Tume ya pamoja ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Msumbiji
imekutana kujadili masuala ya ulinzi na usalama kati ya Mataifa
hayo.
Akiufungua Mkutano huo wa tatu wa Tume ya pamoja ya ulinzi na
usalama kati ya Tanzania na Msumbiji Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, amesema mkutano huo ni wa muhimu
kwakuwa unatoa fursa ya kuangalia namna ya kukabiliana na matukio yanayotishia
ulinzi na usalama yamejitokeza kusini mwa Tanzania na kaskazini mwa Msumbiji
ili kwa pamoja kupata suluhisho la kudumu.
“Mkutano
wa leo pia utatoa fursa ya kuangalia masuala ya Ulinzi na Usalama, masuala ya
mtambuka ambayo ni pamoja na umaskini na utawala bora katika nchi zetu mbili,
kikao hiki ni muhimu sana kwani kitarudisha imani kwa wananchi na kuonesha kuwa
hatujalala hadi hali itengamae kule Msumbiji,” Amesema Balozi Mulamula
Balozi Mulamula ameongeza kuwa,
anaamini kupitia majadiliano yaliyoanza kuanzia tarehe 3 Juni kwa ngazi ya
Wataalamu / Makatibu Wakuu hadi leo terehe 5 Juni mkutano wa ngazi ya Mawaziri utapitia
mapendekezo ya vikao vya awali kuweza kuchukua maamuzi katika maeneo masuala ya
ulinzi, usalama na usalama wa jamiii.
Ujumbe wa Msumbiji umeongozwa na Waziri wa Ulinzi wa Msumbiji Mhe
Jaime Augusto Neto na kuainisha masuala jumuishi kuhusu ulinzi na usalama na
kwamba ni Imani yake kuwa kikao hicho kitatoka na maazimio ya utekelezaji ili
kuwa na mtangamano imara.
Katika tukio jingine Umoja wa Ulaya umesema unaunga mkono hatua za
muendelezo na mabadiliko ya sera za kijamii na maendeleo yanayofanywa
Nchini,chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe Samia Suluhu Hassan na kwamba unapongeza hatua hizo.
Akizungumza kwa niaba ya mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya hapa Nchini
katika kikao kazi walichokiandaa Jijini Dar es Salaam,Balozi wa Umoja huo Mhe
Manfredo Fanti ameongeza kuwa matamko ya Rais Samia kuhusu ushirikiano kati ya
Tanzania na Jumuiya za Kimataifa,sekta binafsi,uhuru wa kujieleza,haki za
binadamu na utawala bora yanatia moyo.
“Matamko na maelekezo ya Mhe. Rais Samia kuhusu ushirikiano
kati ya Tanzania na Jumuiya za Kimataifa,sekta binafsi,uhuru wa kujieleza,haki
za binadamu na utawala bora yanatia moyo na kutuhamasisha kuwashawishi
wawekezaji na wafanyabiashara kuja kuwekeza Tanzania,” Amesema Balozi Fanti.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Liberata Mulamula amesema mkutano huo ulikuwa ni wa muhimu kwa kuwa unaweka
misingi ya kuaminiana na kuimarisha mahusiano kati ya Tanzania na Umoja huo ili
kuweka mazingira bora ya Mabalozi hao kuhamasisha wawekezaji na wafanyabiashara
kutoka katika Mataifa yao kuja kuwekeza hapa nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akipitia moja ya nyaraka kabla ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Tume ya
Pamoja ya Ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika Dar es
Salaam. Kulia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias
Kwandikwa
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiteta jambo na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias
Kwandikwa kabla ya kuanza kwa mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ulinzi na
Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji uliofanyika Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
akifungua mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ulinzi na Usalama kati ya
Tanzania na Msumbiji uliofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Elias Kwandikwa akiwasilisha mada
katika mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ulinzi na Usalama kati ya Tanzania
na Msumbiji uliofanyika Dar es Salaam
Waziri
wa Ulinzi wa Msumbiji, Mhe. Jaime Augusto Neto akiwasilisha mada katika mkutano
wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na Msumbiji
Wajumbe
wa mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Ulinzi na Usalama kati ya Tanzania na
Msumbiji wakifuatilia mkutano
Wajumbe
wakiwa katika picha ya pamoja
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiwa katika kikao kazi na mabalozi wa Umoja wa Ulaya wanaoziwakilisha
nchi zao hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam ambapo Umoja wa
Ulaya umeeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania
katika kuimarisha mahusiano na Jumuiya za Kimataifa.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
(Mb) akiwa katika kikao kazi na mabalozi wa Umoja wa Ulaya wanaoziwakilisha
nchi zao hapa nchini. Kikao hicho kimefanyika Dar es Salaam ambapo Umoja wa
Ulaya umeeleza kuridhishwa na hatua zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania
katika kuimarisha mahusiano na Jumuiya za Kimataifa.