Picha ya Rais wa Burundi Hayati Pierre Nkurunziza wakati wa uhai wake.
|
Sunday, June 14, 2020
WACHEZAJI WA MASHINDANO YA DIPLOMATIC GOLF' WAMUAGA MKURUGENZI MKAAZI WA WFP
Wachezaji
wa Mashindano ya Diplomatic Golf mchezo
ambao unaoratibiwa na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wamemuaga mchezaji mwenzao ambae pia ni
Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael
Dunford.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro,
amebainisha hayo wakati walipokuwa wakifanya mazoezi pamoja na wachezaji
wengine akiwemo, Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford leo katika
viwanja vya gymkhana jijini Dar es Salaam.
Tumekutana
Jijini Dar es Salaam, kumuaga mcheza mwenzetu Michael Danford gofl ambaye
anakwenda Nairobi kikazi……. limekuwa pambano kali lakini tumemaliza salama.
Pia
tutakuwa na fursa ya kumpa zawadi zilizoandaliwa na wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na washindi wengine.
Mchezo
wa leo ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kumuaga Bw. Michael Dunford ambaye amemaliza
muda wake wa kufanya kazi hapa nchini ambapo kwa sasa amepangwa kikazi katika nchi
jirani ya Kenya.
"Diplomatic
Golf, ni fursa mahsusi kwa mawaziri, wabunge, wanasiasa, wanadiplomasia na
wananchi wote wa kawaida kukutana na kubadilishana uzoefu wa mchezo huo na
kutengeneza njia mbadala ya kuikuza tasnia hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali
wapenda golf," Amesema Dkt. Ndumbaro.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)
Bw. Michael Dunford amesema kuwa mchezo ulikuwa mzuri na wakufurahisha.
"Mchezo
wetu wa leo ulikuwa mzuri sana na wakufuraisha…..mimi pamoja na Naibu Waziri,
Dkt. Ndumbaro tumepata alama sawa," Amesema Bw. Dunford
Mwaka
2019, Mashindano ya Diplomatic Golf yalifanyika visiwani Zanzibar katika
Viwanja vya Zanzibar Golf Course Sea Cliff, ambapo mwaka huu yanatarajiwa kuwa
tofauti huku vitu vingi vikiwa vimeboreshwa zaidi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akicheza golf katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam |
Wachezaji
wa Mashindano ya Diplomatic Golf wakiwa
katika picha ya pamoja katika viwanja vya gymkhana leo jijini Dar es Salaam
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akimkabidhi Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford moja kati ya zawadi zilizoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje |
Mkurugenzi
mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford akipokea moja kati ya zawadi zilizoandaliwa
na Wizara ya Mambo ya Nje kutoka kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akiagana na Mkurugenzi mkaazi wa (WFP) Bw. Michael Dunford |
DKT. NDUMBARO ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO CHA RAIS NKURUNZIZA
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) amesaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini kufuatia
kifo cha Rais wa Taifa hilo Pierre Nkurunziza aliyefariki Juni 08, 2020.
Akizungumza
mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi ubalozi wa Burundi nchini, Jijini Dar es Salaam Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa wananchi wote wa Burundi na kuwasihi kuendelea
kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba.
"Kusaini
kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu
na ndugu zetu wa Burundi. Kifo cha Rais Nkurunzinza kinawahusu pia watanzania
kwa sababu Rais Nkurunzinza ni Rais aliyekuwa karibu sana na Tanzania kuliko
nchi nyingine yeyote ile, lakini pia Burundi ipo karibu sana na Tanzania,
Amesema Dkt. Ndumbaro.
Naibu
Waziri, Dkt. Ndumbaro ameongeza kuwa, Pengo la Rais Nkurunzinza ni pengo kubwa
sana kwa watanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na Afrika kwa ujumla.
Nae
Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho, amemshukuru Naibu Waziri wa
mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro kwa kufika
kwake kuhani msiba huo na kuongeza kuwa hali hiyo inaonesha upendo ambao unaendelea
kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya mataifa hayo mawili.
Aidha,
Serikali ya Burundi kupitia ubalozi wake hapa nchini, imetoa mualiko kwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kushiriki
mazishi ya Rais Nkurunzinza yanayotarajiwa kufanyika Alhamisi tarehe 18 Juni
2020 nchini Burundi.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro
(Mb) akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini
Dar es Salaam
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Ndumbaro akisaini
kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Burundi nchini leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto kwake ni Balozi wa Burundi nchini, Mhe. Gervais Abayeho.
