Saturday, October 2, 2021

WAZIRI MULAMULA ASHIRIKI MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA NIGERIA


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameshiriki sherehe ya Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Taifa hilo iliyoandaliwa na Ubalozi wa Nigeria hapa nchini. 

Sherehe za Maadhimisho hayo ambazo zimefanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam zimehudhuriwa na wawakilishi kutoka makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo, Wafanyabiashara, Wanadiplomasia, Watendaji na Viongozi kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. 

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo Waziri Mulamula licha ya kuipongeza Serikali ya Shirikisho la Nigeria kwa kuendelea kulinda Uhuru wake na kudumisha amani na usalama pia, amepongeza hatua ya maendeleo ya kiuchumi iliyofikiwa na Taifa hilo chini ya uongozi mahiri wa Rais Mhe. Muhammadu Buhari. Aliongeza kusema kwa kutambua hilo Tanzania itaendelea kudumisha na kukuza mahusiano ya kidiplomasia na kibiashara na Nigeria ili kwa pamoja kuweza kunufaika kiuchumi kutokana na fursa zilizopo. 

Kwa upande wake Balozi wa Nigeria hapa nchini Mhe. Hamisu Takalmawa amesema Serikali ya Shirikisho la Nigeria itaendelea kutumia matunda ya Uhuru wake kwa kuchukua hatua stahiki za kuboresha na kukuza mahusiano mazuri ya Kidiplomasia yaliyopo baina yake na Mataifa mengine ulimwenguni. 

Nigeria ilipata Uhuru wake Oktoba 1, 1960
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akifurahia jambo kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Nigeria zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Nigeria zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Hamisu Takalmawa akihutubia kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Nigeria zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Hamisu Takalmawa (kulia) na Balozi wa Comoro hapa nchini Mhe. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih (kushoto) wakikata keki kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Nigeria
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akihutubia katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Nigeria zilizofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja Wanadiplomasia walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Nigeria
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Nigeria nchini Tanzania Mhe. Hamisu Takalmawa (kulia) na Balozi wa Comoro hapa nchini Mhe. Ahamada El Badaoui Mohamed Fakih (kushoto) wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea kwenye sherehe za Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Nigeria

Friday, October 1, 2021

WAZIRI MULAMULA AWAAGA MABALOZI WALIOMALIZA MUDA WA UWAKILISHI NCHINI


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) kwa nyakati tofauti amewaaga Balozi wa Indonesia Mhe. Prof. Ratlan Pardede na wa Ethiopia Mhe.Yonas Yosef Sanbe ambao wamemaliza muda wao wa uwakilishi hapa nchini.

Waziri Mulamula akiongea katika hafla ya kuwaaga Mabalozi hao iliyofanyika kwa nyakati tofauti katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, amewapongeza kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kudumisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na nchi wanazoziwakilisha (Indonesia na Ethiopia).

Akizungumza na Balozi wa Indonesia Waziri Mulamula amemuahidi Mhe.Balozi Prof. Pardede kuwa licha ya mahusiano mazuri ya Kidiplomasia yaliyopo, Tanzania itaendelea kushirikiana na Indonesia katika sekta za elimu, kilimo na tehama kwa maslahi ya Nchi zote mbili. 

“Kwa niaba ya Serikali, naishuru Indonesia kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania za kuendeleza kilimo kwa kutoa fursa za masomo kwa vijana wetu, kusomea musuala mbalimbali katika Kilimo na Teknolojia, jambo ambalo litachangia kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya Kilimo hapa nchini” Waziri Mulamula. 

Kwa upande wake Balozi wa Indonesia Mhe. Prof. Pardede licha ya kuishukuru Serikali ya Tanzania kwa kumpa ushirikiano wa kutosha wakati akitekeleza majukumu yake katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini. Vilevile ameelezea kufurahishwa kwake na mahusiano mzuri yaliyopo baina ya Indonesia na Tanzania.

Wakati huohuo Balozi wa Ethiopia hapa nchini Mhe. Sanbe amepongeza hatua mbalimbali ambazo Serikali ya Tanzania imeendelea kuzichukua katika kutekeleza diplomasia ya uchumi sambamba na kutoa msukumo wa matumizi ya lugha ya Kiswahili barani Afrika. Aidha ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuendelea kudumisha na kukuza mahusiano ya Kidiplomasia na Ethiopia.

Tanzania na Ethiopia zimeendelea kuwa na uhusiano na ushirikiano mzuri wa muda mrefu. Nchi hizi mbili zimeendelea kushirikiana katika maeneo mbalimbali ikiwemo kukuza lugha ya Kishwahili, utalii, ulinzi na usalama, na usafiri wa anga.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Prof. Ratlan Pardede yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (Mb) akimsikiliza Balozi wa Indonesia Mhe. Prof. Ratlan Pardede ambaye anamaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini. Wa kwanza kulia ni Balozi Caesar Waitara Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia akifuatilia mazungumzo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Indonesia hapa nchini Mhe. Prof. Ratlan Pardede yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Mazungumzo yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akielezea jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Ethiopia anayemaliza kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini Mhe.Yonas Yosef yaliyofanyika jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Ethiopia anayemaliza kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini Mhe. Yonas Yosef wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza Balozi wa Ethiopia anayemaliza kipindi cha uwakilishi wake hapa nchini Mhe.Yonas. Wa kwanza kulia ni Balozi Naimi Azizi Mkurugenzi wa Idara ya Afrika akifuatilia mazungumzo
Mazungumzo yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Balozi wa Indonesia Mhe. Prof. Ratlan Pardede wakiwa katika mazungumzo. 

