Thursday, June 17, 2021

WAZIRI MULAMULA AFUNGUA MKUTANO WA MABALOZI WA EAC AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA EAC JIJINI ARUSHA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata  Mulamula akisaini kitabu cha wageni ofisini kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Dkt.Peter Mathuki muda mfupi baada ya kuwasili katika ofisi za makao makuu ya jumuiya hiyo jijiini Arusha leo.


Mhe. Waziri Mulamula  akiwa katika mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga  katika Makao Makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mh.Jaji Nestory Kayobera akimkabidhi Waziri Mulamula  machapisho mbalimbali yahusuyo Mahakama hiyo wakati Mhe. Waziri alipomtembela Rais huyo ofisini kwake makao makuu ya Mahakama hiyo iliyopo jijii Arsuha.

Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mh.Jaji Nestory Kayobera akimtembeza Mhe.Waziri Mulamula katika chumba cha Mahakama hiyo.

Mhe. Waziri Balozi Mulamulla akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha                                                                
  
  
Mhe. Waziri Balozi Mulamulla akifungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha leo

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (MB) ametembelea Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki yaliyopo Jijii Arusha. 

Mhe. Balozi Mulamula amefungua Mkutano wa Mashauriano wa Mabalozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa Taasisi za Jumuiya hiyo yenye makao yake Makuu jijini Arusha. 

Mhe. Mulamula kwanza amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt.Peter Mathuki na baadaye amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika Mashariki Mhe. Jaji Nestory Kayobera katika Makao Makuu ya jumuiya hiyo. 

Katika ziara hiyo Mhe. Waziri Mulamula pia amekutana na kufanya mazungumzo na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe.Martin Ngoga. Mikutano kati ya Mhe. Waziri na Mhe. Ngoga umefanyika katika Makao Makuu ya jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

NAIBU WAZIRI AFANYA MAZUNGUMZO NA WAANDAAJI MASHINDANO YA UREMBO AFRIKA MASHARIKI

 

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma

Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu na Huduma za Jamii Bw. Eliabi Chodota akizungumza wakati Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk wakati walipokutana na akizungumza na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwa Naibu Waziri jijini Dodoma

Makamu Rais wa Kamati ya Waandaaji wa Mashindano ya Urembo Afrika Mashariki bi Jolly Mutesi wa Rwanda (katikati) akizungumza akiwa na bi Mariam Ikoa kutoka Tanzania wakia na naibu Waziri Ofisini kwake jiini Dodoma.

mazungumzo yakiendelea

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika picha ya pamoja na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (walioko Kulia kwake) walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodom


Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk amekutana na kufanya mazungumzo na waandaaji wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki (Miss East Africa beauty Pegeant) ofisini kwake jijini Dodoma.

Waandaaji hao ni  bi Jolly Mutesi ambaye ni makamu wa Rais anayetokea nchini Rwanda na bi Mariam Ikoa ambaye ni muandaaji wa kimataifa anayetokea Tanzania.

Katika mazungumzo hayo  na waandaaji hao wa mashindano ya urembo kwa nchi za Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk amewapongeza waandaaji hao  kwa kuja na wazo  hilo pamoja na kutaka kufahamu miongozo na itifaki za kufuatilia ili kufanikisha mashindano hayo.

Akizungumza  katika kikao hicho Mratibu wa mashindanoo hayo Bi Mariam Ikoa amemuelezea Mhe. Naibu Waziri Mbarouk kwamba ujio wao Wizarani una lengo la kujitambulisha pamoja na kupata miongozo na itifaki za jinsi ya kuendelea na taratibu za mashindano hayo ya urembo kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema mashindano hayo yamepangwa  kufanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 26 Oktoba hadi Novemba 20 2021

SADC yaitaka EU Kuiondolea Vikwazo Zimbabwe

SADC yaitaka EU Kuiondolea Vikwazo Zimbabwe

Na Mwaandishi Maalum, Dodoma

Tanzania imeendelea kutoa wito wa kuiondolea vikwazo vya kiuchumi Zimbabwe, ambavyo vimetajwa kuwa vinadumaza jitihada za nchi hiyo za kujiletea maendeleo. Wito huo umetolewa wakati wa Mkutano wa majadiliano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya mtandao tarehe 16 Juni 2021.


