Sunday, October 24, 2021

RAIS NDAYISHIMIYE AHITIMISHA ZIARA YAKE NCHINI, KUREJEA BURUNDI

Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye leo amehitimisha ziara yake ya kikazi ya siku tatu nchini na kurejea nchini Burundi.

Rais Ndayishimiye kabla ya kuondoka nchini, alitembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na kupata fursa ya kupata taarifa za utendaji wa Bandari.

Akiwa katika Mamlaka ya Bandari, Mhe. Ndayishimiye ameipongeza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kwa kazi nzuri mnayoifanya na inayorahisisha biashara kati ya Tanzania na Burundi.

“Nashukuru sana pia kwa maamuzi mazuri mliyofanya ya kuweka Ofisi zenu Bujumbura-Burundi ili wafanyabiashara waweze kusafirisha bidhaa zao,” Amesema Rais Ndayishimiye.

Ameongeza kuwa amefurahi sana kuona Serikali ya Tanzania inaendelea kurahisisha biashara kati yake na Burundi……“sisi hatuna bahari, lakini mnarahisisha usafiri wetu,” Ameongeza Rais Ndayishimiye.

Nimetembea Kwara nimeona ujenzi wa reli umeanza, itafika Burundi kutoka Uvinza hadi Kitega, Mji Mkuu wa siasa. Kwa kweli namshukuru sana Rais Samia Suluhu pamoja na watanzania wote kwa mapokezi mazuri.



Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akisalia wananchi mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  leo jijini Dar es Salaam. Mhe. Ndayishimiye ameambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula 




 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)

Bw. Eric Hamissi akitoa taarifa fupi juu ya utendaji wa Bandari kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa akitoa salamu za Wizara   


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akisalimia wananchi 


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akiongea na wananchi katika viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA)  leo jijini Dar es Salaam   


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akipokea zawadi ya picha ya muonekano wa zamani wa Bandari kutoka kwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa jijini Dar es Salaam   


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye pamoja na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa wakiangalia picha muonekano mpya wa  Bandari     


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akipokea zawadi ya picha kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula  


Wananchi wakifuatilia hotuba ya Mhe. Ndayishimye katika viwanja vya Mamlaka ya Bandari Tanzania


Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye akiagana na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kurejea Burundi 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuaga Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam  





No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.