Thursday, February 4, 2021
IOM YAIPONGEZA TANZANIA KWA KUWASAMEHE RAIA WA ETHIOPIA
Wednesday, February 3, 2021
BALOZI BRIGEDIA GENERALI IBUGE AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI LUVANDA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi na ujumbe wa Tanzania wakifuatilia ufunguzi wa Mkutano wa 38 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia ya video.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi akifuatilia ufunguzi wa Mkutano huo unaofanyika kwa njia ya video.
Mkutano wa Kawaida wa Baraza la
Mawaziri wa Umoja wa Afrika unaofanyika kwa njia video (video conference) umeanza.Mkutano huo umefunguliwa na Mwenyekiti wa
Baraza la Mawaziri la Umoja huo na Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa
Kimataifa wa Afrika Kusini Mhe. Dkt. Naledi Pandor
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi ameongoza ujumbe wa Tanzania kutokea katikaa mji wa Serikali Mtumba ulioko Makao Makuu ya nchi jijini Dodoma.
Mkutano huo wa kawaida wa siku mbili unaongozwa na Mwenyekiti wa
Baraza hilo Mhe. Dr. Naledi Pandor Waziri wa Ushirikiano na Uhusiano wa
Kimataifa wa Afrika Kusini pamoja na mambo mengine utaandaa rasimu ya agenda za
Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika
utakaofanyika tarehe 6 na 7 Februari, 2021 kwa njia video
Mkutano huo unajadili na kupitisha mapendekezo ya taarifa ya
Mkutano wa 41 wa Kamati ya Kudumu ya Uwakilishi (Permanent Representatives Committee –PRC),taarifa ya hali ya
ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19)
Barani Afrika na taarifa ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Baraza la Mawaziri
ya Tathimini na Kamati ya Mawaziri 15 wa Fedha.
Mkutano
pia utafanya uchaguzi na Uteuzi wa Wajumbe Sita (6) wa Bodi ya Ushauri ya
Masuala ya Rushwa ya Afrika, Makamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na
Majaji wanne (4) wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Tuesday, February 2, 2021
MKUTANO WA 38 WA BARAZA LA MAWAZIRI WA UMOJA WA AFRIKA KUFANYIKA KWA NJIA YA MTANDAO
Mkutano wa Kawaida wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika unatarajiwa kufanyika tarehe 3 na 4 Februari, 2021 kwa njia mtandao (video conference).
Mkutano huo pamoja na mambo mengine utaandaa rasimu ya agenda za Mkutano wa 34 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika utakaofanyika tarehe 6 na 7 Februari, 2021.
Mkutano huo utajadili
na kupitisha mapendekezo ya taarifa ya Mkutano wa 41 wa Kamati ya Kudumu ya
Uwakilishi (Permanent Representatives
Committee –PRC),taarifa ya hali ya ugonjwa wa Homa Kali ya Mapafu (COVID-19) Barani Afrika na taarifa ya
Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Baraza la Mawaziri ya Tathimini na Kamati ya
Mawaziri 15 wa Fedha.
Mkutano pia
utafanya uchaguzi na Uteuzi wa Wajumbe Sita (6) wa Bodi ya Ushauri ya Masuala
ya Rushwa ya Afrika, Makamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika na Majaji wanne
(4) wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu.
Friday, January 29, 2021
PROF. KABUDI ATEMBELEA MAONESHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA
Tuesday, January 26, 2021
NAIBU WAZIRI OLE NASHA AKUTANA NA SPIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI JIJINI DODOMA
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (wa Pili Kulia)) akiwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin Ngaga (wa pili kushoto) walipokutana Ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. William Ole Nasha (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Martin K. Ngoga ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 26 Januari, 2021.
Viongozi hao wamejadili namna watakavyoimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Bunge hilo la Afrika Mashariki na kuliwezesha Bunge hilo kutekeleza majukumu yake kikamilifu huku likizingatia sheria, kanuni , taratibu na uadilifu.
Amemuomba Mhe. Spika kuendelea kulisimamia Bunge hilo kwa kufuata Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki, Itifaki na Kanuni za Jumuiya ili kuzingatia utawala bora.
Mhe. Naibu Waziri amemkumbusha Spika huyo kwamba
Bunge la Afrika Mashariki ni chombo kinachoziangalia taasisi za Jumuiya hivyo
lazima kiwe chombo cha mfano kwa Serikali za nchi wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki katika uendeshaji wa shughuli zake na kuzingatia weledi.
Akizungumzia kuhusu bajeti ya Jumuiya kwa mwaka wa fedha 2020/2021, Mhe. Naibu Waziri alimtakia heri katika kupitisha Bajeti hiyo kwenye Mkutano wa Bunge hilo utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Februari, 2021.
Naye Mhe. Spika Ngoga ameshukuru kwa maoni na msimamo wa Tanzania katika masuala mbalimbali ndani ya Jumuiya na kuelezea masikitiko yake baada ya Bunge kushindwa kupitisha Bajeti iliyowasilishwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya.
Ameahidi kuyafanyia kazi maoni ambayo ameyapokea kutoka kwa nchi wanachama ikiwamo Tanzania kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo na wananchi wake na kuongeza kuwa atatumia uzoefu wake kuhakikisha Bajeti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki inapitishwa na Bunge ili shughuli za Jumuiya ziendelee.
RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA AHITIMISHA ZAIRA YAKE YA SIKU MOJA NCHINI
Kwa Heri, Rais Zewde karibu tena wakati mwingine nchini Tanzania |
Mheshimiwa Sahle-Work Zewde Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Shirikisho la Ethiopia akipiga ngoma kwenye hafla ya mapokezi ya kumkaribisha alipowasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku moja |
Monday, January 25, 2021
MHE. SAHLE-WORK ZEWDE, RAIS WA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA SHIRIKISHO LA ETHIOPIA KUFANYA ZIARA NCHINI
Mkutano ukiendelea |
Friday, January 22, 2021
DKT. MWINYI: MAZINGIRA YA KISIASA ZANZIBAR YANATOA FURSA YA KUWALETEA WANANCHI MAENDELEO
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesema
Zanzibar iko salama na mazingira ya kisiasa yanatoa fursa ya kuwaletea wananchi
wa Zanzibar maendeleo kutokana na uwepo wa Serikali ya umoja wa kitaifa.
Rais
Mwinyi ameyasema hayo Ikulu ya Zanzibar wakati alipokutana na ufanya mazungumzo
na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi na kuongeza kuwa uongozi wake unajipanga kutimiza ahadi
alizotoa kwa wananchi.
Pia
Rais Mwinyi ameongeza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja
na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa kipaumbele katika kuimarisha Uchumi
wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia
kukuza uchumi na kupunguza mzigo wa kodi kwa wananchi.
“Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimetoa
kipaumbele katika kuimarisha Uchumi wa Bahari kuu hasa Uchumi wa bluu kama
chanzo mbadala cha mapato kitakachosaidia kukuza uchumi,” Amesema Dkt.
Mwinyi
Katika
tukio jingine, Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje umekutana na kufanya
mazungumzo na Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar,
Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad ambaye amesisitiza kuwa uchumi wa bluu ni muhimu
sana kwa maendeleo ya Zanzibar hivyo ni muhimu kwa Serikali zote mbili
(Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania) kulinda mipaka yake ya bahari ambapo pia ulinzi huo utasaidia kuzuia
na kupambana na uingizwaji wa dawa za kulevya hapa nchini.
“Naamini
kabisa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania tukishirikiana katika kuimarisha ulinzi wa baharini itasaidia
kupunguza uingizwaji wa dawa a kulevya hapa nchini,” Amesema Maalim Seif
Kwa
upande wake Prof. Palamagamba John Kabudi ameupongeza uongozi wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kwa kwa hatua ulizozichukua katika kuhakikisha uwepo wa
amani na utulivu visiwani humo na kwamba uwepo wa amani na utulivu utachangia
kuleta maendeleo haraka kwa wananchi wa Zanzibar.
“Zanzibar
imetulia na uchumi wake umezidi kuimarika sote ni mashahidi wa ongezeko la
watalii hapa Zanzibar hii ni ishara ya kuwa na amani na utulivu, na jambo hili
linachangia kukua kwa uchumi wa Zanzibar,” Amesema Prof. Kabudi
Mbali
na kukutana na Rais wa Zanzibar na Makamu wa Kwanza wa Rais, pia Uongozi huo
umekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdulla ambapo wamejadili masuala
mbalimbali ya maendeleo yanayohusu Tanzania Bara na Zanzibar hususan yanayohusu
Muungano.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi katika ziara yake ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea
na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
ukiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) Ikulu Zanzibar wakati wa ziara ya kikazi ya Prof.
Kabudi Zanzibar. Prof. Kabudi ameambatana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. William Olenasha pamoja na Katibu Mkuu wa
Wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi akiongea
na viongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, (hawapo pichani) katika Ikulu ya Zanzibar
Kikao
cha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali
Mwinyi na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki, kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar
Makamu
wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Maalim Seif Sharif
Hamad akimsikiliza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Prof. Palamagamba John Kabudi wakati alipokuwa akimuelezea jambo wakati uongozi
wa Wizara ulipomtembelea Mhe. Seif kwa zaiara ya kikazi mjini Zanzibar
Kikao
cha Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mhe. Maalim Seif
Sharif Hamad na uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki kikiendelea katika Ikulu ya Zanzibar
BALOZI IBUGE AKUTANA, KUFANYA MAZUNGUMZO NA MWANASHERIA MKUU WA ZANZIBAR
Na Nelson Kessy, Zanzibar
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akutana na kufanya mazungumzo na Mwanasheria Mkuu wa
Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Afisi za Mwanasheria Mkuu mjini Zanzibar
Mazungumzo
hayo yamelenga kuimarisha ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu ya kazi
baina Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar.
Balozi
Ibuge amesema kuwa jukumu kubwa la watendaji wa Serikali hizi mbili ni
kuhakikisha wanatekeleza maono (vision) viongozi wakuu wa Serikali hasa kwa
kuzingatia maelekezo yaliyopo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM). “Ni
jukumu letu sisi kama watendaji wa serikali kuwasaidia viongozi wetu kutekeleza
maoni ya viongozi wetu kwa kuzingatia Ilani ya CCM ya 2020 – 2025,” Amesema
Balozi Ibuge.
Kwa upande wake Dkt. Mwinyi Talib Haji amemuahidi Balozi Ibuge kuwa wataendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa malengo ya serikali zote mbili yanatekelezwa kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
“Nakuahidi kuwa sisi kama
Afisi ya Mwanasheria Mkuu – Zanzibar tutashirikina na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikino wa Afrika Mashariki katika kuhakikisha tunatekeleza majukumu ya
serikali,” Amesema Dkt. Haji.
Mwanansheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akimkaribisha Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar leo
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu
cha wageni katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu Zanzibar, kulia ni Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Dkt. Mwinyi Talib Haji
Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge akiongea na Mwanansheria
Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji katika Ofisi za Mwanasheria Mkuu
Zanzibar
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akimkabidhi moja ya zawadi Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge
Mwanasheria
Mkuu wa Zanzibar Dkt. Mwinyi Talib Haji akiwa katika picha ya pamoja na Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia
Jenerali Wilbert Ibuge. Wengine ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mambo ya Nje –
Zanzibar Bw. Masoud Balozi Masoud (kushoto) pamoja na Msaidizi wa Katibu Mkuu
Bw. Hangi Mgaka (kulia).