Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Lusaka, Zambia ukiendelea. |
Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika uliofanyika jijini Lusaka, Zambia ukiendelea. |
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ufaransa zimeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja za elimu, afya, maji, usafirishaji, kilimo na utalii kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.
Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliposhiriki hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai 2022.
Balozi Mbarouk alisema Tanzania na Ufaransa zimekuwa na uhusiano mzuri tangu mwaka 1961 na mataifa hayo yamekuwa na ushirikiano katika nyanja za elimu, afya, maji, usafirishaji, mawasiliano, utalii, kilimo, biashara na uwekezaji.
“Ufaransa imekuwa mdau mkubwa katika masuala ya uchumi ambapo kampuni mbalimbali kutoka Ufaransa zimewekeza nchini na zimekuwa zikichangia kutoa ajira kwa watanzania na kuongeza pato la taifa,” alisema Balozi Mbarouk
Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Ufaransa imekuwa mdau mkubwa wa utalii ambapo idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka kutoka 25,000 kwa mwaka 2020 hadi 50,000 kwa mwaka 2022.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza nchini…….pia Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyabishara wa Ufaransa katika kukuza sekta uchumi,” alisema Balozi Mbarouk.
Awali Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui alisema Ufaransa imefurahishwa na ushirikiano mzuri inaoupata kutoka Serikali ya Tanzania na kuahidi kuwa Ufaransa itaendelea kudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya mataifa yote mawili.
Balozi Hajlaoui aliongeza kuwa Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania kuunga mkono juhudi mbalimbali za kukuza maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania.
“Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Ufaransa kwa muda mrefu nawaahidi hapa kuwa uhusiano huu tutaendelea kuudumisha na kuulinda wakati wote,” alisema Balozi Hajlaoui
Balozi Hajlaoui aliongeza kuwa Ufaransa inaridhishwa na jitihada za Tanzania katika kuhakikisha usawa wa kijinsia katika jamii, uhuru wa demokrasia, kulinda amani na usalama ndani na kwenye kanda.
Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui akiwasilisha hotuba yake katika hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai 2022 |
Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) ukiendelea jijini Lusaka, Zambia. |
Mkutano wa 41 wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Afrika (AU) ukiendelea jijini Lusaka, Zambia. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk ameipongeza Taasisi ya Maendeleo ya Aga Khan (AKDN) kwa mchango wake mkubwa katika kukuza na kuendeleza sekta za elimu, afya, miundombinu, utalii na utamaduni hapa nchini. Balozi Mbarouk ameyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 65 ya Uimamu wa Kiongozi wa Kiroho wa Madhehebu ya Shia Ismailia duniani, Mhe. Karim Aga Khan. Balozi Mbarouk ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi hiyo, amesema Taasisi hiyo ambayo kupitia miradi mbalimbali iliyopo Tanzania Bara na Zanzibar ikiwemo ya elimu na afya na ile ya kujikwamua kiuchumi imewasaidia watu wengi ambapo hadi sasa takriban watoto 10,000 nusu ya hao wakiwa wasichana wamefaidika kwa kupata elimu bora kupitia taasisi hiyo "Kupitia uongozi mzuri wa Mheshimiwa Aga Khan, Taasisi ya AKDN imekuwa mstari wa mbele kuchangia katika sekta za elimu, afya, maendeleo ya uchumi na kuondoa umaskini kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Hivyo ninayo furaha kuungana na jamii ya Ismailia ya hapa nchini na duniani kwa ujumla kusherehekea siku hii muhimu ya miaka 65 ya Mhe. Aga Khan kuwa Imam wa Madhehebu ya Shia Imailia” alisema Balozi Mbarouk. Kadhalika, Mhe. Balozi Mbarouk alisema anapongeza jitihada zinazoendelea kufanywa na AKDN katika kuboresha huduma za afya nchini ambapo kupitia jitihada hizo, mwezi Aprili 2022, Mkuu wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii ya AKDN, Mhe. Zahra Aga Khan, Mkuu wa Kamati ya Jamii ya AKDN alitembelea Tanzania na kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Huduma za Saratani jijini Dar es Salaam cha kiwango cha kimataifa ambacho kitakuwa na uwezo wa kutoa huduma mbalimbali kuhusu ugonjwa wa saratani ikiwemo kinga, utambuzi wa mapema wa ugonjwa, matibabu na huduma za nyumbani kwa wagonjwa Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya AKDN hapa nchini, Mhe. Balozi Amin Kurji amesema Taasisi yake itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia sekta mbalimbali zikiwemo za afya na elimu. Amesema, kupitia taasisi hiyo tayari miradi mbalimbali ikiwemo ya Vyuo Vikuu, Vyuo vya Afya vya wauguzi na wakunga vimeanzishwa nchini. Aidha, ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Uongozi wa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa maendeleo makubwa ya uchumi na jamii yaliyopatikana nchini katika kipindi kifupi tangu aingie madarakani na kwamba Taasisi ya AKDN itaendelea kushirikiana na Serikali ili kuunga mkono jitihada hizo. “Nampongeza Mhe. Rais Samia na Serikali yake kwa ujumla. Tumeshuhudia uwekezaji mkubwa unaofanywa na Serikali katika kuboresha sekta za afya, elimu maji, umeme, miundombinu na sekta za uzalishaji. AKDN inaahidi kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuboresha maisha ya Watanzania” alisisitiza Balozi Kurji. Maadhimisho hayo ambayo yalifanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam yalihudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye, Mabalozi, Wabunge na Wageni wengine waalikwa. |
Mhe. Balozi Mbarouk akihutubia wageni waalkiwa wakati wa maadhimisho ya miaka 65 ya Imam Aga Khan |
Mwakilishi Mkazi wa Taasisi ya AKDN nchini, Mhe. Balozi Amin Kurji naye akizungumza wakati wa maadhimisho hayo |
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye akifuatilia maadhimisho ya miaka 65 ya Imam Aga Khan |
Wageni waalikwa wakifuatilia maadhimisho ya miaka 65 ya Uimamu wa Aga Khan |
Mhe. Naibu Waziri akipata maelezo kuhusu kazi mbalimbali za uchapishaji vitabu unaofanywa na Taasisi ya AKDN |
Mhe. Balozi Mbarouk akiwa katika picha ya pamoja |
Balozi wa Tanzania nchini Austria, Mhe. Celestine Mushy na Meya wa Jiji la Linz, Mhe. Mstahiki Klaus Luger wakiwa katika picha ya pamoja na wasaidizi wao baada ya kufanya mazungumzo. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula (kulia) akiwa katika mazungumzo na Rais na Mtendaji Mkuu wa Care International, Bi. Michelle Nunn huku maafisa walio chini yao wakifuatilia mazungumzo hayo. |
Serikali za Tanzania na Cuba zipo katika mchakato wa kupanua kiwanda cha Labiofam kilichopo Kibaha, Pwani cha kuzalisha viuadudu vya mazalia ya mbu ili kiwe na uwezo wa kuzalisha mbolea na dawa nyingine za kuua wadudu waharibifu wa mazao ya kilimo.
Hayo
yamesemwa leo tarehe 12 Julai 2022 jijini Dar Es Salaam na Naibu Katibu Mkuu wa
Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt Grace Magembe wakati wa ufunguzi wa kikao kati ya
Serikali za Tanzania na Cuba cha kujadiliana kuhusu upanuzi wa kiwanda hicho
kinachoendeshwa kwa ubia baina ya Serikali hizo mbili.
Dkt.
Magembe ambaye ni kiongozi wa ujumbe wa Tanzania unaojadiliana na ujumbe wa
Cuba, alisema kuwa ana matumaini makubwa katika kikao hicho cha siku mbili,
wajumbe watafikia makubaliano yatakayokuwa na manufaa kwa wananchi wa pande
zote mbili.
“Kama
unavyofahamu asilimia 70 hadi 80 ya Watanzania ni wakulima, hivyo, uwepo wa kiwanda
hiki na uzalishaji wa mbolea na viuadudu ni fursa nzuri kwa wakulima wetu na nchi
kuendeleza sekta ya kilimo pamoja na wananchi kujipatia kipato kwa mazao watakayovuna”,
Dkt. Magembe alisema.
Kwa
upande wake kiongozi wa ujumbe wa Cuba ambaye ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa
Kimataifa kutoka Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo, Bw. Orlando Diaz Rodriguez
alisema kuwa uwepo wa kiwanda hicho ni ishara ya wazi ya uhusiano mzuri uliopo
kati ya Cuba na Tanzania.
Aidha,
naye alielezea matumaini yake kuwa majadiliano hayo ya siku mbili yatakuwa na
faida kubwa kwa maendeleo ya sekta ya kilimo ya Tanzania na azma ya Serikali ya
kupamabana na ugonjwa wa malaria na hatimaye kuuangamiza kabisa.
Wataalamu wa Tanzania wanaoshiriki kikao cha majadiliano kati ya Tanzania na Cuba kuhusu upanuzi wa kiwanda cha LABIOFAM kinachoendeshwa kwa ubia kati ya Cuba na Tanzania |
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Dkt Grace Magembe (katikati), Kiongozi wa ujumbe wa Cuba ambaye ni Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa kutoka Wizara ya Kilimo ya nchi hiyo, Bw. Orlando Diaz Rodriguez (kulia) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), Dkt. Nicolous Shombe wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania na Cuba unaofanya majadiliano kuhusu upanuzi wa kiwanda cha LABIOFAM |