Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk N.
Mbarouk amesema kuwa Wizara pamoja na balozi zake, itaendelea kuhamasisha nchi
marafiki na mashirika ya kimataifa kushiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara
(Sabasaba) ambayo amesema yanazidi kuimarika ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Kauli
hiyo ameitoa leo tarehe 08 Julai 2022 alipotembelea maonesho hayo yanayofanyika
kwenye viwanja vya Julius Nyerere, barabara ya Kilwa jijini Dar Es Salaam.
Balozi
Mbarouk amesema kuwa kushiriki kwa wageni wengi kutoka nje ya nchi, kuna faida
kubwa kwa wafanyabiashara wa hapa nyumbani, kwa kuwa kuna wapa fursa ya
kujifunza teknolojia mpya, kupata masoko ya bidhaa wanazozizalisha na wabia wa
kushirikiana nao katika biashara na uwekezaji.
Akiwa
kwenye viwanja hivyo, Mhe. Naibu Waziri alitembelea mabanda mbalimbali ya
washiriki wa maonesho hayo, hususan wale wa kutoka nje ya nchi ili kujionea
bidhaa, huduma na teknolojia walizokuja nazo. Katika maongezi na washiriki hao
alisisitiza umuhimu wa kubadilishana teknolojia na uzoefu na wafanyabiashara wa
hapa nchini ili kujenga uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zitakazokuwa na uwezo wa
kukabili ushindani wa soko la dunia.
Katibu
Mkuu wa Wizara hiyo, Balozi Joseph Sokoine aliahidi kuwa Wizara yake
itashirikiana na wadau wengine kama Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara (TANTRADE)
na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara kuhakikisha kuwa wafanyabiashara
wengi zaidi kutoka nje ya nchi wanashiriki maonesho hayo. “Wizara yetu ni mdau mkubwa
katika utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi na maonesho ni jukwaa muhimu katika
diplomasia ya uchumi, hivyo tutaongeza nguvu zaidi kushajihisha kampuni nyingi
zaidi kutoka nje, zishiriki maonesho haya mwakani na miaka mingine”, Alisema
Balozi Sokoine.
Maonesho
ya Biashara ya Kimataifa ya mwaka 2022 yalianza tarehe 28 Juni na yanatarajiwa
kuhitimishwa tarehe 13 Julai 2022 ambapo nchi 20 zinashiriki kwa kuoenesha
bidhaa, huduma na teknolojia mbalimbali. |
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Bnada la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba). Aliyesimama ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga.
|
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akipewa maelezo kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga. |
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa katika moja ya banda yaliyopo kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) |
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisikiliza maelezo ya mshiriki wa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kutoka nje ya nchi |
|
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) |
KATIBU MKUU KATIKA MAONESHO YA SABASABA |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwa kwenye viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) kwa ajili ya kutembelea mabanda mbalimbali kujionea bidhaa, huduma na teknolojia.. |
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili katika Bnada la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba).
|
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akipewa maelezo kuhusu ushiriki wa Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba) na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga. |
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akisalimiana na Balozi wa Marekani hapa nchini ambaye alifika kutembelea |
Bnada la Wizara ya Mambo ya Nje lilipo katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba). |
|
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Joseph Sokoine akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Biashara (Sabasaba |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.