Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula
amekutana na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani
wanaofundisha na kusoma vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa
ziara ya kikazi hadi tarehe 17 Julai 2022.
Ziara
hiyo iliyoratibiwa na Mtanzania-Diaspora, Bi Zawadi Sakapala ambaye ni mmiliki
wa kituo cha “Community Centre” kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam inalenga
pamoja na mambo mngine, kutoa fursa kwa wanafunzi hao kujifunza masuala ya
utamaduni wa Tanzania na kubadilishana ujuzi na uzoefu katika masomo ya
sayansi, ufundi, ufundishaji na Usimamizi wa watoto wadogo (daycare).
Katika
kikao hicho, Bi Zawadi alimfahamisha Mhe. Balozi Mulamula kuwa kituo chake
kimekuwa kikishirikiana na vyuo vikuu mbalimbali nchini Marekani kuratibu ziara
za walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani kutembelea nchi za
Afrika kwa ajili ya kubadilishana uzoefu katika sekta ya elimu.
Hivyo,
ili kuimarisha sekta ya elimu katika nchi za Afrika, kikao hicho kiliazimia
kuongeza jitihada za kuhamasisha Waafrika wengi zaidi kujiunga na vyuo vya
Marekani, kuunganisha vyuo vya Afrika na Marekani, wanafunzi-Watanzania wanaopata
fursa ya kusoma Marekani, watumike kufundisha lugha ya Kiswahili ikiwa ni moja
ya njia ya kueneza lugha hiyo duniani pamoja na kwahimiza watu wenye asili ya
Afrika kutumia elimu, ujuzi na maarifa waliyopata wakiwa ughaibuni kuinua jamii
za nchi za Afrika.
Wakati
huo huo, Balozi Mulamula amekutana na Ujumbe wa Shirika la Umoja wa Mataifa la
Programu ya Maendeleo (UNDP) ambao upo nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo
na wadau wa siasa ili kubainisha maeneo ambayo, shirika hilo linaweza kusaidia
katika uendeshaji wa uchaguzi mkuu ujao.
Ujumbe
huo unaongozwa na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani
ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola umefanikiwa kufanya vikao na wadau
mbalimbali ikiwa ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi, wawakilishi wa vyama
vya siasa na asasi za kiraia, umepokea maoni ya wadau hao ya maoneo yanayohitaji
msaada na umeahidi utayafanyia kazi kikamilifu. Maeneo hayo ni pamoja na uelimishaji
wa wapiga kura, msaada wa kiufundi katika upigaji na uandikishwaji wa wapiga
kura na teknolojia ya mawasiliano wakati zoezi la uchaguzi.
Kwa
upande wake, Balozi Mulamula aliueleza ujumbe huo kuwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kipindi kifupi cha
uongozi wake ameonesha dhamira ya dhati ya kuboresha mazingira ya kisiasa
nchini, kwa kuhamasisha majadiliano ya kisiasa, ushirikishwaji wa wadau wote,
umoja na mshikamano wa kitaifa. Hivyo, aliuhakikishia ujumbe huo kuwa uchaguzi
ujao utaendelea kuwa huru, haki na amani kama ilivyo desturi ya Tanzania. |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani (hawapo pichani) wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani ambao wapo nchini kwa ziara maalum hadi tarehe 17 Julai 2022. |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimsikiliza mmoja wa mwanafunzi anayesoma katika vyuo vikuu vya Marekani kuhusu mikakati ya kusaidia vijana wa Afrika kupata elimu bora itakayoweza kukabili mazingira ya dunia ya sasa. |
|
Mhitimu wa Shahada ya Uzamivu kutoka Chuo Kikuu cha Howard cha nchini Marekani ambaye pia ni Kiongozi wa Taasisi ya 3GC Inc. akieleza shughuli za taasisi hiyo zinazolenga kuwasaidia vijana wa Afrika |
|
Mkurugenzi wa Kitengo cha Diaspora katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi James Bwana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Balozi Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimvisha scurf ya bendera ya Tanzania, mmiliki wa kituo cha “Community Centre”
kilichopo Kijichi jijini Dar Es Salaam, Bi. Zawadi Sakapala |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na walimu na wanafunzi wenye asili ya Afrika na Marekani wanaosoma na kufundisha vyuo mbalimbali vya Marekani |
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA AFISA UCHAGUZI MKUU WA UN
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na
Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
|
Baadhi ya ujumbe uliongozana na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa, Bw. Akinyemi Adegbola kwenye mazungumzo ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula na Afisa huyo. |
|
Ujumbe wa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ukifuatilia mazungumzo yake na Afisa Uchaguzi Mkuu katika Idara ya Siasa na Masuala ya Amani ya Umoja wa Mataifa |
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiagana na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi.
|
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa UNDP ambao upo nchini kwa ajili ya kuzungumza na wadau wa siasa kuhusu uchaguzi.
|
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA MWAKILISHI MKAZI WA UN WOMEN
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa UN Women, Bi. Hodan Addou kwenye Hoteli ya Seana jinini Dar Es Salaam.
|
BALOZI MULAMULA AKUTANA NA BALOZI MTEULE LT. JEN. MATHEW EDWARD MKINGULE
|
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushiikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiwa na Balozi Mteule Lt. Jen. Mathew Edward Mkingule baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika jijini Dar Es Salaam |
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.