Na Mwandishi
Wetu
Taasisi
ya Uongozi yatakiwa kuhakikisha kuwa inaendelea na maradi wa kuweka kumbukumbu sahihi
za viongozi na taifa kwa kuandika vitabu na machapisho mbalimbali yanayowahusu viongozi
nchini Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.
Wito huo
umetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli leo jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akizindua kitabu cha maisha
ya binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa kiitwacho
'My Life, My Purpose'.
"Napenda
kutumia fursa hii, kumpongeza Rais Mstaafu, Mzee Mkapa kwa kuandika kitabu hiki
na kwa mchango wake mkubwa alioutoa na anaoendelea kuutoa kwa taifa letu pia
naipongeza Taasisi ya Uongozi kwa kuratibu zoezi zima la uandishi wa kitabu
hiki kwa kuwa na mambo mengi mazuri" Alisema Rais Magufuli.
Mhe. Rais
aliongeza kuwa kama alivyoeleza Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Prof.
Joseph Semboja kuwa jukumu la taasisi hii ni kuwaanda, kuwaimarisha na
kuwaendeleza vingozi….bila shaka kuratibu na kuchapisha machapisho mbalimbali
ni sehemu ya jukumu hilo hasa barani Afrika.
"Wito
wangu kwenu Taasisi ya Uongozi muangalie jinsi ya kutafsiri kitabu hiki kwa
lugha ya Kiswahili…..naomba kusisitiza viongozi wastaafu wengine waandike
vitabu ili kutoa chachu kwa vijana wetu ambao watakuwa viongozi wa baadae
kujifunza mambo mbalimbali, tusiishie tu kwa viongozi wastaafu katika ngazi ya
Urais bali hata viongozi wengine," Amesema Rais Magufuli.
Rais
Magufuli ameongeza kuwa nitafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif, …….nitafurahi
kusoma kitabu cha mzee Warioba…… nitafurahi kusoma kitabu cha Spika Job Ndugai kuwa
nae amezaliwa kongwa.
Uzinduzi
wa kitabu cha maisha binafsi ya Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. William
Benjamin Mkapa kijulikanacho kwa jina la "My Life, My Purpose" ulihudhuriwa
na Rais wa Mstaafu wa awamu ya pili, Mhe. Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu wa
awamu ya Tatu Mhe. Benjamini William Mkapa na Rais wa awamu ya Nne Mhe. Jakaya
Mrisho Kikwete pamoja na Rais wa Zanzibar, Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed
Shein.
Mbali na
kuzindua kitabu hicho, pia leo ilikuwa ni siku muhimu kwa Rais Mstaafu wa awamu
ya Tatu, kwani leo alikuwa akisheherekea kumbukizi ya siku yake ya kuzaliwa
akiwa ametimiza miaka 81 ya kuzaliwa.
Viongozi mbalimbali
waandamizi wa Serikali waliohudhuria uzinduzi wa kitabu hicho ni pamoja na Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, Katibu Mkuu Kiongozi John Kijazi, Spika wa Bunge la
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai na Balozi wa Finland Nchini Tanzania
Riita Swan
Wengine ni
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Elimu na
Sayansi, Prof. Joyce Ndalichako, Mabalozi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba
na Sheria, Bw. Amon Mpanju, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda,
viongozi wa vyombo vya ulinzi na Usalama, wakuu wa mikoa, viongozi wa dini,
wakuu wa taasisi mbalimbali na asasi za kiraia.
Awali
akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli, Rais Mstaafu Mhe. Benjamin Mkapa alimpongeza Rais Magufuli kwa
jitihada zake za kuhakikisha kuwa taifa linajitegemea hasa katika maendeleo.
"Kujitegemea
ni muhimu sana kama nchi, na ni muhimu kwa heshima ya taifa letu" amesema
Rais Mkapa.
|