“Hakuna sababu ya kuendelea kuiwekea vikwazo Zimbabwe ilihali imefanya mabadiliko ya kimfumo katika maeneo mengi yakiwemo ya siasa, uchumi na mifumo ya sheria”, walisikika wakisema Mawaziri wa SADC, baada ya ujumbe wa Tanzania ambao uliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) kuwasilisha hoja hiyo.

Ikijibu hoja hiyo, EU kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Ureno, Mhe. Augusto Santos Silva ilisisitiza umuhimu wa Zimbabwe kuendelea kufanya mabadiliko katika mifumo yake na kudai kuwa vikwazo vilivyosalia havina athari yoyote kwa watu wa Zimbabwe. Ilisema, licha ya vikwazo hivyo, EU imeendelea kushirikiana na Zimbabwe kwa kuipatia misaada ya maendeleo na ya kibinadamu ambapo Euro milioni 366 na milioni 66 mutawalia zimetolewa kwa Zimbabwe katika kipindi cha miaka saba iliyopita.

 

Katika majadiliano hayo yenye lengo la kusaidia kukuza uchumi na maendeleo katika kanda ya SADC, Waheshimiwa Mawaziri walijadili kuhusu janga la UVIKO-19 na athari zake katika ukuaji wa uchumi na mikakati ya kujikwamua kiuchumi baada ya ugonjwa huo kudhibitiwa. EU iliahidi kuendelea kushirikiana na nchi za SADC kupitia programu mbalimbali zikiwemo za kuhakikisha kuwa kila mtu anapata chanjo na programu nyingine za unafuu wa kulipa madeni na misaada ya fedha za kukabiliana na athari za UVIKO-19.

Kuhusu mikakati ya kukabiliana na UVIKO-19, Nchi za SADC kupitia Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji, Mhe. Verónica Macamo alizihimiza nchi za EU kuzijengea uwezo nchi za SADC wa kutengeneza vifaa vya kukabiliana na UVIKO-19 badala ya kuagiza vifaa hivyo kutoka nchi zilizoendelea.

Kwa upande wa agenda ya hali ya siasa, ulinzi na usalama katika kanda ya SADC, Waheshimiwa Mawaziri walieleza kuwa hali ni ya kuridhisha, isipokuwa kumekuwepo na matishio na mashambulizi ya kigaidi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji. EU iliahidi kuendelea kushirikiana na nchi hizo ili kukabiliana na changamoto za kiusalama katika Mashaiki ya DRC na jimbo la Cabo Delgado nchini Msumbiji.

Nchi za SADC, zilitoa shukrani kwa misaada ya kiusalama inayopokea kutoka EU na kuzisihi nchi hizo kuendelea kutoa misaada hiyo kwa kuwa suala la ulinzi na usalama ni ndiyo moyo wa progarumu za ushirikiano wao kuendelea. Kutokana na umuhimu wa usalama katika kanda, EU iliombwa kuunga mkono mchakato wa uanzishaji wa Kituo cha Kukabiliana na Ugaidi cha SADC (SADC Regional Counter Terrorism Centre-RCTC).

Suala lingine lililojadiliwa na Waheshimiwa Mawaziri ni biashara na uwekezaji ambapo EU imepongeza jitihada zinazoendelea za kuwa na Soko Huru la SADC-EAC-ECOWAS na la Bara la Afrika (AFCFTA). Ilielezwa kuwa masoko hayo itakuwa chachu katika uwekezaji, ujenzi wa miundombinu, kuongezeka kwa ajira na kumaliza umasikini barani Afrika.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiongea wakati wa Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N. Mbarouk akifuatilia majadiliano ya Mkutano wa  Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao.


