu kwenye jamii pamoja na kuendeleza jitihada za kuimarisha
amani na usalama barani Afrika. Agenda za Mkutano wa Saba zinaenda sambamba na
agenda 2063 ya Umoja wa Afrika, Agenda 2030 ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa
Mataifa na maazimio mengine ya kimataifa kama Mkataba wa Paris kuhusu
Mabadiliko ya Hali ya Hewa.
Kutokana
na mchango wa sekta binafsi katika maendeleo ya kiuchumi barani Afrika, Mkutano
wa TICAD 7 umeandaa ratiba maalum itakayozishirikisha taasisi binafsi na za umma
kwenye majadiliano ya kibiashara yatakayofanyika tarehe 29 Agosti 2019. Lengo
la majadiliano hayo ni kuwaleta pamoja wadau mbalimbali wakiwemo Viongozi wa
Serikali wamiliki wa Kampuni, wafanyabiashara na wawekezaji ili kujadili kwa
pamoja masuala mbalimbali ya kukuza baishara, uwekezaji na utalii kati ya Japan
na Afrika.
Kadhalika wakati wa mkutano wa saba nchi zote za Afrika zimepatiwa nafasi ya kushiriki katika shughuli mbalimbali kwa lengo la
kutangaza fursa za biashara, uwekezaji na vivutio vya utalii za nchi husika. Tanzania kupitia Bodi ya Utalii (TTB) imejipanga kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini wakati wa mkutano huo.
Mkutano
wa Saba wa TICAD utahitimishwa kwa Wakuu wa Nchi kupitisha Azimio la Yokohama
na Mpango Kazi wa utekelezaji wa Azimio hilo. Serikali ya Japan ilianzisha jukwaa
la majadiliano kati yake na nchi za Afrika mwaka 1993 kwa ajili ya kujadili
maendeleo na nchi hizo.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ataongoza
ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.
Imetolewa na:
Kitengo cha
Mawasiliano ya Serikali,
Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Yokohama,
Japan.
26 Agosti 2019
Friday, August 23, 2019
Naibu Waziri Mhe.Dkt Damas Ndumbaro afanya mazungumzo na Mabalozi
Mhe. Dkt Ndumbaro Naibu Waziri akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Sanbe walipokutana kwa mazungumzo. |
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akisalimiana na Mhe. Mousa Farhang Balozi wa Iran nchini Tanzania |
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kulia) akimsikiliza Mhe. Abdelilah Benryane Balozi wa Morocco nchini Tanzania |
Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakati akifanya mazungumzo na Balozi wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane |
Sehemu ya Wafanyakazi wa Ubalozi wa China wakifuatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea |
Thursday, August 22, 2019
WAZIRI KABUDI AMUAGA MRATIBU MKAZI WA UMOJA WA MATAIFA NCHINI
Bi.Ramla Khamis Afisa Mambo ya Nje Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akizungumza katika hafla ya kumuaga Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini |
Wednesday, August 21, 2019
WAZIRI KABUDI AFANYA MKUTANO NA WANAHABARI
Bibi Agnes Kayola Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda akizungumza wakati wa Mkutano na waandishi wa habari |
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mkutano |
Meza kuu ikifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea. Wakati huohuo Waziri Kabudi amepokea ujumbe wa wawaendesha baiskeli unaojumuisha washiriki kutoka nchi wanachama wa Jamuiya ya Afrika Mashariki. Ziara hii ya waendesha baiskeli imeandaliwa na asasi ya kiraia "Camp fire" ya nchini Uganda. Ziara yao inahusisha kuzunguka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa lengo la kukuza umoja na ushirikiano wa kikanda. Akizungumza kiongozi wa waendesha baiskeli hao bwana John Balongo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwapa ushirikiano na mapokezi mazuri katika kipindi chote walichokuwa nchini. |
Msafara wa waendesha Baiskeli wakiwasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam Agosti 21, 2019 |
Waziri Kabudi akisalimiana na ujumbe wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama za Afrika Mashariki walipowasili katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere |
Waziri Kabudi akimkabidhi bendera ya Taifa mwakilishi wa Tanzania katika ziara ya baiskeli ya Afrika Mashariki, mara baada ya kuwapokea katika viunga vya Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam |
Waziri Kabudi akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa ujumbe wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki |
Bw. Eliabi Chodota, Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Kiuchumi na Huduma za Kijamii (mwenye tai nyekundu) Wizara ya Mambo ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza wakati wa mapokezi ya msafara wa waendesha baiskeli kutoka nchi wanachama wa Afrika Mashariki |
Bw. John Barongo, Kiongozi wa msafara wa waendesha baiskeli wa Afrika Mashariki akizungumza baada ya mapokezi |
Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nchi za Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa waendesha baiskeli |
Tuesday, August 20, 2019
WAZIRI KABUDI AFUNGUA KIKAO KAZI MAALUMU CHA MABALOZI WA TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Kabudi afungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi amewataka Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania nje kuongeza jitihada katika kuhamasisha wawekezaji, wafanyabiashara na watalii kuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi.
Waziri Kabudi ameyasema hayo tarehe 20 Agosti 2019 wakati akifungua rasmi kikao kazi maalum cha Mabalozi kinachofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 20 hadi 23 Agosti 2019.
