Shirika
lisilo la kiserikali la Care International limetakiwa kupanua huduma zake katika
mikoa mingi zaidi badala ya mikoa tisa tu ambayo shirika hilo kwa sasa linatoa
huduma zake hapa nchini.
Wito huo umetolewa
leo tarehe 13 Julai 2022 jijini Dar Es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula, wakati wa mazungumzo
yake na Rais na Mtendaji Mkuu wa Shirika hilo, Bi. Michelle Nunn
Bi. Nunn
ametaja baadhi ya shughuli ambazo shirika lake inazifanya hapa nchini kuwa ni pamoja
na utunzaji wa mazingira, afya, elimu, kuwawezesha wanawake kiuchumi, kilimo,
haki za kijamii na usawa wa kijinisa. Amesema utekelezaji wa shughuli hizo umezingatia
kipaumbele cha mwanamke.
“Tunasaidia
watoto wa maeneo ya vijijini kupata elimu bora, tunasaidia jamii kutumia aridhi
yao vizuri ili izalishe chakula, wakati huo huo ikitunzwa vizuri na programu zetu
za kutoa mikopo na kuwasaidia wanawake wa vijijini kujiwekea akiba kwa kutumia
teknolojia ya kisasa ya kidigitali zimewawezesha wanawake wengi kumiliki rasilimali
na kunyanyuka kiuchumi”, Alisema Bi. Nunn.
Kwa upande
wake, Balozi Mulamula alilishukuru shirika hilo kwa misaada inayotoa nchini na
kueleza kuwa programu zao za misaada zinaenda sanjari na dira ya maendeleo ya
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Aliendelea kueleza
kuwa changamoto kwa wanawake ni nyingi zikiwemo za afya ya uzazi na ugonjwa wa
malaria ambao bado unakatisha maisha ya watu wengi katika nchi za Afrika, hivyo
alishauri umuhimu wa “Care International” kuangalia kwa jicho la pekee eneo
hilo.
Aidha,
Balozi Mulamula alilipongeza shirika hilo kwa kujikita katika utunzaji wa
mazingira kwa kuwa tatizo hilo ni kubwa na watu wengi hawalioni, ingawa madhara
ya uharibifu wa mazingira yanamfikia kila mmoja wetu. |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.