Saturday, June 26, 2021

TANZANIA NA PAKISTAN ZA ADHIMISHA SIKU YA URAFIKI


Tanzania na Pakistan zimefanya madhimisho ya siku ya urafiki wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu baina ya Mataifa haya mawili rafiki, yaliyochazwa na hafla fupi iliyofanyika tarehe 25 Juni 2021 katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 

Madhimisho haya ambayo yamefanyika kwa mara ya kwanza, yalihudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali katika jamii kama vile, Wafanyabiashara, Wanadiplomasia, Watendaji na Viongozi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali, Watendaji wa Jumuiya za Kikanda, Wanasiasa na baadhi ya Viongozi Wastaafu wa Serikali. 

Pamoja na masuala mengine maadhimisho haya yanalenga kukuza zaidi mahusinao ya kibiashara baina ya Tanzania na Pakistan kwa kuwakutanisha wafanyabisha wa pande zote mbili ili waweze kubadilishana uzoefu na kujenga urafiki ambao utawazesha kwa pamoja kutumia na kuibua fursa za kibiashara zinazopatika katika nchi hizi mbili (Tanzania na Pakistan).

Akizungumza katika maadhimisho hayo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameeleza kuwa Tanzania itaendelea kuendeleza na kuboresha mahausiano mazuri yaliyodumu kwa muda mrefu na Pakistan. Ameongeza kusema kuwa Serikali ya Tanzania imejipanga kutumia muhusionao haya mazuri kuibua fursa za kibiashara ambazo zitanufaisha Serikali na raia wa pande zote mbili. “Takwimu za hivi karibuni zinaeleza, kuna zaidi ya kampuni 100 kutoka Pakistan ambazo zimewekeza nchini Tanzania. Ni lengo la Serikali ya awamu ya 6 kuhakikisha kunakuwepo na muafaka mzuri wa kisheria na kitaasisi na mazingira kwa wawekezaji hawa kufanya biashara nchini Tanzania bila bugudha.”

Akizungumza katika maadhimisho hayo Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem amepongeza Serikali ya Jumhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Uongozi Mahiri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendele kuchukua hatua za kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. “Tunaendelea kushuhudia juhudi na mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya usimamizi mahiri wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ya kuboresha mazingira ya biashara nchini, hakika jitihada hizi zinatoa matumaini na faraja kubwa kwa wawekezaji waliopo nchini na wale ambao wanania ya kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali nchini”. 

Mahusiano ya Kidiplomasia kati ya Pakistan na Tanzania yamedumu kwa tariban miaka 54 tokea yalipoanzishwa mwaka 1967 ambapo nchi ya Pakistani ilifungua Ofisi zake za Ubalozi hapa nchini Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiwasili katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam kushiriki maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akikabithiwa picha yenye maudhui ya utamaduni wa Pakistani na Mhe. Mohammad Saleem (kulia) Balozi wa Pakistani nchini, kwenye maadhimisho ya maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania.

Balozi wa Pakistan nchini Tanzania Mhe. Mohammad Saleem akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akihutubia hadhara iliyojitokeza kwenye maadhimisho ya Siku ya Urafiki wa Pakistani na Tanzania yaliyofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.
Hafla ya maadhimisho ikiendelea.

BALOZI MULAMULA AKUTANA NA WAWAKILISHI WA St. EGIDIO

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akionesha zawadi iliyotolewa na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiangalia zawadi iliyotolewa na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia walipomtembelea ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.

mazungumzo yakiendelea

Mmoja wa wawakilishi wa Jumuiya ya St. Egidio ya nchini Italia Bw. Andrea Bartoli akizungumza wakati wawakilishi hao walipomtembelea Balozi Mulamula ofisini kwake jijini Dodoma tarehe 25/06/2021






Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio ya nchini Italia.

Katika mazungumzo hayo wawakilishi wa Jumuiya hiyo wakiongozwa na Bw. Andrea Bartoli wamemuhakikishia Mhe. Waziri Mulamula kuwa Jumuiya yao itaendelea na kazi ya kuhakikisha amani inatamalaki katika nchi mbalimbali barani Afrika ikiwemo Tanzania.

