Maafisa Waandamizi wa nchi za SADC wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano kutokea nchini Tanzania kupitia mfumo wa video |
Mkutano ukiendelea.
|
Maafisa Waandamizi wa nchi za SADC wakifuatilia hafla ya ufunguzi wa mkutano kutokea nchini Tanzania kupitia mfumo wa video |
Mkutano ukiendelea.
|
Mhe. Prof. Kabudi akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya NUU |
Wajumbe wa Kamati ya NUU akiwemo Mhe. Vuai Nahodha (kulia) wakimsikiliza Prof. Kabudi (hayupo pichani). Kushoto ni Mhe. Augustino Masele. |
Wajumbe wengine wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe. Bonnah Kaluwa na Sophia Mwakagenda nao wakimsikiliza Mhe. Prof. Kabudi ambaye hayupo pichani |
Mhe. Masoud Abdalla Salim, Mjumbe wa Kamati akichangia hoja wakati wa ziara yao kwenye Ofisi za Wizara zilizopo Mtumba, Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akimsikiliza Mjumbe wa Kamati, Mhe. Silafu Maufi alipotoa ushauri kwa Wizara kuhusu kuboresha maeneo kadhaa ya Jengo walilotembelea |
Mhe. Almas Maige, Mjumbe wa Kamati naye akizungumza. Kulia ni Mhe. Ruth Mollel na Mhe. Mhandisi Gerson Lwenge (kushoto) |
Sehemu ya Wakuuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Bw. Ng'imba ambaye hayupo pichani |
Msimamizi wa Miradi ya Majengo ya Wizara, Mhandisi John Kiswaga akijibu hoja kadhaa zilizowasilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama wakati wa ziara yao Wizarani |
Mhe. Mwakagenda akizungumza wakati wa ziara yao |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaeleza jambo Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama walipotembelea chumba cha ofisi yake wakati wa ziara yao kwenye jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akimwonesha Mhe. Mwambalaswa mandhari ya nje ya jengo akiwa ndani ya ofisi yake |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama chumba cha wageni mashuhuri kilichopo kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba |
|
Mhe. Prof. Kabudi akiwaonesha eneo la nje la Jengo la Wizara |
Mhe. Mwambalaswa akimweleza jambo Mhe. Prof. Kabudi |
Jengo la Wizara kama linavyoonekana |
Mhe. Prof. Kabudi akiwaongoza Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama kurejea ndani mara baada ya kutembelea eneo la nje la Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi akijadiliana jambo na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao. |
Mhe. Prof. Kabudi akiagana na Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama mara baada ya kukamilisha ziara yao kwenye Jengo la Wizara lililopo Mtumba jijini Dodoma ====================================================
WAJUMBE WA KAMATI YA BUNGE YA NJE, ULINZI NA USALAMA WATEMBELEA JENGO LA WIZARA LILILOPO MTUMBA
Wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU)
wakiongozwa na Mhe. Victor Mwambalaswa (Mb.), Mwenyekiti wa Kamati hiyo
wamefanya ziara ya kikazi kwenye Jengo la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki lililopo kwenye Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma leo
tarehe 15 Machi 2020.
Wajumbe
hao ambao wapo kwenye program ya kukagua miradi iliyopo kwenye Wizara
zinazosimamiwa na Kamati hiyo, wamepokelewa na mwenyeji wao Mhe. Prof.
Palamagamba John Kabudi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki mara baada ya kuwasili.
Wakizungumza
wakati wa ziara hiyo, baadhi ya Wajumbe hao, wameipongeza Wizara kwa kukamilisha ujenzi
wa jengo hilo kwa wakati ikiwa ni utekelezaji wa azma ya Serikali ya Awamu ya
Tano ya kuhamia Dodoma. Pia wameishauri Wizara kuendelea kuboresha maeneo
kadhaa katika jengo hilo ikiwa ni pamoja na kuweka uzio kuzunguka jengo hilo na
kukamilisha mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kuboresha mawasiliano. Vilevile,
Wajumbe wa Kamati hiyo wameitaka Wizara kuzingatia kanuni za ujenzi wa majengo
ya Ofisi za Mambo ya Nje pale Wizara itakapoanza ujenzi wa jengo lake la kudumu
katika siku zijazo.
Kwa
upande wake, Mhe. Prof. Kabudi aliahidi kutekeleza ushauri uliotolewa na
Wajumbe wa Kamati hiyo na kuwahakikishia kuwa, mapungufu kadhaa yaliyopo
yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.
Aidha,
akitoa taarifa fupi kuhusu ugonjwa wa Corona kwa Wajumbe wa Kamati hiyo, Mhe.
Prof. Kabudi alisema kuwa, Serikali ya Tanzania imechukua hatua madhubuti kwa
ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo endapo utaingia nchini. Hatua hizo ni
pamoja na mikutano ya kikanda kuanza kufanyika kwa njia ya video ukiwemo
Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)
utakaofanyika nchini kuanzia tarehe 16 hadi 18 Machi 2020.
Pia
Kamati ya Kitaifa inayojumuisha Sekta mbalimbali imeundwa kwa ajili ya kuandaa
mikakati mbalimbali ya kukabiliana na ugonjwa huo. Kadhalika vifaa, wataalam na
maeneo ya karantini tayari yametengwa kwa ajili ya kukabiliana na ugonjwa huo.
“Tanzania
inaendelea kuchukua tahadhari mbalimbali kuhusu ugonjwa wa Corona ambao hadi
sasa haujaingia nchini. Hatua hizo ni pamoja na kuandaa mikutano ya kikanda
ambayo itafanyika kwa njia ya video. Katika kutekeleza hilo, Mkutano wa Baraza
la Mawaziri wa SADC unaoanza tarehe 16 Machi mwaka huu utafanyika kwa njia ya
video na utafuata taratibu zote za mikutano ya kikanda wakati wa ufunguzi”
alisisitiza Prof. Kabudi.
Jengo
la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambalo lipo Mtumba
jijini Dodoma lina ukubwa wa Mita za Mraba 1,002 na vyumba 17 vyenye matumizi
mbalimbali zikiwemo Ofisi. Jengo hilo lilianza kujengwa mwezi Desemba 2018 na kukamilika
mwezi Machi 2019.
|
Sehemu ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma |
Sehemu nyingine ya Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nao wakifuatilia hotuba ya Mhe. Prof. Kabudi (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara hiyo uliofanyika jijini Dodoma |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Kanali Ibuge naye akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika jijini Dodoma |
Mhe. Prof. Kabudi na wajumbe wengine wakimsikiliza Katibu Mkuu, Balozi Kanali Ibuge (hayupo pichani) |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Baraza hilo |
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Amani Simon Msuya akiwa na Mwakilishi wa TUGHE-Dodoma wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Wajumbe wa Baraza la Wafanayakazi wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano |
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano wa Baraza hilo |
Wajumbe wa Baraza wakiwa kwenye ufunguzi wa mkutano |
Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya nae akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu TUGHE-Taifa, Bw. Msuya (hayupo pichani) |
Sehemu nyingine ya Wajumbe wa Baraza |
Mjumbe wa Baraza la Wafanayakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Zanzibar, Balozi Mohammed Hamza akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Wajumbe wa Baraza hilo wakati wa ufunguzi |
Sehemu ya Wajumbe wa Baraza wakimsikiliza Balozi Hamza (hayupo pichani) |
Wajumbe wa Baraza |
Wajumbe wengine wa Baraza |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu, Balozi Ibuge na Wajumbe wa TUGHE-Taifa na Wizarani |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ambao pia ni Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa Baraza hilo |
Mhe. Prof. Kabudi akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wote wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki |