Na Mwandishi wetu, Dar
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango ameuhakikishia Umoja wa Mataifa (UN) kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Umoja huo katika miradi mbalimbali ya maendeleo.
Dkt. Mpango aliyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo (UNSDCF) wa Miaka Mitano (2022-2027) wa ushirikiano baina ya Tanzania na Umoja wa Mataifa nchini Jijini Dar es Salaam.
Dkt. Mpango ameongeza kuwa Serikali itaendelea kufanya kazi kwa pamoja Mashirika ya Kimataifa ili kuleta mafanikio ya nchi ya Tanzania.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (Mb) aliishukuru UN kwa kazi nzuri ambayo wameifanya ya kusuma maendeleo ya nchi ya Tanzania.
Balozi Mulamula aliongeza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kufanya kazi pamoja na UN kwa lengo la kuhakikisha inajenga mazingira mazuri ili kuweza kufanikiwa kimaendeleo.
Naye Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said alisema mpango huo umejumuisha maendeleo ya watu wa Zanzibar ili kuleta maendeleo.
Awali Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic alisema mfumo wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania umebaini maeneo manne ya kimkakati kwa maendeleo endelevu 2030.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akizindua Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam |
Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Zena Said akiwasilisha hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam |
Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Zlatan Milisic akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam |
Balozi wa Canada nchini Tanzania, Mhe. Pamela O'Donnell akizungumza na washiriki wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2022-2027) Jijini Dar es Salaam |