Friday, June 12, 2020
KATIBU MKUU BALOZI BRIGADIA JENERALI IBUGE AMEKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA UJUMBE KUTOKA NMB
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigadia Jenerali Wilbert A.Ibuge akisimsikiliza Bw. Jeremiah Lymo kutoka NMB wakati akiwasilisha mada. |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigadia Jenerali Wilbert A. Ibuge akichangia jambo wakati wa mazungumzo na ujumbe kutoka NMB |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigadia Jenerali Wilbert A. Ibuge akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa NMB na baadhi ya Watumishi wa Wizara |
Thursday, June 11, 2020
MKURUGENZI MKAZI WA WFP APONGEZA UAMUZI WA RAIS DKT.JOHN POMBE MAGUFULI WA KUTOWEKA ZUIO LA KUTOKA NJE (LOCKDOWN) KATIKA KIPINDI CHA MAPAMBANO YA UGONJWA WA COVID 19.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford ametembelea vikundi vya wakulima vinavyofadhiliwa na miradi ya Shirika hilo Kibaigwa mkoani Dodoma. Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kupata mrejesho wa maendeleo ya mradi kutoka kwa wanakikundi, na kupokea mapendekezo ya kuboresha maradi huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford, akimsikiliza mmoja wa wanufaika wa ufadhili wa WFP alipowatembelea wanufaika hao Kibaigwa, Dodoma. |
Wanakikundi wakiwa katika majadala na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bw. Michael Dunford . |
Monday, June 8, 2020
SERIKALI YAAGIZA CHUO CHA DIPLOMASIA KUONGEZA TAFITI, MACHAPISHO
Serikali
imekiagiza Chuo cha Diplomasia kujikita kuongeza tafiti pamoja na machapisho
mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wahitimu wa chuo hicho kutoa mchango wao katika
Taifa hususani wakati huu wa utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi.
Maagizo
hayo yametolewa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) wakati alipotembelea
chuo hicho na kuongea na wahadhiri, wafanyakazi pamoja na wanafunzi.
Dkt.
Ndumbaro amesema ili chuo cha diplomasia kiendelee kuheshimika zaidi duniani lazima
kihakikishe kuwa kinazalisha tafiti na machapisho ya kutosha.
"Utafiti
na machapisho siyo suala la wahadhiri peke yao…..siyo suala la wanafunzi peke
yao ni suala la wanachuo…… mawazo yenu lazima yafanyiwe utafiti kwa kushirikiana
na wahadiri wenu na ni lazima tuwe na machapisho zaidi," Amesema DKt.
Ndumbaro
Naibu
Waziri ameongeza kuwa moja kati ya changamoto inayoikumba diplomasia hivi sasa ni
mabadiliko ya mifumo mbalimbali duniani ambapo wanadiplomasia wanapaswa kujua
kuwa dunia ipo katika mlengo upi, hivyo vyema mkajikita katika tafiti zenu ili
kuweza kusaidia kufafanua masuala ya kidiplomasia na uhusiano wa kimataifa
yanayotokea duniani.
"Lakini
pia niliagiza muongeze lugha zaidi kwa sababu pia diplomasia pia ni mawasiliano
na unawasiliana na watu wa lugha tofauti tofauti, kwa hiyo tuongeze lugha
mbalimbali ili diplomasia iweze kufanya kazi yake," Amesema DKt. Ndumbaro.
Aida,
Naibu Waziri ameagiza pia chuo hicho kuanzisha semina za kila mwezi ambapo
zitajumuisha Wahadiri na wanafunzi pamoja na mabalozi wastaafu kwa lengo la
kujadili mambo yanayohusu diplomasia na kuwapa uzoefu wa masuala ya
kidiplomasia.
Wanafunzi
kwa upande wao wamepata fursa ya kumuelezea Naibu Waziri changamoto mbalimbali zinazo
wakabili zikiwemo za kupata asilimia ndogo za mkopo wa elimu ya juu, ukosefu wa
mafunzo kwa vitendo, ukosefu wa mabweni pamoja na mazingira ambayo siyo wezeshi
kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum.
"Mkopo
tunaopewa ni mdogo sana na hautoshi hivyo tunaomba serikali itusaidie kutuongezea
fedha za mkopo ili tuweze kukidhi mahitaji yetu wakati tunapokuwa chuoni,"Amesema
Isack Sadock
Pia,
Dkt. Ndumbaro baada ya kusikiliza changamoto zinazowakabili wanafunzi chuoni hapo,
ameuagiza uongozi wa chuo kuandaa na kuratibu mafunzo kwa vitendo badala ya kufuatiliwa
na wanafunzi, kutoa huduma stahiki kwa wanafunzi wenye ulemavu/maitaji maalumu
ili waweze kusoma katika mazingira mazuri.
Nae
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Jeremia Ponera amemhakikishia Naibu
Waziri kuwa chuo kitayafanyia kazi na kuyatekeleza maagizo yote aliyoyatoa.
"Mhe.
Naibu Waziri naomba nikuhakikishie kuwa maagizo yako tumeyapokea……….mimi kwa
kushirikiana na menejimenti, wahadhiri na wafanyakazi tayafanyia kazi kwa
wakati," Amesema Dkt. Ponera
Aidha,
Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro amekagua mradi wa ujenzi wa jengo jipya la chuo cha
Diplomasia.