Akizungumza nao Mhe. Waziri amewahakikishia wawakilishi hao kwamba Tanzania itaendelea kuwaunga mkono katika harakati zao za kuwa na jamii salama kwani kufanya hivyo kunasaidia dunia kuwa salama.

Amewaomba kuendelea na kazi ya kuifahamisha jamii juu ya kazi zinazofanywa na Jumuiya hiyo katika sehemu mbalimbali nchini na barani Afrika kwa ujumla.

Jumuiya hiyo inajihusisha na masuala ya utafutaji wa amani kwa njia ya midahalo na mazungumzo ikiwa ni pamoja na kutoa misaada ya kijamii katika jumuiya mbalimbali nchini na katika Bara la Afrika.


BALOZI MULAMULA AZINDUA BARAZA LA WAFANYAKAZI LA WIZARA

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (katikati) akiwa na viongozi wa Baraza la Wafanyakazi la Wizara wakiimba wimbo wa mshikamano daima alipowasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua Baraza jipya la Wafanyakazi wa wizara jijini Dodoma tarehe 25/06/2021

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiimba wimbo wa mshikamano daima baada ya mgeno rasmi kuwasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua rasmi Baraza hilo jijini Dodoma 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiimba wimbo wa mshikamano daima baada ya mgeni rasmi kuwasili ukumbini kwa ajili ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma 

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.
Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na Mhe. Waziri Mulamula

Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki katika picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuzindua Baraza hilo jijini Dodoma tarehe 25/06/2021.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) amezindua Baraza jipya la Wizara na kuwataka wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara kuwa mabalozi wazuri wa watumishi wa Wizara wanaowawakilisha.

Mhe. Waziri Mulamula ametoa rai hiyo jijini Dodoma alipokuwa akizindua Baraza hilo jijini Dodoma baada ya baraza la awali kumaliza muda wake.

Amesema kwamba uongozi wake kwa kushirikiana na watendaji wengine wa Wizara wako tayari kuyasikiliza na kuyafanyia kazi mapendekezo watakayoyapeleka kwa uongozi wa Wizara na kuwataka kuyafanyia kazi mapendekezo yanayotolewa na wafanyakazi ili yaweze kushughulikiwa.

Mhe. Waziri pia amewaambia wajumbe wa Baraza hio kwamba uongozi wake hautovumilia tabia au vitendo vya utovu wa nidhamu kama vile rushwa vitakavyolalamikiwa kufanywa na watumishi wa Wizara dhidi ya watu wanaowahudumia.

Amesema ni matarajio yake kwamba watumishi wa Wizara watakuwa waadilifu na wenye tabia njema wanapowahudumia wadau mbalimbali wa Wizara na hivyo kutekeleza majukumu yao kwa kufuata Sheria, Taratibu na Kanuni za Utumishi wa Umma na hivyo kutekeleza majukumu ya wizara ipasavyo.

Amesema kuwa Wizara imejipanga kuhakikisha inatoa vifaa na vitendea kazi kwa watumishi wake ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara unakamilika na kuwa na ufanisi.

Kikao hicho cha Baraza kiliwapitisha wajumbe wake katika mpango wa Bajeti wa mapato na matumizi ya wizara iliyopitishwa na Bunge mapema mwezi huu, kiliwachagua Bibi Judica Nagunwa kuwa Katibu na Bw. Hassan Mnondwa kuwa katibu Msaidizi wa Baraza hilo jipya ambalo litakaa madarakani kwa muda wa miaka mitatu.


Friday, June 25, 2021

MAWAZIRI WA EAC WAKUBALIANA KUSHIRIKIANA KATIKA SEKTA YA UCHUKUZI, MAWASILIANO NA HALI YA HEWA


Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaosimamia Sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa leo tarehe 25 Juni 2021 kwa pamoja wamekubaliana kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya sekta ya uchukuzi, mawasiliano na hali ya hewa. Makubaliano haya yamefikiwa katika Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa (TCM) la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Dar es Salaam.

Lengo la Mkutano huo wa 17 wa TCM pamoja na mambo mengine ilikuwa ni kupitia na kujadili utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki sambamba na kupitia na kujadili utekelezaji wa sera, mikakati, miradi na program mbalimbali katika sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa. 

