|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akipokea Nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akionesha Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akiangalia Nakala ya Hati za Utambulisho alizopokea kutoka kwa Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini
|
|
Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini |
|
Mazungumzo yakiendelea
|
|
Mazungumzo yakiendelea
|
|
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakiongozwa na Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa (wa kwanza kushoto) ulioambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula hayupo pichani ukifuatilia mazungumzo kati wa Balozi Mulamula na Balozi Mteule wa Ethiopia nchini alipofika katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kuwasilisha nakala ya Hati za Utambulisho |
|
Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kukabidhi nkala ya Hti za Utambulisho baada ya kuwasili nchini |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (wa pili kulia) akiwa na Balozi
Mteule wa Ethiopia nchini Mhe. Sibru Mamo Kedida (wa pili kushoto) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi Nakala ya Hati za Utambulisho alipofika katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kujitambulisha baada ya kuwasili nchini. wa kwanza kulia ni Mkuu wa Itifaki nchini Balozi Yusuph Mndolwa na wa kwanza kushoto ni ofisa Ubalozi wa Ethiopiaa nchini Bw. Mulato.
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula
(Mb) amepokea nakala ya Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa
Ethiopia nchini Mhe. Shibru Mamo Kedida leo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini
Dar es Salaam.
Baada
ya kupokea nakala ya hati hizo viongozi hao walipata fursa ya kuzungumza ambapo
Balozi Mulamula alimhakikishia Balozi Mteule ushirikiano wa hali ya juu
kumuwezesha Balozi huyo kutekeleza majukumu yake ya kibalozi hapa nchini na
kuhakikisha uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia unaendelea kuimarika.
‘‘Unaona
timu yangu niliyoambatana nayo hapa, nichukue nafasi hii kukuhakikishia kuwa
Wizara itakupa ushirikiano wote utakaouhitaji katika kutekeleza majukumu yako,
saa 24 milango yetu iko wazi, tunataka uhusiano kati ya nchi zetu uzidi
kuimarika,’’ alisema Balozi Mulamula.
Balozi
Mulamula amesema Tanzania imefarijika kupata balozi mpya baada ya Balozi wa
awali kumaliza muda wake wa uwakilishi, na kuongeza kuwa kitendo hicho ni
ishara ya uhusiano mzuri na urafiki uliopo baina ya Tanzania na Ethiopia.
Naye
Balozi Mteule wa Ethiopia Mhe. Sibru Mamo Kedida amemshukuru Waziri
Mulamula kwa jinsi alivyompokea na kuelezea
uhusiano kati ya Tanzania na Ethiopia ulivo mzuri na kuahidi kuwa atahakikisha
uhusiano huo unazidi kukua na kuimarika.
“Ethiopia
na Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri sana
kidiplomasia, nchi zzetu zimekuwa na lengo moja, nitahakikisha uhusiano kati
ya nchi hizi unaimarika na hata kufikia nchi hizi Tanzania na Ethiopia
zinashirikiana kufanya biashara na uwekezaji kwa maslahi ya pande mbili,” amesema
Mhe. Balozi Kedida