Katika
hatua nyingine, ametoa msimamo wa Serikali kuhusu changamoto zinazojitokeza
mipakani hasa katika mpaka wa Tanzania na Kenya na kusema kuwa Serikali ipo
kwenye mazungumzo na Kenya ili kuweza kubaini tatizo ni kitu gani.
"Kwa
sasa tupo kwenye majadiliano na wenzetu wa Kenya na kuona tatizo ni kitu gani
je ni corona tu au ni zaidi ya corona? Msimamo wa serikali yetu ni kuwa kila nchi
ipime watu wake…..na tunaamini huo ndiyo msimamo sahihi wa diplomasia ya uchumi,"
Amesema Dkt. Ndumbaro.
Chuo
cha Diplomasia kilianzishwa rasmi tarehe 13 Januari 1978 kwa kusainiwa
Makubaliano yaliyofanywa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wa wakati huo,
Mhe. Benjamini William Mkapa wa Tanzania na Mhe. Joaquim Chissano wa Msumbiji.
Baadhi ya wanafunzi wakimsikiliza Mhe. Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (hayupo pichani) |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro akiongea na wanafunzi (hawapo pichani) |
Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro akioneshwa mchoro wa jengo jipya la chuo cha Diplomasia na meneja mradi Abdalla Khama |
Meneja mradi wa jengo jipya Abdalla Khama akimuelezea jambo Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro wakati alipotembelea eneo la mradi |
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia, Dkt. Jeremia Ponera (aliyesimama) akimkaribisha Naibu Waziri, Dkt. Ndumbaro (aliyekaa wa kwanza kushoto) kwenye kikao cha menejimenti ya chuo |
Saturday, June 6, 2020
NCHI ZA NORDIC ZAAHIDI KUENDELEZA, KUIMARISHA UHUSIANO WAKE NA TANZANIA
Nchi za NORDIC ambazo ni Norway, Sweden, Finland na
Dernmark zimeahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuhakikisha kuwa
Tanzania inasonga mbele katika maendeleo yake kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Akiongea wakati wa maadhimisho ya wiki ya Nordic
jijini Dar es Salaam, Balozi wa Norway nchini, Mhe. Elisabeth Jacobsen amesema
kuwa nchi za Nordic zimeadhimisha wiki ya Nordic nchini Tanzania na zimejadili
masuala ya malengo ya maendeleo endelevu ambapo pamoja na mambo mengine, wametumia
wiki ya Nordic kuendeleza uhusiano na ushirikiano mkubwa uliopo kati ya Nordic na
Tanzania.
"Wiki ya Nordic inatoa fursa ya kushirikiana na
kujifunza mambo mbalimbali yakiwemo ya kijamii, kisiasa na kichumi pamoja na kupata
uzoefu wa maendeleo kutoka kwa kila mmoja wetu," Amesema Balozi Jacobsen.
Ameongeza kuwa, nchi za Nordic zimejidhatiti kufanya
kazi kwa karibu na Tanzania ili kuhakikisha kuwa Tanzania inasonga mbele katika
maendeleo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiongea mara baada ya kukabidiwa mpira ulioandikwa malengo 17 ya maendeleo endelevu ikiwa ni ishara ya kuhamasisha maendeleo ya Tanzania, amesema kuwa mpira huo ni ishara ya ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na nchi za Nordic.
"Ushirikiano wetu (Tanzania) na nchi za Nordic
ni wa muda mrefu kabla ya uhuru na hata baada ya uhuru. Tumekuwa tukifurahia ushirikiano
wetu na nchi za Nordic na umekuwa ukimarika kila wakati, ni matumaini yetu sisi
kama serikali kuwa uhusiano utaendelea kuimarika zaidi," amesema Dkt.
Ndumbaro
Mwezi Novemba 2019, ulifanyika Mkutano wa Mawaziri
wa Mambo ya nje wa Afrika na Nordic, ambapo pamoja na mambo mengine, mkutano
huo uzikutanisha nchi za Afrika na Nordic na kutoa fursa ya kujadili masuala mbalimbali
yakiwemo, elimu, kilimo biashara na uwekezaji.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akiwaelezea jambo Mabalozi wa nchini za Nordic |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na mabalozi wa nchini
za Nordic wakiwa
wameshikilia mpira ulioandikwa malengo 17 ya maendeleo endelevu
|
Thursday, June 4, 2020
Monday, June 1, 2020
KATIBU MKUU BALOZI KANALI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA TAIFA LA ISRAEL KWA TANZANIA
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Kanali Wilbert A. Ibuge akifafanua jambo kwa Balozi wa Taifa la Israel nchini Mhe.Balozi Oded wakati wa mazungumzo. |
Subscribe to:
Posts (Atom)