Mhe. Waziri Kabudi alisema kuwa, Mabalozi ambao wana jukumu kubwa la kusimamia maslahi ya Tanzania kwenye nchi mbalimbali duniani, wameendelea kufanya kazi nzuri katika kuhakikisha dhana ya diplomasia ya uchumi inafikiwa na kwamba matokeo ya jitihada hizo ni pamoja na kuongezeka kwa watalii, wawekezaji na wafanyabiashara nchini. Pia kumekuwa na ongezeko la fursa za ufadhili wa masomo na ajira kwa Watanzania kwenye nchi mbalimbali.
“Hii ni mara yangu ya kwanza kukutana nanyi Waheshimiwa Mabalozi tangu niteuliwe na Mhe. Rais kwenye wadhifa huu. Nazipongeza jitihada zenu katika utekelezaji wa diplomasia ya uchumi kwani matokeo tunayaona kwa biashara kuongezeka hapa nchini watalii na hata wawekezaji. Hivyo nataka mwongeze jitihada zaidi ili nchi yetu ifikie azma yake ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025” alisema Mhe. Kabudi”.
Aidha, Mhe. Waziri Kabudi alitoa rai kwa Mabalozi kuendelea kuwahamasisha Watanzania waishio nje (Diaspora) kujiandikisha na kuanzisha jumuiya zao ili kwa namna moja au nyingine na wao washiriki kuchangia maendeleo hapa nchini.
Akizungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili Mabalozi hao ikiwa ni pamoja na uchakavu wa baadhi ya majengo ya balozi, Mhe. Kabudi alieleza kuwa Wizara inaendelea kutafuta suluhisho la kudumu kwa changamoto hizo.
Akizungumza kwa niaba ya Mabalozi, Kiongozi wa Mabalozi hao, Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia alipongeza jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha na kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo Mabalozi walipata fursa ya kuitembelea. Alisema kuwa, miradi hiyo ni chachu ya maendeleo katika kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
"Tunaipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa kuanzisha miradi mikubwa ya kimkakati. Tumepata fursa ya kuiona miradi hiyo ikiwemo ile ya ujenzi wa barabara, reli na umeme. Kimsingi miradi hii inalenga kumwondolea umaskini Mtanzania kwa vile pamoja na mambo mengine itarahisha usafirishaji na kumwezesha mkulima kusafirisha kwa urahisi mazao yake kutoka sehemu moja kwenda nyingine kupitia miundombinu hiyo", alisema Balozi Aziz.
Pia aliipongeza Serikali kupitia Wizara ya mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa na kufanikisha Mkutano wa 39 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kufanyika nchini kwa mafaniko makubwa.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dar es Salaam
20 Agosti 2019
Mhe. Prof. Paramagamba Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam Agosti 20,2019 Lengo la kikao hicho ni kujadili masula mbalimbali yanayohusu utekelezaji wa diplomasia ya uchumi. |
Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe akizumgumza kwenye kikao na Mabalozi wa wanaoiwakilisha Tanzania sehemu mbalimbali duniani. |
Mabalozi na Watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya ufunguzi iliyo kuwa ikitolewa na Waziri Mhe. Prof Kabudi (Hayupo pichani). |
Sehemu ya Watendaji wa Wizara wakifuatilia kikao |
Mabalozi wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Wakuu wa Wizara mara baada ya ufunguzi wa kikao kazi cha Mabalozi |
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi Wanawake |
Viongozi Wakuu wa Wizara wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki mara baada ya ufunguzi wa Kikao kazi maalum. |
Mhe. Naimi Aziz Balozi wa Tanzania Addis Ababa, Ethiopia akitoa hutuba kwenye ufunguzi wa Kikoa kazi cha Mabalozi kinachoendelea katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam |
MAAZIMIO YA MKUTANO WA 39 WA WAKUU WA NCHI WA SADAC
COMMUNIQUE OF THE
39TH SADC SUMMIT OF HEADS OF STATE AND GOVERNMENT
JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CONVENTION CENTRE
DAR ES SALAAM, UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
17 – 18 AUGUST 2019
1. The 39th Ordinary Summit of the Heads of State and Government of the Southern African Development Community (SADC) was held at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar es Salaam, United Republic of Tanzania, on the 17th and 18th August 2019.
2. Summit was attended by the following Heads of State and Government and/or their representatives:
Angola: H.E. President João Manuel Gonçalves Lourenço
Comoros: H. E. President Colonel Azali Assoumani
DRC: H.E. President Félix Antoine Tshisekedi Tshilombo
Madagascar: H.E. President Andry Rajoelina
Mozambique: H.E President Felipe Jacinto Nyusi
Namibia: H.E. President Dr Hage G. Geingob
Seychelles: H.E. President Danny Faure
South Africa: H.E. President Cyril Ramaphosa
United Republic of Tanzania: H.E. President Dr. John Pombe Joseph Magufuli
Zambia: H.E. President Edgar Chagwa Lungu
Zimbabwe: H.E. President Emmerson Dambudzo Mnangagwa.
Lesotho: Right Hon Prime Minister Dr. Motsoahae Thomas Thabane
Malawi: Rt. Hon. Everton Herbet Chimulirenji – Vice President
Eswatini: H.E. The Right Hon. Prime Minister Mandvulo Dlamini
Botswana: Hon. Dr. Unity Dow – Minister of International Affairs and Cooperation
Mauritius: Hon. Nandcoomar Bodha – Minister of Foreign Affairs, Regional Integration and International Trade.
Subscribe to:
Posts (Atom)