Thursday, July 7, 2022

UONGOZI WA CCM MKOANI KAGERA WAPONGEZA UTENDAJI WA WAZIRI MULAMULA

Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera wamempongeza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya ya kuimarisha Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Mataifa mengine ulimwenguni sambamba na kutekeleza vyema diplomasia ya uchumi. 

Haya yamesemwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costansia Guhiye wakati wa mazungumzo yaliyofanyika baina ya Viongozi wa Chama wa Mkoa huo na Waziri Mulamula alipotembelea Ofisi Kuu ya Chama Mkoa wa Kagera mjini Bukoba.

Katika mazungumzo hayo Waziri Mulamula alitoa rai kwa viongozi hao kuendelea kuwahamasisha na kuwahimiza wananchi wa Mkoa wa Kagera kuchangamkia fursa zinazopatika katika Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kama vile biashara na fursa za kufundisha Kiswahili zinazopatikana katika Nchi wanachama wa Jumuiya. 

Sambamba na hayo Waziri Mulamula amepongeza jitihada zinazofanywa na viongozi hao katika kulea na kukuza Chama, kuhamasisha amani, maendeleo, umoja na mshikamano kwa wananchi wa Mkoa huo. Aidha amewatakia maandalizi mema ya uchaguzi wa Chama unaotarajiwa kufanyika katika siku za usoni. 

Waziri Mulamula amewasili Mkoani Kagera leo tarehe 7 Julai 2022 ambapo anatarijiwa kuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya kilekile cha Monesho ya Bukoba “Bukoba Expo” tarehe 8 Julai 2022 yanayofanyika katika viwanja vya CCM mjini humo. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akizungumza na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera 
Kuotaka kushoto, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costansia Guhiye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula na Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Ndugu Christopher Paranjo wakifurahia jambo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa CCM Mkoa wa Kagera.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kagera 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Bi. Costansia Guhiye akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo baina ya Uongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Kagera na Waziri Mulamula
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula (kulia) akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Ofisi Kuu ya Chama Mkoa wa Kagera mjini Bukoba
Katibu wa CCM Mkoa wa Kagera Ndugu Christopher Paranjo akielezea jambo wakati wa mazungumzo baina ya Uongozi wa Chama cha Mapinduzi wa Mkoa huo na Waziri Mulamula

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.