Maafisa waandamizi kutoka taasisi za Serikali wakifuatilia majadiliano ya Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao. 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwa na Kaimu Mkurugenzi wa Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Mteule Agnes Kayola na Bw. Joseph Haule kutoka Wizara ya Fedha na Mipango kabla ya kuanza  Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Umoja wa Ulaya (EU) uliofanyika kwa njia ya Mtandao. 




 

Wednesday, June 16, 2021

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA KONGAMANO LA BIASHARA NA VIWANDA LA AFRIKA MASHARIKI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda, na Wakulima Tanzania (TCCIA) Bw. Paul Koyi pamoja na Mratibu wa Kanda wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye viwanda na Wakulima  Afrika Mashariki (EACCIA) Bw. Charles Kahuthu walipomtembelea ofisini kwake tarehe 16 Juni 2021 Jijini Dodoma.

Ujumbe huo unaosimamia masuala mbalimbali ya sekta binafsi ulikutana na Mhe. Balozi Mulamula kwa lengo la kuwasilisha serikalini kusudi la sekta hiyo kuipendekeza Tanzania kuwa mwenyeji wa Kongamano la Biashara na Viwanda linalotarajiwa kufanyika kuanzia tarehe 30 Agosti  hadi  3 Septemba 2021 katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Lengo la kongamano hili ni kuziunganisha sekta binafsi ili zipate uzoefu zaidi katika masuala ya viwanda na biashara. Pia kuviandaa vyama vya biashara, viwanda na kilimo vya kanda kuwa tayari kwa ushindani wakati huu ambapo mataifa ya Afrika yanajiweka tayari kuingia katika soko huru la biashara la Afrika (CFTA).

Aidha, Rais wa TCCIA Bw. Koyi alieleza kuwa  kongamano hilo litaambatana na maonesho ya bidhaa na huduma mbalimbali zinazotolewa na sekta binafsi hivyo, itakuwa ni fursa nzuri kwa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kongamano hilo ili kujifunza masuala ya biashara na uwekezaji.

Naye mratibu wa kanda wa EACCIA, Bw. Charles Kahuthu alifafanua malengo madhubuti ya chama hicho katika kuhakikisha kongamano hilo linakuwa tofauti na makongamano mengine yaliyokwishafanyika ni pamoja na kuhakikisha kinaongeza ushirikiano na kanda nyingine ndani ya Afrika ili kuweza kufungua fursa zaidi kwa wananchi wake.

“Sisi waratibu wa sekta binafsi tumepanga Kongamano hili liwakutanishe wafanyabiashara kutoka nchi za Afrika Mashariki, nchi za Maziwa makuu, na nchi nyingine ndani ya Afrika” alisema Bw. Kahuthu

Akiongea na ujumbe huu Mhe. Balozi Mulamula ameihakikishia sekta binafsi juu ya utayari wa serikali katika kuhakikisha inafanikisha jitihada hizi zenye lengo la kuinua uchumi na kwamba itakuwa bega kwa bega kutoa ushirikiano wakati wa maandalizi na wakati wa kongamano.

Vilevile, ametoa wito kwa TCCIA kuiandaa sekta binafsi kushiriki kikamilifu kuzinadi fursa mbalimbali katika kongamano hilo. Pia akaongeza kuwa kongamano litasaidia katika kupeana uzoefu wa kukuza mitaji na masoko ya biashara nje ya mipaka ya Tanzania sambamba na kuvutia uwekezaji.

Kadhalika, ametoa wito kwa wananchi kujiandaa kutumia fursa mbalimbali zitakazopatikana kupitia ugeni huo utakaowasili nchini.

Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Afrika Mashariki (EACCIA) chenye makao yake makuu nchini Kenya ni mdau muhimu katika kusimamia masuala ya sekta binafsi ndani ya jumuiya na pia kimekuwa kikiainisha vipaumbele mbalimbali vya sekta binafsi ndani ya jumuiya kwa kushirikiana na vyama vya kitaifa vinavyosimamia sekta hiyo.  

