Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye leo amehitimisha ziara yake ya
kikazi ya siku tatu nchini na kurejea nchini Burundi.
Rais
Ndayishimiye kabla ya kuondoka nchini, alitembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
na kupata fursa ya kupata taarifa za utendaji wa Bandari.
Akiwa
katika Mamlaka ya Bandari, Mhe. Ndayishimiye ameipongeza Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) kwa kazi nzuri mnayoifanya na inayorahisisha biashara kati ya
Tanzania na Burundi.
“Nashukuru
sana pia kwa maamuzi mazuri mliyofanya ya kuweka Ofisi zenu Bujumbura-Burundi
ili wafanyabiashara waweze kusafirisha bidhaa zao,” Amesema Rais Ndayishimiye.
Ameongeza
kuwa amefurahi sana kuona Serikali ya Tanzania inaendelea kurahisisha biashara kati
yake na Burundi……“sisi hatuna bahari, lakini mnarahisisha usafiri wetu,”
Ameongeza Rais Ndayishimiye.
Nimetembea
Kwara nimeona ujenzi wa reli umeanza, itafika Burundi kutoka Uvinza hadi
Kitega, Mji Mkuu wa siasa. Kwa kweli namshukuru sana Rais Samia Suluhu pamoja
na watanzania wote kwa mapokezi mazuri.
Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akisalia wananchi mara baada
ya kuwasili katika viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) leo jijini Dar es Salaam. Mhe. Ndayishimiye
ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Balozi Liberata Mulamula
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)
Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akitoa salamu za Wizara
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimia wananchi
Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akiongea na wananchi katika
viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) leo jijini Dar es Salaam |
Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akipokea zawadi ya picha ya
muonekano wa zamani wa Bandari kutoka kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.
Makame Mbarawa jijini Dar es Salaam |
Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye pamoja na Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakiangalia picha muonekano mpya wa Bandari |
Rais
wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akipokea zawadi ya picha
kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Liberata Mulamula |
Wananchi
wakifuatilia hotuba ya Mhe. Ndayishimye katika viwanja vya Mamlaka
ya Bandari Tanzania |