Miongoni mwa maeneo ambayo Mawaziri hao wamekubaliana kushirikiana ni pamoja na mapendekezo ya Taasisi ya Afrika Mashariki kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano; utekelezaji wa miradi na programu katika sekta ndogo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa njia ya maji, hali ya hewa na mawasiliano.

Akizungumza baada ya Mkutano huo, Mwenyekiti Mhe. Wavinya Ndeti ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi na Miundombinu wa nchini Kenya amesema kuwa makubaliano muhimu yaliyofikiwa yatafungua zaidi fursa zinazotokana na sekta ya uchukuzi na usafirishaji kupitia anga, bararaba, reli na maji. Aliongezea kusema hatua hii itachangia kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi na kuboresha hali ya maisha ya watu katika Jumuiya. 

Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo Mhe. Mhandisi Dkt. Leonard Madaraka Chamulio (Mb) Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi ameeleza “tumekubaliana katika masuala yote tuliyojadiliana na hivyo tumeyapeleka katika Baraza la Mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, vilevile tumejadili na kupeleka mapendekezo kwa Baraza la Mawaziri wa Jumuiya kuhusu uunganishaji wa huduma katika anga la Afrika Mashariki”.

Kwa upande wa Tanzania ushirikiano huu katika sekta ya anga unatarajiwa kuongeza mapato ya nchi kwa kuwa huduma za uongozaji ndege zitatozwa kutokana na ukubwa, uzito na muda utakaotumiwa na ndege kupita katika Anga la Tanzania.

Mkutano huo wa Mawaziri ambao awali ulitanguliwa na mikutano ya Wataalam na Makatibu Wakuu iliyofanyika kwa nyakati tofauti kuanzia ya tarehe 21 hadi 24 Juni 2021 jijini Dar, licha ya kupitia utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya wamepokea na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu ikiwemo, mapendekezo kuhusu Taasisi ya Afrika Mashariki kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mhe. Mhandisi Dkt. Leonard Madaraka Chamulio akichangia jambo kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.

Afisa Uchumi Bi. Edna Chuku kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano uliokuwa ukiendelea.

Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Mipango, Miundombinu, Fedha na Utawala Mhandisi Steven Mlote akifafanua jambo kweye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam

Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Masharikia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kusaini taaraifa ya Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa uliofanyika katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam

Wajumbe wakifuatilia majadala uliokuwa ukiendelea katika Mkutano.
 

Mkutano ukiendelea


                                          Mkutano ukiendelea

MKUTANO WA 14 WA BARAZA LA KISEKTA LA MAWAZIRI WA KILIMO NA USALAMA WA CHAKULA WA EAC WAFANYIKA ARUSHA

Mkutano wa 14 Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefanyika leo tarehe 25 Juni 2021 jijini Arusha huku Mawaziri wakikubaliana kuendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali ya kilimo ili kujihakikishia usalama wa chakula kwa wananchi wote Afrika Mashariki.

 

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na mikutano ya Wataalam na Makatibu Wakuu iliyofanyika jijini hapa kuanzia tarehe 21 hadi 24 Juni 2021, ulilenga kupitia na kujadili utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya Baraza la Mawaziri wa Jumuiya pamoja na kupitia na kujadili masuala mbalimbali  muhimu ya kisera, kimkakati, miradi na program zinazotekelezwa katika sekta ya kilimo.

 

Aidha, Mawaziri hao wamepokea na kujadili agenda mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Makatibu Wakuu kama vile Taarifa ya Usalama wa Chakula ya Jumuiya ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Mradi wa Afrika wa Kilimo cha Ushindani cha Mpunga kwa Kanda ya Afrika Mashariki; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Mifugo; Taarifa kuhusu Mradi wa Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu; Taarifa kuhusu Maendeleo ya Uvuvi; na Taarifa kuhusu Uhamasishaji wa Uchangiaji Rasilimali.

 

Ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Mawaziri umeongozwa na Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda na kuhudhuriwa pia na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki, Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Soud Nahodha Hassan, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Bw. Andrew Massawe, Katibu Mkuu  wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Rashid Tamatama pamoja na Maafisa Waandamizi kutoka Sekta mbalimbali zinazojishughulisha na masuala ya kilimo na usalama wa chakula hapa nchini. 