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Kulia) akizungumza na Rais wa Chama cha Wafanyabiashara,Wenye Viwanda na Wakulima Tanzania (TCCIA), Bw. Paul Koyi alipomtembelea ofisini kwake tarehe 16 Juni 2021 Jijini Dodoma.
Bw. Koyi alimueleza Mhe, Balozi Mulamula lengo la ujio wake pamoja na kumtambulisha Mratibu wa Kanda wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Afrika Mashariki(EACCIA) Bw. Charles Kahuthu(hayupo pichani)
Mhe. Balozi Mulamula akieleza nia ya dhati ya serikali katika kuhakikisha sekta binafsi inapewa ushirikiano ili kukuza na kuimarisha biashara ya kimataifa sambamba na uwekezaji. 
Wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Kanda wa Chama cha Wafanyabiashara, Wenye Viwanda na Wakulima Afrika Mashariki (CCIA) Bw. Charles Kahuthu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Bernard Haule (wa kwanza kulia) akifafanua programu mbalimbali za kitaifa na kikanda zilizofanyika katika kuhamasisha sekta binafsi na umma kwa ujumla juu ya fursa zinazopatikana katika soko la Afrika Mashariki na kuwaandaa wananchi kuingia katika ushindani wa soko huru la biashara la Afrika (CFTA).
Mazungumzo yakiendelea.

WANAFUNZI WA CHUO CHA DIPLOMASIA NA WAKUFUNZI WAO WATEMBELEA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI

Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi  wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega akizungumza kuwakaribisha Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao  waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza 

Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Stephen Mbundi akizungumza baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao  waliotembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa ajili ya kujifunza

Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki 


Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki


Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) waliotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki



Wakufunzi wa Chuo cha Diplomasia (CFR) wakisikiliza mawasilisho mbalimbali yaliyokuwa yakitolewa na watendaji wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, walipowaongoza Wanafunzi wa kozi ya stashahada ya uzamili kutembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za Wizara


Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) walotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma


Baadhi ya Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) walotembelea Wizarani kwa ajili ya kujifunza wakiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Wizara ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma



 



Wanafunzi wa kozi ya Astashahada ya uzamili kutoka Chuo cha Diplomasia (CFR) na wakufunzi wao wamefanya ziara ya mafunzo kwa kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki jijini Dodoma na kuzungumza na watendaji wa Wizara kwa ajili ya kujifunza namna Wizara watendaji wa Wizara wanavyotekeleza diplomasia ya uchumi kupitia kazi zao.

Wanafunzi hao kutoka kampasi ya Dar es Salaam na Dodoma walipata nafasi ya kusikiliza mada za muundo na majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001.

Akizungumza wakati wa kuwakaribisha wanachuo hao kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mkurugenzi wa Kitengo cha wa Diaspora Balozi Anisa Mbega aliwataka wanachuo hao kusikiliza kwa umakini mada zitakazotolewa na watendaji wa Wizara ambao wanafanya shughuli za kidiplomasia kwa vitendo ili kujiongezea ujuzi zaidi.

Balozi Anisa aliwaambia wanachuo hao kuwa Wizara inaona fahari kuwa na chuo hicho kwani kinawezesha upatikanaji wa elimu ya diplomasia kwa wananchi wengi na kuwataka wanachuo hao kuitumia elimu wanayoipata kwa manufaa yao na taifa kwa ujumla

Akizungumza kukamilisha mazungumzo kati ya wanachuo hao na watendaji wa Wizara Mkurugenzi wa Idara ya Siasa, Ulinzi na Usalama Balozi Stephen Mbundi aliwataka wanachuo hao kuwa tayari na kujiandaa na dunia ya sasa ili waende na wakati uliopo na aliwaahidi kuwa Wizara iko tayari muda wowote kuwasaidia ili waweze kuitendea haki elimu waliyoipata.

Wanachuo hao na wakufunzi wao walikuwa na ziara ya siku mbili jijini Dodoma ambapo siku ya kwanza walienda kutembelea Bunge kwa mwaliko wa Naibu Waziri –Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Nassor Mbarouk na kujionea jisni Bunge la Tanzania linavyoendesha shughuli zake.