Thursday, September 30, 2021

UFAFANUZI KUHUSU MAGARI YA MIZIGO YA TANZANIA YALIYOKWAMA NCHINI MALAWI


 

TANGAZO LA NAFASI YA KAZI KATIKA KAMISHENI YA UMOJA WA AFRIKA


 

WAZIRI MULAMULA AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA MAKAMPUNI YA THE PULA GROUP JIJINI DAR

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Makampuni ya The Pula Group Dkt. Mary Stith katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Kampuni ya The Pula Group ni Kampuni ya Kimarekani inayojishughulisha na uchimbaji wa madini ya risasi (graphite) hapa nchini ambayo ni moja ya malighafi muhimu katika uzalishaji wa betri. Pamoja na mambo mengine mazungumzo hayo yalijikita katika kujadili masuala mbalimbali muhimu katika kutangaza fursa kwa lengo la kuvutia wawekezaji wengi zaidi katika sekta hiyo. 

Akizungumza baada ya mkutano huo Dkt. Mary ameeleza sambamba na kumshirikisha Waziri Mulamula kuhusu mchango na nafasi ya Kampuni yake katika kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini hasa kwenye sekta ya madini pia ametumia fursa hiyo kujifunza na kupata uzoefu wa masuala mengi kuhusu Wanawake na Uongozi kutoka kwa Waziri Mulamula.

“Wakati huu ambao Dunia inakabiliana na adhari za madiliko ya Tabianchi, mahitaji ya madini ya ghraphite ambayo ni muhimu katika uzalishaji wa nishati ya umeme yameendelea kuongezeka Duniani kwa sababu ni rafiki kwa mazingira, nafarijika kuona Tanzania ikiwa na kiasi kikubwa cha hifadhi ya madini haya yenye viwango vya kimataifa” Amesema Dkt. Mary. 

Aidha Waziri Mulamula kwa upande wake amemwakikishia Dkt. Mary kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi madhubuti wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan itaendelea kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji nchini sambamba na kudumisha ulinzi na usalama. 

Kampuni ya The Pula Group ilianza kuendesha shughuli za utafutaji na uchimbaji wa madini ya graphite nchini mwaka 2014. 


Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula amekutana na kufanyamazungumzo na Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. Prof. Adelardus Kilangi aliteuliwa kuwa Balozi Septemba 12, 2021.


Katika tukio jingine Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula ameshiriki Sherehe ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam. Maadhimisho hayo yaliongozwa na kauli mbiu “Miaka Sitini ya Huduma na Urafiki”. 

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Waziri Mulamula ameeleza kuwa Tanzania ina thamini sana jitihada na mchango wa Marekani katika maendeleo ya Kijamii na Kiuchumi kwenye maeneo mabalimbali hapa nchini ikiwemo; afya, elimu, miundombinu, maji, teknolojia ya habari na mawasiliano, kuimarisha demokrasia, haki za binadamu, utawala wa sheria na utawala bora.

Waziri Mulamula aliongeza kusema wakati huu ambao nchi hizi mbili zinasherekea Maadhimisho ya Miaka Sitini ya Huduma na Urafiki, ni fursa nyingine ya kutafakari mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano wetu ambayo ni chachu katika kudumisha na kuimarisha ushirikiano wa karibu zaidi baina ya Nchi hizi mbili rafiki. Aidha, Waziri Mulamula amewashukuru Raia wa Marekani ambao kwa muda mrefu wamejitolea kufanya kazi bila kuchoka katika maeneo mbalimbali ya vijijini nchini wakishirikiana na Washirika wa ndani ikiwemo kufundisha hesabu na sayansi katika shule za upili, wakufunzi wa walimu katika teknolojia ya habari na mawasiliano na sekta ya afya.

“Nitumie fursa hii kusisitiza kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Marekani na itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na Peace Corps Tanzania katika kuleta maendeleo endelevu kwa Nchi yetu”. Alisema Waziri Mulamula.

Peace Corps Tanzania ni Taasisi ya Kimarekani inayochangia nguvu kazi katika shughuli 

mbalimbali za maendeleo ya Kijamii na Uchumi kwa kujitolea. Kazi na majukumu ya Peace Corps Tanzaniayanaongozwa na Mkataba uliosainiwa kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Marekani Januari 9, 1979.

Maadhimisho hayo pamoja na washiriki wengine yalihudhuriwa na Mhe. Dr. Donald Wright Balozi wa Marekani nchini Tanzania na Bi. Stephanie Joseph de Goes Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzaniayaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright alipowasili kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na Balozi Mteule Prof. Adelardus Kilangi wakiwa katika mazungumzo
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (katikati), Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright (kulia) na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes (kushoto) wakiwa wamesimama wakati Wimbo wa Taifa la Tanzania na Marekani unaimbwa. 
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkaazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzania yaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula, Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Dr. Donald Wright na Mkurugenzi Mkazi wa Peace Corps Tanzania Bi. Stephanie Joseph de Goes wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Ubalozi wa Marekani na Peace Corps Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula na Rais wa Makampuni ya The Pula Group Dkt. Mary Stith wakiwa katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Rais wa Makampuni ya The Pula Group”Dkt. Mary Stith yaliyofanyika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Muzungumzo yakiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Balozi Liberata Mulamula (Mb) akizungumza kwenye sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Peace Corps Tanzaniayaliyofanyika kwenye viunga vya Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.