Kiongozi wa ujumbe wa Tanzania ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Mhe. Prof. Adolf Mkenda akizungumza  wakati wa Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021
Mhe. Prof. Mkenda akisaini Ripoti ya Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021


Mhe. Prof. Mkenda (kushoto) akiwa na Mawaziri wengine wa Tanzania walioshiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021. Kulia ni Waziri wa Kilimo, Umwagiliaji, Maliasili na Mifugo Zanzibar, Mhe. Soud Nahodha Hassan na katikati ni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Mashimba Ndaki.

Mwenyekiti wa Mkutano wa Mawaziri ambaye ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Ushirika wa Kenya, Mhe. Lawrence Angolo akizungumza wakati wa Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Ujumbe wa Burundi ukishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Sehemu ya ujumbe wa Kenya ukiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Kenya katika Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Udhibiti wa Mbegu Tanzania, Bw. Patrick Ngwediadi akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 

Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Benjamin Mwesiga akishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021 pamoja na Bibi Jackline Mpuya kutoka Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa

Sehemu ya washiriki wakifuatilia Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Sehemu ya ujumbe wa Tanzania wakishiriki Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Mtendaji Mkuu wa Mpango wa Kuboresha Kilimo Ukanda wa Nyanda za Juu Kusini (SAGCOT), Bw. Geoffrey Kirenga (kulia) akiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Mkutano ukiendelea

Maafisa Waandamizi wakiwa kwenye Mkutano wa 14 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Kilimo na Usalama wa Chakula wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha tarehe 25 Juni 2021

Picha ya pamoja



 

Thursday, June 24, 2021

MAKATIBU WAKUU WA EAC WANAOSIMAMIA SEKTA YA UCHUKUZI, MAWASILIANO, NA HALI YA HEWA WAKUTANA DAR ES SALAAM.


Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa (TCM) la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Makatibu Wakuu umefanyika leo tarehe 24 Juni, 2021 jijini Dar es Salaam. Makatibu Wakuu hao wamekutana, sambamba na masuala mengine kukamilisha maandalizi ya mwisho kuelekea Mkutano wa Mawaziri unaotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 25 Juni, 2021. 

Katika Mkutano huo Mkatibu Wakuu, wamepokea, kupitia na kujadili taarifa ya utekelezaji wa programu, mikakati, miradi, maelekezo na maauzi yaliyotolewa katika Mikutano ya awali ya Sekta hiyo. Vilevile, Makatibu Wakuu hao wamepitia na kujadili agenda zitakazo jadiliwa na Mawaziri katika mkutano wao unaotarajiwa kufanyika hapo kesho. Agenda hizo ni pamo na; kujadili kuhusu mapendekezo ya Taasisi ya Afrika Mashariki juu kuratibu programu za maendeleo katika Sekta ya Mawasiliano; kuangalia hatua ya maendeleo iliyofikiwa ya utekelezaji wa miradi na programu katika sekta ndogo ya barabara, reli, usafiri wa anga, usafiri wa majini, hali ya hewa na mawasiliano. 

Akizungumza wakati akifungua mkutano huo, Mwenyekiti ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma kutoka Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki ya nchini Kenya Bw. Charles Ngunjiri amesema Jumuiya ya Afrika imepiga hatua kubwa katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo imechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa biashara na kurahisha upatikanaji wa huduma mbalimbali katika ya Jumuiya. Aliongeza kutoa rai kwa wajumbe wa mkutano kutumia vyema mkutano huo kutoa michango ya kujenga zaidi itakayo endelea kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili Jumuiya katika sekta ya Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa. 

Katika Mkutano huu wa ngazi ya Makatibu Wakuu, kwa upande wa Tanzania umehudhuriwa na Ndg. Mussa Haji Ali, Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais – Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar na Ndg. Amour Hamil Bakari, Katibu Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Zanzibar.

Mkutano ukiendelea

Kaimu Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii, Bw. Eliabi Chodota akifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Meza kuu ikiongoza majadilino kwenye Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Ujumbe wa Tanzania wakifuatilia Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Uchukuzi, Mawasiliano, na Hali ya Hewa ngazi ya Makatibu Wakuu uliokuwa ukiendelea katika Hoteli ya Four Points jijini Dar es Salaam